ONYO kwa wapiga chabo magazeti. Kusoma gazeti mezani sh. 2,000/= kununua sh. 400/= 02

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Huo ndiyo ujumbe walioweka wauza magazeti mkoani Iringa ili kupunguza idadi ya 'watazamaji' wanaosoma magazeti hayo yakiwa yametundikwa kwa kuuzwa.

Vijana wauza magazeti katika eneo la Posta mjini Iringa wameweka matangazo yanayopiga marufuku tabia ya watu kukusanyika katika maeneo hayo na kusoma magazeti mezani bila kununua. Matangazo hayo yana ujumbe unaosema kuwa "hapa haturuhusu kusoma magazeti mezani bure, ukitaka kusoma mezani shilingi 2,000/= na kununua gazeti shilingi 400/= n.k, pia huruhusiwi kukaa hapa wala kuvuka kamba". Mbinu hii imeanza kuonyesha mafanikio makubwa ndani ya mji wa Iringa ambapo tabia ya watu kusoma bure mezani imeanza kupungua.
 
du huo ubunifu babukubwa na mm ninakaugonjwa ako sana sijui wakianzisha hapa dar cjui itakuwaje
 
Acheni ugumu DrPhone!
Shing 400 inakutesa hivyo aisee?
Sasa utauziwa magaeti 5 bila kupenda!...huh!
 
Huo ndiyo ujumbe walioweka wauza magazeti mkoani Iringa ili kupunguza idadi ya 'watazamaji' wanaosoma magazeti hayo yakiwa yametundikwa kwa kuuzwa.

Vijana wauza magazeti katika eneo la Posta mjini Iringa wameweka matangazo yanayopiga marufuku tabia ya watu kukusanyika katika maeneo hayo na kusoma magazeti mezani bila kununua. Matangazo hayo yana ujumbe unaosema kuwa "hapa haturuhusu kusoma magazeti mezani bure, ukitaka kusoma mezani shilingi 2,000/= na kununua gazeti shilingi 400/= n.k, pia huruhusiwi kukaa hapa wala kuvuka kamba". Mbinu hii imeanza kuonyesha mafanikio makubwa ndani ya mji wa Iringa ambapo tabia ya watu kusoma bure mezani imeanza kupungua.
Na mbaya zaidi wanaokutana kwenye kusoma magazeti mezani huwa hawasalimiani............kila mtu kama bubu vile.......... anakuja anatumbua macho kwenye headlines akimaliza anaondoka zake
 
Acheni ugumu DrPhone!
Shing 400 inakutesa hivyo aisee?
Sasa utauziwa magaeti 5 bila kupenda!...huh!

mkuu mm napendaga kununua mwanahalisi na ss hivi nashukuru mengi tuna soma online so not bigi dili ww vp ujawai kupiga chabo
 
Na mbaya zaidi wanaokutana kwenye kusoma magazeti mezani huwa hawasalimiani............kila mtu kama bubu vile.......... anakuja anatumbua macho kwenye headlines akimaliza anaondoka zake
yani mkuu ujakosea kila mtu anakuwa busy bila shaka na ww ni mwenzetu
 
Dah ni ubunifu mzuri kwa kweli..Ktika pitapita yangu kwenye blog ya maggid nikakutana na picha hizi hapa chini
 
Attachments

  • 7.jpg
    7.jpg
    80 KB · Views: 119
  • 5.jpg
    5.jpg
    146.2 KB · Views: 48
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom