Onyo na ushauri wa bure kwa Panya Road, ndugu na wazazi wao

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu zangu nimepata taarifa kutoka kwa baadhi ya ma homeboyz kwamba kuna baadhi ya vijana wa panya road wako katika process za kutaka kuikimbia nchi ili waje Kaburu kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.

Inasemekana kuwa kuna baadhi ya wazazi sasa hivi wako katika harakati za kuuza viwanja, vitu vya ndani nk ili wapate pesa ya kuwatorosha watoto wao wanaosakwa usiku na mchana na vyombo vya dola kwa sababu ya tuhuma za kuvamia nyumba za watu usiku, kuiba, kujeruhi na wengine kuuwa.

Ushauri wangu kwa vijana hao na wazazi wao, ni kwamba wasijaribu kufanya hicho wanachotaka kufanya, maana kitakachowakuta huku kitaleta majuto makubwa kwao na kwa wazazi wao.
Kaburu sio nchi ya kufanyia mzaha, hapa kila mtu katoboka roho kwahiyo kuuwa au kuuwawa ni jambo la kawaida.

Kuna vijana wengi tu kutoka Mbagala, Vingunguti, Buguruni, Temeke, Mburahati, mw/nyamala nk walikimbia kesi mbali mbali ila walipofika hapa baada ya muda mchache wazazi wao walirudishiwa maiti wazike. Wizi wa kijinga jinga kama vile Dar hapa hauna nafasi. Yes unaweza kutumia bisibisi kufanya uhalifu wako lkn ukiotewa hakuna mswalie mtume, unatafutwa kimya kimya, na baada ya muda watu wanasikia kuna mbongo kapigwa risasi kwenye robot (trafik light) fulani na muuaji hajakamatwa na kamwe hatokamatwa.

Kwahiyo mnaofikiria kuwa mkikwepa mkono wa sheria na kukimbilia huku kutawafaa naomba mbadilishe mawazo, maana mtakuwa mmekifuata kifo wenyewe. Maana najua mkifika hapa mtakuwa hamna shughuli nyingine ya kufanya ili mjipatie riziki, wengi mtajiingiza kwenye makundi bila kujua madhara yake ya baadae mkizani kuwa hata hapa unaweza kuvamia nyumba ya mtu usiku kwa kutumia panga 😂😂😂😂 so mtapukutishwa kama punje za mahindi mashineni. Trust me what i say 🤞.
Msije kusema ma brother hatukuwaonya.

Kwa sasa nipo njiani naelekea Botswana kwahiyo nitakuwa naingia mara moja moja kusoma na hata ku reply comments mbali mbali.

Asanteni.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu zangu nimepata taarifa kutoka kwa baadhi ya ma homeboyz kwamba kuna baadhi ya vijana wa panya road wako katika process za kutaka kuikimbia nchi ili waje Kaburu kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.

Inasemekana kuwa kuna baadhi ya wazazi sasa hivi wako katika harakati za kuuza viwanja, vitu vya ndani nk ili wapate pesa ya kuwatorosha watoto wao wanaosakwa usiku na mchana na vyombo vya dola kwa sababu ya tuhuma za kuvamia nyumba za watu usiku, kuiba, kujeruhi na wengine kuuwa.

Ushauri wangu kwa vijana hao na wazazi wao, ni kwamba wasijaribu kufanya hicho wanachotaka kufanya, maana kitakachowakuta huku kitaleta majuto makubwa kwao na kwa wazazi wao.
Kaburu sio nchi ya kufanyia mzaha, hapa kila mtu katoboka roho kwahiyo kuuwa au kuuwawa ni jambo la kawaida.

Kuna vijana wengi tu kutoka Mbagala, Vingunguti, Buguruni, Temeke, Mburahati, mw/nyamala nk walikimbia kesi mbali mbali ila walipofika hapa baada ya muda mchache wazazi wao walirudishiwa maiti wazike. Wizi wa kijinga jinga kama vile Dar hapa hauna nafasi. Yes unaweza kutumia bisibisi kufanya uhalifu wako lkn ukiotewa hakuna mswalie mtume, unatafutwa kimya kimya, na baada ya muda watu wanasikia kuna mbongo kapigwa risasi kwenye robot (trafik light) fulani na muuaji hajakamatwa na kamwe hatokamatwa.

Kwahiyo mnaofikiria kuwa mkikwepa mkono wa sheria na kukimbilia huku kutawafaa naomba mbadilishe mawazo, maana mtakuwa mmekifuata kifo wenyewe. Maana najua mkifika hapa mtakuwa hamna shughuli nyingine ya kufanya ili mjipatie riziki, wengi mtajiingiza kwenye makundi bila kujua madhara yake ya baadae mkizani kuwa hqtq hqpq unaweza kuvamia nyumba ya mtu usiku kwa kutumia panga 😂😂😂😂 so mtapukutishwa kama punje za mahindi mashineni. Trust me what i say 🤞.
Msije kusema ma brother hatukuwaonya.

Kwa sasa nipo njiani naelekea Botswana kwahiyo nitakuwa naingia mara moja moja kusoma na hata ku reply comments mbali mbali.

Asanteni.
 
Mzazi anayeuza kiwanja amtoroshe mtoto mhalifu toka kwenye mkono wa sheria anamuangamiza mwanae kwa mikono yake mwenyewe
Na kama ndivyo Huyu mzazi ni panya zaidi ya mwanae
Kweli kabisa. Mtoto au mtu yoyote akifanya uhalifu ni lazima aadhibiwe kwa uhalifu wake, sasa inapotokea mtu akatafuta njia au njama za kumtorosha muhalifu basi na yeye mtoroshaji moja kwa moja anakuwa ni muhalifu.
 
Back
Top Bottom