Onyo kwa wafanyabiashara wote wa tanzania, wanaotumia tanga port na boda

Major... wewe sasa ni captain au hata generali kabisa

Nakushukuru binafsi kwa kuwa courageous enough... kusema ukweli tatizo la TRA na polisi ni letu wenyewe. Ni la kujitakia kwani hakuna mfumo unaopima utendaji wa mtu yoyote.

Mwajiriwa serikali anapimwa kwa namna anavyoishi vyema na bosi wake, mwajiriwa wa polisi au TRA anapimwa na namna anavyompelekea bosi "mboga" na maji ya kunywa.

the real Ben, Ben Mkapa saw this na akaleta good appraisal system na kupatikana kazi kwa ushindani, unfortunately the king of PhD akaona ule ni ujinga kwani wanaokuja hawajui mfumo wa serika, amesahau kwamba mfumo wa serikali haukua na tija, alisahahu kwamba mfumo wa serikali ni wa kiswahiba na majungu

nasema kwamba... huyo Ben wa Tanga ni mmoja tu, wapo kila sehemu, usipoangalia hata mortuary utawakuta... nao huaga majumbani kwamba wanaenda kazini


SITUMII TENA, NITASHIRIKI KUIENEZA HII HABARI MBAYA NA PIA NITASHIRIKI KUENEZA HABARI NJEMA YA BANDARI YA ZANZIBAR

TUMEZIDI SANA SISI
 
Jamani nimekumbushwa maumivu ya kidonda ambacho kilikua kinakaribia kupona, Nilifilisiwa kabisa na hawa jamaa wa TRA tanga, nilitokea nairobi na mzigo wangu tena kidogo tu nimeulipia vizuri namanga nimepita kote naonyesha documents zangu na ninapita bila tatizo, kufika segera nikakuta na jamaa wa TRA tanga, mmoja wao aliitwa KISAKA na wengine watatu. Walikataa zile document zangu na kunitaka niwape millioni 2, kwa kuwa mimi ndio kwanza naanza biashara wakati huo sikuwa na pesa za kuwapa, wakakamata gari ikawekwa kituoni pale segera siku tisa,nikaenda TRA tanga kujua hatma ya mzigo wangu, mzigo ukakadiriwa nikatakiwa kulipa millioni 60 na dolla 1000 za gari kukaa pale kituoni juu ya zile nilizokua nimelipa namanga, dhamani ya mzigo haifiki hata millioni 20 kweli niliteseka, ikabidi niongee na mtu aliewahi kufanya kazi TRA akaja akawaomba wakasema wapewe milioni 2 then wataachia mzigo. Mpaka leo nalipa madeni yaliyotokana na ule mzigo mwaka wa tatu. I libidi niache biashara. Namshukuru Mungu nimepata Kazi huku Kenya. Ila yale maumivu siwezi kuyasahau. Watoto kukosa ada , chakula, hata pesa ya pango. Kweli hawa jamaa wanajibebea laana nyingi.
 
Mpaka sasa bado sijajua kwa Tanga, kati ya TRA na polisi nani haswa anayehusika kukusanya kodi, maana Tanga ni maajabu. polisi wana nguvu kuliko TRA, Mbona mambo hayo ya ma-road block Dar hakuna? au labda tuseme ile ni nchi nyingine?. KWELI NIMEAMINI UONGOZI WA NCHI UKIWA LEGELEGE KILA MTU ANAJIKATIA ENEO LAKE LA KUTAWALA, inauma sana
 
Huyu Meja Kalembo waliyempa cheo cha ukuu wa mkoa, mimi naona kile cheo siyo saizi yake. Maana ananishangaza, eti anapoteza mapesa mengi ya kufanya mavikao yasiyo na tija. wakati wauwaji wa mkoa wa tanga ni JESHI LA POLISI, NINA WASIWASI NA UMEJA WAKE.KAMA NINGEKUWA NI MIMI. NINGETOA AMRI MOJA TU,"KUANZIA LEO POLISI NI MARUFUKU KUKAMATA MZIGO WA MTU YEYOTE, HII NI KAZI YA TRA, NAWAAGIZA MKOME KAMA MLIVYOKOMA ZIWA LA MAMA ZENU" Kwisha,
 
images
Hiyo ni bandari ya Tanga, wakati wa Mkapa ilikuwa iko bize. yaani meli zilikuwa zinasubiriana kushusha mizigo, na hata wakati wa Mwinyi. Lakini sasa hivi hii bandari IMETEKWA NYARA NA JESHI LA POLISI MKOA WA TANGA,Pamoja na boda yake ya horohoro. WAFANYABIASHARA WOTE WAMEINGIA MITINI. Wengi wamehamia Zanzibari na Dar angalau kuna nafuu, hata wafanyabishara wa hapo tanga wanaogopa hawaitumii. Hii ni noma. BORA WAMUUZIE MUSEVENI MAANA BADO ANAITAKA KWA GARAMA YOYOTE.Sasa hivi hakuna meli inayotia nanga hapa,Check mwenyewe,ilivyo wazi, empty. hiyo unayoiona hapo, ni meli ndogo ila ni mbovu iko tu hapo muda wote
 
Hii ni Tanga eneo la ngamiani, HUU NI MJI AMBAO ULIKUWA UNACHUKUA NAFASI YA PILI KWA MAPATO NA MAENDELEO TANZANIA, WAKATI WA MWALIMU J K NYERERE, ukifika sasa hivi utafikiri labda serikali hawautaki, kama vipi watuambie tutafute wazungu wa kuununua huku, maana huku watu wana pesa za kutosha, kuliko kuwapotezea watanzania waoishi hapo muda
 
Back
Top Bottom