Onyo Madini kuwekwa Nyumbani bila Nyaraka

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Arusha



Waziri wa Madini,Doto Biteko amewataka wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite katika Mikoa ya Arusha na Manyara kuacha mara moja kuweka madini ya Tanzanite majumbani bila ya kuwa na nyaraka yoyote ya serikali iliyomuidhinisha kumiliki vinginevyo madini hayo yatataifishwa na serikali na ikiwa ni pamoja na mtuhumiwa kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi.



Biteko alitoa onyo hiloJijini Arusha katika hotel ya kitalii ya Mount Meru wakati akizungumza na wafanyabiashara wakubwa,kati na wadogo wa madini ya Tanzanite ,wamiliki wa migodi,wachimbaji wakubwa na wadogo,viongozi wa vyama vya madini ,wakuu idara zote za serikali Mkoani Arusha na watendaji wa idara zote za Wizara ya Madini katika Mkutano ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ili wafanyabiashara hao waweze kueleza changamoto katika biashara hiyo kwa Waziri.



Waziri Biteko amesema kukutwa na madini ya Tanzanite nyumbani wakati huna nyaraka yoyote ya serikali inayoonyesha kuwa madini hayo ni mali yako utakuwa umefanya kosa kisheria kwani madini hayo ulikuwa na lengo ovu hivyo madini hayo yatataifishwa na mhusika utachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi.



Alisema kuwa serikali inataka kila mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite na madini mengine kuuza madini yake katika masoko yaliyotengwa na serikali na sio vinginevyo na kuwa na madini nyumbani kinyume na utaratibu ni kuihujumu serikali na hilo halitavumiliwa kamwe.



Waziri alisema kuwa iwapo mfanyabiashara atakwenda katika soko la madini na madini yake kwa bahati mbaya bei haikufika kama alivyopanga anapaswa kupewa nyaraka inayomruhusu kumiliki madini hayo na afisa madini aliyepo katika soko hilo na kamwe hatasumbuliwa pindi atakapokuwa nayo nyumbani.




Akizungumzia minada wa madini Tanzanite iliyokuwa ikifanyika katika miaka ya nyuma Jijini Arusha ,Waziri Biteko alisema serikali inaweza kuruhusu kufanyika kwa minada kwa utaratibu mzuri na sio ule wa kiini macho na ujanja ujanja uliokuwa ukifanyika katika miaka ya nyuma

Naye Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Ajira,Vijana na Ulemavu,Antony Mavunde aliwataka wafanyabiashara wa Tanzanite kuacha mara moja kutumia watu wa kati katika kutafuta vibali vya kufanya kazi kwa baadhi ya wafanyakazi wao kutoka nje ya nchi.



Alisema kufanya hivyo ni kupoteza pesa na kuchelewa kupata kibali kwani kibali huchukuwa muda wa siku 21 tu na sio vinginevyo hivyo mlango uko wazi kwa kila mfanyabiashara kuhakikisha anafuata sheria.



Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wauzaji madini Wakubwa Nchini{TAMIDA} Thomas Munis alisema kuwa wafanyabiashara hao kwa sasa wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa ikilinganishwa na hapo awali ambapo kulikua na na kero ya tozo mbali mbali kwa wafanya biashara Wa Madini ya Tanzanite .

Munisi alisema wao kama viongozi Wa kitaifa wataakikisha wanatembea nchi nzima kuongea na wafanya biashara Wa Madini kueshimu sheria za uzaji Wa madini kwani Mh Rais amepunguza kodi na sasa wanafanya biashara bila kuwepo na vikwazo vya utitiri Wa Kodi na pia wanasikilizwa wakiwa na mamalamiko yoyote juu ya biashara ya Madini lakini kuna wachache wanatoka Nje ya sheria kuuza Madini Nje ya nchi bila utaratibu .


Alisema TAMIDA iko mstari wa mbele kulipa kodi ya serikali kwa maendeleo ya nchi na Rais ameonyesha maendeleo makubwa kutumia fedha za ndani kuimarisha Sekta ya Elimu kwa kutoa Elimu bure pamoja na kuimarisha uduma za afya katika kila kata ununuzi Wa Ndege kubwa za kisasa

Munisi Amesema nia yao ni kuakikisha wachimbaji wadogo na wakubwa wanafuata sheria na taratibu za uzaji Wa madini lengo ikiwa ni kuimarisha uchumi Wa nchi kwani nchi ni ya watanzania nasio ya wageni.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha alimshukuru Waziri Biteko kwa uamuzi wake wa kuja na jopo kubwa la watendaji wake na kusema kuwa changamoto zilizotolewa na wafanyabiashara huenda zikapata majibu kwa maslahi ya nchi.



Mwisho.
FB_IMG_1577091517335.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom