kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
Huo ndiyo ujumbe walioweka wauza magazeti mkoani Iringa ili kupunguza idadi ya 'watazamaji' wanaosoma magazeti hayo yakiwa yametundikwa kwa kuuzwa.
Vijana wauza magazeti katika eneo la Posta mjini Iringa wameweka matangazo yanayopiga marufuku tabia ya watu kukusanyika katika maeneo hayo na kusoma magazeti mezani bila kununua. Matangazo hayo yana ujumbe unaosema kuwa "hapa haturuhusu kusoma magazeti mezani bure, ukitaka kusoma mezani shilingi 2,000/= na kununua gazeti shilingi 400/= n.k, pia huruhusiwi kukaa hapa wala kuvuka kamba". Mbinu hii imeanza kuonyesha mafanikio makubwa ndani ya mji wa Iringa ambapo tabia ya watu kusoma bure mezani imeanza kupungua.