ONYO: Ubungo Darajani kuna wezi balaa

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Habari za siku Mingi ?

Leo nilikua pale ubungo darajani stand,maeneo haya ni maeneo yangu ya kujidai kabisa toka 2006 napajua ubungo vizuri na washenzi wote wa pale tena enzi za Hamidu mzawa.

Leo naomba nikujulishe wewe mtanzania unaetumia kituo kile ni kwamba kimejaa wasafiri wengi feki,kuna vijana kama thelathini wao hushinda pale kama wasafiri kumbe ni wezi tu,na huwa wana vibegi mgongoni kazi yao kubwa ni kuiba tu.

Kama wewe ni mtumiaji wa eneo hilo kuwa makini sana.Leo nilikaa pale Masaa matatu nikaona walivyo na network yao kubwa.

Kuweni makini.ukifika pale angalia vijana waliovaa mabegi mgongoni wanapokimbikia gari huwa hawapandi.

Yang hayo.

Zubedayo_mchuzi MZEE kutembea mpk chalinze.
 
"ulikaa pale masaa 3"?

Uliwaona wezi wanavibegi mgongoni wanapokimbilia gari huwa hawapandi!!!

Hapa mimi napata mshangao, watu waliopita leo darajani wakienda nakurudi wakikuona umekaa kwa muda wa Masaa 3 watakufirikiaje?

Sasa wewe na wale waobeba vibegi mgongoni japo wanakimbilia gari na hawapandi ninani kati yenu atakuwa mshukiwa?
 
Kweli mkuu pale ubungo kwanza wavuta bangi na mateja wamejaa. Me niliibiwa simu mwaka JUZI
 
Tunasubiri Tamko. Ngoja Makonda aamke toka usingizini.
 
Hivi ni kusema ukweli njia za kudhibiti vibaka zimeshindikana kabisaaaaa???? Ni askar wachache ama sio kipao mbele....hata pale bugurun usiku nyuma ya daraja pale kote hadi tazara utaona vijana wanapita katikati ya tuta lile la barabara wakijifanya wanatembea kwa miguu baada ya kuona kuna traffic jam...kumbe lah sio watembea kwa miguu ila wanaangalia gari lipi ahlijafunga vioo wapokonye simu...pale kuna follen ya hatar jion hivyo watu huzima magari na kushusha viooo wapate upepo aiseee take care with zero seconds huna simu mkononi.
 
Sasa nyinyi mlitusema wanaume wa Dasalamu tunaogopa panya road. Kumbe ya nyinyi mnaogopa wizi wa Ubungo


Ndukiiiii
 
Kile kituo ni hatari...ukifika pale usijisahau...umust be active..kama gari imejaa usipande.otherwise utaumia
 
"ulikaa pale masaa 3"?

Uliwaona wezi wanavibegi mgongoni wanapokimbilia gari huwa hawapandi!!!

Hapa mimi napata mshangao, watu waliopita leo darajani wakienda nakurudi wakikuona umekaa kwa muda wa Masaa 3 watakufirikiaje?

Sasa wewe na wale waobeba vibegi mgongoni japo wanakimbilia gari na hawapandi ninani kati yenu atakuwa mshukiwa?
Mkuu masaa 3 yangu pale yalikua na kitu nachotafuta,ila kama upo dar kama si wewe basis hata mdogo ataingia mikononi mwao siku moja...yangu taarifa tu
 
Pâle uwizi ndiyo asili yake na kamwe hauwezi kuisha....

OVA
 
Mnajuwa kazi ya vile vibegi? Kazi yake ukiwa umekaa kwenye siti ukawa makini utaona wanaume wengi huweka pesa mfuko wa nyuma hivyo basi lile begi hujifanya kukuwekea pale matakoni na kujifanya kabanwa huku likiwakinga abiria wasione mkono wake unavyo kuchomolea pesa makonda wengi wanawafahamu waungwana huwafukuza wengine ni sehemu ya michongo hiyo kuweni makini mnapopanda DALADALA lilojaa kupita kiasi
 
Umenikumbusha mkuu, kuna siku nilishuhudia watu wanaporwa hapohapo kituoni halaf wezi wanashuka kule chini darajani!
Nilishawah kuwapgia hata polisi simu na aliyekua mkuu wao kabla ya huyu aliyepo ,walijaribu kuwasafisha sasa naonda njaa imewarudidha tena!
Lile eneo pamoja na pale darajani kama unaenda chuo(kituo cha zamani cha chuo) na pale kwenye njia ya kuingilia mawasiliano ni hatar sana kuanzia saa moja usiku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom