ONYO kwa wanaonunua simu humu

Kuwasaidia wengine, mtaje. Sisi tutaangalia IDs zake zote na kuziunganisha.

Ikibidi, tupe # yake ya simu tutamwanika hadi majina halisi. Threads zake zote zitafutwa na ID itawekewa status ya TAPELI.

Thanks
Invisible sikiliza na upande wa pili ili kubalance story then ufanye maamuzi yatakayokua na tija kwetu sote hapa JF. Halafu njia aliyotumia jamaa ya kuanika namba yake hadharani ili hali Mshitakiwa hajasikilizwa mimi naona sio sahihi...alipaswa aku-PM hiyo namba kwanza. Hayo ndio maoni yangu.

Utapeli sio mzuri washikaji, kwani wengine hapa tunaweza kua na shida kweli na tukataka kuuza SAMANI zetu lakini tukashindwa kwakua tayari baadhi ya watu wameshachafua hali ya hewa. UTAPELI sio mzuri ndugu zangu, kama mnafanya muache!
 
ndo maana uzi ukawa sticky kwa sababu utapeli haufai na tapeli ukimstukia inakula kwako tu..
 
PICHA LILIKUWA HIVI:
nimekuta tangazo la BB CURVE inauzwa kwa 100k,
kwa sifa zilizowekwa nikawa interested.
Nikamtafuta jamaa ili ninunue simu,
akanambia nimfate kwao TABATA,
kwakuwa mimi naishi SINZA nikamwambia tukutane UBUNGO TERMINAL ili kushare cost.....
Jamaa akafika eneo husika akiwa na bidhaa husika ikiwa ipo ON tayari!
Kama ilivyo kwa mtoto wa mjini mwingine sikutaka kuuziwa mbuzi kwenye kiroba nikaizima na kuiwasha simu,
yan process ya kuwasha tu ilichukua dk10 na charge ikawa imeisha hapohapo hivyo simu ikazima zzzzzz....!
(Kimoyomoyo nikasema biashara hakuna hapa)
MUUZAJI:(kwa kujistukia)dah..!ndo kawaida ya BB ukiwasha inaload sana na sijaichaj toka juz

MNUNUZI: sasa kwanini hukuichaj full leo na unajua toka jana kama kuna biashara?kwnza vitu vyake viko wapi?(charger&earphone)

MUUZAJI: ah!nilijisahau kuichaj ila charger ilipotea mi huwa naazima ya samsung

MNUNUZI: dah!sasa hapo itabidi katika hiyo pesa nitakayokupa itakayokupa itabidi ipungue ninunue charger

MUUZAJI: sawa haina shida,

MNUNUZI: sasa wewe nenda kachaj full,alafu tukutane hapahapa badae sawa?
(tukakubaliana akaondoka,akajua kashaula tayari)
ilipofika badae

MUUZAJI: tayari iko poa hii hapa mkubwa

MNUNUZI: ok!nikaizima nikaweka line yangu na memory card,
simu ilipowashwa ikakata display
(jamaa akawa anaiweka kwa kufichaficha inaelekea ndo tatizo la hyo simu)

MUUZAJI: (baada ya kuhangaika sana bila mafanikio,huku akinichek kwa jicho la wizi)
dah!yan tatizo hili ndo kwanza linantokea leo,itakuwaje mkuu?

MNUNUZI: nakusikiliza wewe unasemaje?

MUUZAJI: mi naona biashara ishakuwa ngumu hapa.

MNUNUZI: kama umelitambua hilo vizuri,
kajipange upya ukiwa na simu nzuri,nzima nitafute()

Tumekusikia mkuu, maelezo yako nasi tume ya record....Upande wa pili nae aitwe aje kutoa maelezo yake.
 
wewe umekutana na mzinguaji mmoja unahukumu wauzaji wote......mimi nishauzia watu humu vitu vingi tu na wananipm kuappreciate.....sasa hivi nauza iPHONE 4S brand new....boxed na accessories zote njoo ni-pm ununue na uje utoe feedback hapa....hata sisi wauzaji kuna wanunuzi tunagongana na wayeyushaji wengi tu lakini ni sehemu ya biashara...

Mkuu itabidi sasa mambo yote yafanyike hapa Ukumbini....weka bei mkuu ili itutie tamaa kama tunaweza kuinunua au la?
 
Kweli kuna watu wanaharibu biashara za watu wa kweli kwa kuuza simu mbovu
 
Pole sana mkuu kwa utapeli ila nataka niwashauri wote kuwa kama una uwezo hata siku moja vitu vy aelectronics uwe unanunua vipya tu. Kwa mfano simu na laptop pia vinakuwa vya wizi kwa baadhi ya wauzaji. Sioni ni kwa nini siku moja unakamatwa mwizi kwa mali uliyouziwa na mwizi. Pia kama umekubaliana na ununuzi wa mitaani maana hakuna hata ofisi basi uhakikishe unapafahamu nyumbani kwa muuzaji na kiongozi wake wa serikali za mitaa na mjumbe. Be careful, online wezi na matapeli wako wengi sana siku hizi.
 
