Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,514
- 19,266
Watu wenye tabia ya kubeba makopo ya pombe ndani ya garimoshi za chini ya ardhi katika jiji la London, watasheherekea onyo lililotolewa na Meya wa London la kukataza tabia hiyo.
Wameamua kunywa usiku wa Jumamosi kukaribisha onyo hilo ambalo linaanza kutumika Jumapili,tarehe 7.
Watu zaidi ya 4,000 wamejiorodhesha katika orodha hio ya walevi ambao watakwenda na pombe zao katika treni inayopita njia iitwayo "circle line" ambayo kwa kawaida ni ya mzunguko katikati ya jiji la London au "Central London".
Meya mpya wa jiji la London bwana Boris Johnson ambe ni wa chama cha conservative ametimiza ahadi ya kutoa onyo hilo ili kuzuia tabia ya ajabu ya baadhi ya abiria kubeba pombe zao za makopo na kuwa wanakunywa kidogokodogo huku wakitoa maneno ya kejeli na matusi kwa abiria wengine.
Hii sijawahi kuona kabisa na kwa maana hio watu hawatatumia circle line siku ya Jumamosi jioni.
Je kuna yeyote ambae amepata kuona mambo haya ya ajabu mahali alipo ughaibuni?
Source: Evening Standard