ONYO: Mitutu ya bunduki katika siasa na uvumilivu wa wananchi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ONYO: Mitutu ya bunduki katika siasa na uvumilivu wa wananchi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Nov 15, 2011.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,121
  Trophy Points: 280
  Hadi sasa tumeshuhudia utumiaji mkubwa wa nguvu kupita kiasi wa Polisi dhidi ya wananchi wa Tanzania. Ukweli ni kwamba Tanzania imefikia hatua ambayo inafadhaisha, inakera na inasikitisha sana. Wengi wetu tunajua vurugu na maandamano mengi ni matokea badala ya chimbuko la tatizo.

  Suala la msingi lililopo ni uongozi mbaya, mbaya kwa kadiri ambayo haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii. Ubovu wa uongozi unaanzia katika ngazi ya ofisi ya Raisi, mawaziri hadi ngazi za chini.

  Ni wazi uongozi wa juu ukiwa ovyo na wa chini utakuwa ovyo, na wananchi watatafuta haki zao kwa namna inayoeleza hasira yao. Kadiri Polisi wanavyoendelea kutumia nguvu badala ya akili, wanawafanya wananchi wazidi kuwa sugu, na itafikia mahali ambapo si maji ya kuwasha, wala mabomu ya machozi wala risasi za moto zitaweza kuzima vurugu na maandamano yanayoendelea sasa, katika kile wananchi wanachoona ni kudai haki zao za msingi. Hiki ndicho kilichotokea Tunisia, Misri, Libya na kinachoendelea Syria kwa sasa.

  Inafikia mahali ambapo wananchi wanaamua liwalo na liwe, hawajali kuuwawa. Angalia kwa mfano Spika anavyoendesha Bunge kuhusu mjadala wa Katiba. Maoni ya wananchi yanajulikana, sasa kwa kuwa maoni ya wananchi yanawasilishwa na kusemwa na wabunge wa upinzani Spika anayabeza. Hivi serikali inatarajia nini kitatokea? Hivi kweli viongozi wa Tanzania wamekosa busara na akili kiasi hiki? Yaani, utadhani tunaongozwa na watoto wa chekechea.

  Ninahofia sana kwamba amani tuliyojivunia kwa muda mrefu iko mbioni kutoweka. Nani alikuwa na askari wa kutisha na wanaoua wananchi hapa Afrika zaidi ya Ghadafi? Sasa yuko wapi yeye na askari wake waliokuwa wakitisha? Nani anajua kuua wananchi wanaoandamana kama Syria? Je vifo vya wananchi wa Syria vimefanikiwa kuzima maandamano na nguvu ya wanachi wa Syria kudai haki zao?

  Serikali kwa sasa inafanikiwa kulifanya kila jambo ambalo linapiganiwa haki nchini lionekane kama ni la Chadema. Ukweli wananchi wa Tanzania si wajinga kiasi hicho. Huu ni mchezo wa hatari kwa serikali, na bila kujua ukweli ni kwamba wanawafaidisha Chadema. Wamachinga walioandamana Mbeya hawakuwa watu wa Chadema pekee, lakini sasa wengi wamekuwa Chadema.

  Wanafunzi wa Chuo Kikuu waliopigwa na kudhalilishwa hawakuwa wa Chadema pekee, lakini sasa wengi wamekuwa Chadema. Katiba mpya si ya Chadema, lakini serikali bila kufikiria na kutumia akili inataka kufanya Katiba mpya liwe suala la Chadema. Licha ya hivi, kuna wakati wananchi wataamua kuweka U-Chadema, U-CCM pembeni, na hapo ndipo tutaona kwamba inafikia wakati mwanadamu yeyote anaamua kifo si muhimu zaidi ya kutimiziwa haki zake za msingi. Hatuko mbali sana na hapo. Ni jambo ndogo sana litachochea hali kama hii; kwa mfano ukweli ni kwamba serikali kwa sasa imeishiwa fedha vibaya sana, hata mishahara hailipwi kikamilifu na huduma nyingi za jamii hazina fedha za kutosha.

  Hili ndio linaweza kuwa kichocheo au "catalyst" au "critical mass" ya kuwaunganisha wananchi, wa CCM, Chadema, NCCR, UDP nk, dhidi ya serikali katika hali ambayo haijawahi kutokea Tanzania. Mind you, kwa jinsi uongozi wa sasa wa nchi usivyo popular na Jeshi la Wananchi, ni wazi jeshi hilo litaegemea upande wa wananchi, maana kwao itakuwa ni sababu muafaka ya kuleta mabadiliko kwa namna ambayo Jumuiya ya Kimataifa haitawalaumu kukiuka misingi ya demokrasia - kama tu ilivyokuwa Misri.

  Mie yangu macho. Sijui wana Jamii mnaonaje hili.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Umesema ukweli kabisa na huu ndio ukweli utakaosimama milele
   
 3. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,121
  Trophy Points: 280
  Bwana wee. mie nashikwa na hasira juu y viongozi wetu ambayo siwezi hata kuielezea. Sasa naelewa kwa nini watu huwa wanaamua kuingia msituni.
   
Loading...