Kumekuwa na matangazo mengi sana yahusuyo mauzo ya simu na vitu vingine,
ila mimi nitaongelea zaidi kwenye simu,
simu nyingi zinazouzwa humu ni vimeo utakuta mtu anajua kimeo kinaelekea kumfia anakitupia huku,
juzi kuna jfmember nusu nimpeleke polisi kama si huruma iliyonijia ghafla,

wengi wanauza vimeo vilivyoshindikana au cm za kuungaunga kwa mafundi!
USHAURI:Tuache uvivu twende madukani,simu mpya na guarantee bei rahisi,tupunguze tamaa za kupata vitu vizuri kwa bei za kutupa

kijana ndo kwanza umeingia JF siku moja tu ushapiga majanga??

Join Date : 5th June 2012
Posts : 82
Rep Power : 369
Likes Received: 18

Likes Given 0

hebu cheki hii profile yako nahisi we nae mwizi
 
kijana ndo kwanza umeingia JF siku moja tu ushapiga majanga??

Join Date : 5th June 2012
Posts : 82
Rep Power : 369
Likes Received: 18

Likes Given 0

hebu cheki hii profile yako nahisi we nae mwizi

soma vizuri mkuu hiyo tarehe..
 
wewe umekutana na mzinguaji mmoja unahukumu wauzaji wote......mimi nishauzia watu humu vitu vingi tu na wananipm kuappreciate.....sasa hivi nauza iPHONE 4S brand new....boxed na accessories zote njoo ni-pm ununue na uje utoe feedback hapa....hata sisi wauzaji kuna wanunuzi tunagongana na wayeyushaji wengi tu lakini ni sehemu ya biashara...
Unauzaje hiyo iPHONE 4S?
 
rekebisha usemi kuna wauza simu humu wana maduka yao kama Godfrey Electronics sasa wewe unapotoa onyo sielewi
Hapa kila mtu kakomaa akili akiona simu akaipenda humu anawasiliana muuzaji anaiona face yake akiridhika ndo analipa

usitaku ku implant spirit mbaya kwa watu

pia hii ni sehemu ya biashara sana so ktk soko au market place mambo kama hayo hayakosi ni wewe tu kuangalia wapi kuna ukweli na uhakika

Hope nimeeleweka na sitaki tangazo hili likutwe na wageni sababu litachafua jukwaa kwa mambo ambayo yanaitaji umakini wa mnunuaji

Uwezi enda duka la vifaa used ukakurupuka kununua kitu
pia kama ujui hili soma sticky hapo juu kaweka robot inayotutahadharisha na haya yote

Lidumu jukwaa la matangazo

huyo mtu uliyemtaja hapo juu (Godfrey electronics) ni brother ninayemuheshim sana,
yupo makini na biashara zake na anajiamini,kikubwa anafanya hyo biashara kama kazi,kwani ana bidhaa nyingi na zinaonekana kila mahali(fb,mnada.com na kwingneko) na simu zake ni mpyaaaaaa...na kikubwa matangazo yake yanakamilika huna haja ya maswali kwa huyu jamaa
Naweza sema yeye pekee ndiye anastahili kupewa sifa kwa hili,
japo anafanya ONLINE BUSNESS na hana duka ila namkubali sana.
Ninaoongelea hapa ni wale wa simu moja moja na matangazo yasiyo na tija mtu anaweka tangazo halikamiliki,
huoni SPECIFICATION za bidhaa anakwambia google,picha haweki,
bei hawek anakwambia um-PM,
MI NAONA TANGAZO LISILOKAMILIKA MODS WALIFUTE LISIWEPO HEWANI!
wewe unayesema hutaki kuiona thread hii unanpa wakati mgumu kukuelewa ndugu,
"look your self"
 
Last edited by a moderator:
kijana ndo kwanza umeingia JF siku moja tu ushapiga majanga??

Join Date : 5th June 2012
Posts : 82
Rep Power : 369
Likes Received: 18

Likes Given 0

hebu cheki hii profile yako nahisi we nae mwizi

tabulalasa
 
Umekoswa koswa kupitiwa na kimbunga shukuru unakaujanja kidogo
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Kweli kuna watu wanaharibu biashara za watu wa kweli kwa kuuza simu mbovu

ni dhahiri ndugu yangu,penye wengi pana mengi wapo waaminifu wapo pia wasio waaminifu hatuwezi kufanana daima tupo kama vidole,
dawa ni kuwaanika ili wajulikane jukwaa libaki safi!
TANZANIA BILA UFISADI NI NGUMU KIDOGO
ILA
JF BILA MATAPELI INAWEZEKANA KABISA
 
Invisible sikiliza na upande wa pili ili kubalance story then ufanye maamuzi yatakayokua na tija kwetu sote hapa JF. Halafu njia aliyotumia jamaa ya kuanika namba yake hadharani ili hali Mshitakiwa hajasikilizwa mimi naona sio sahihi...alipaswa aku-PM hiyo namba kwanza. Hayo ndio maoni yangu.

Utapeli sio mzuri washikaji, kwani wengine hapa tunaweza kua na shida kweli na tukataka kuuza SAMANI zetu lakini tukashindwa kwakua tayari baadhi ya watu wameshachafua hali ya hewa. UTAPELI sio mzuri ndugu zangu, kama mnafanya muache!

namba haijawekwa hadharani mkuu!
Thanks
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom