Onyo kwa wafanyabiashara wote wa tanzania, wanaotumia tanga port na boda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Onyo kwa wafanyabiashara wote wa tanzania, wanaotumia tanga port na boda

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Major, Dec 16, 2010.

 1. M

  Major JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Nawatahadharisha wafanya biashara wote wanaotumia bandari ya Tanga au boda ya Horohoro kupitisha bidhaa zao.Na kama ukitaka kufilisika basi puuza onyo hili

  Kama wote mnavyojua utaratibu wa TRA siku hizi, mahala popote sasa hivi tanzania ukitaka kulipia bidhaa zako ni lazima docoment zako ziazie tiscan, wakishakadiria kiwango unachotakiwa kulipa na ukishakubali basi unawalipa kupitia benki walizozichagua wao. baada ya hapo mnakwenda kuhakiki mzigo kama uko sawa. Kama uko sawa basi unapewa mzigo wako. kule Tanga ni kama nchi nyingine kabisa, Kwa pale bandarini tanga ikifika wakati wa kukagua, kama ni kakontena kamoja, watakuja wakaguzi zaidi ya 20 na kila mmoja anajifanya ametilia shaka mzigo wako, na kuanza kukutisha,utasikia "HUYO TUMPELEKE KWA BEN HUYO"

  Ben ni mkuu wa forodha pale Tanga, na kwa ninavyosikia historia yake ni kwamba fail la mzigo wako likifika kwake, kwanza huo ushuru uliolipia ataukataa halafu anasema ni sawa na hujalipa kodi halafu anakupigia hesabu zake ambazo yeye anasema ni za kitaaluma,baada ya hapo ni lazima huo mzigo uachane nao maana hata kama ukienda kuuza huwezi kupata hiyo pesa ya ushuru anayotaka.

  Kwa kuwa hiyo tabia yake imewatisha sana wafanyabiashara, maana kwa kweli ni wengi wamefilisiwa na huyo Jamaa, basi watu wanaamua kupitia horohoro boda angalau wamkwepe.Sasa basi huko horohoro ndiyo balaa kabisa, Pale TRA horohoro hakuna tatizo sana vijana pale wanafanya kazi vizuri kabisa , kama umeshalipia wanakagua na kama mzigo upo sawa, wanakupa mzigo wako unaondoka,

  KIMBEMBE, Kutoka horohoro mpaka tanga ni kilometa 70, lakini kuna ROAD BLOCK 12, ktk hizo road block za TRA ni 2 tu, 10 ni za Askari polisi, TRA ukiwaonyesha Docoment za mzigo na kama umelipa vizuri hawana neno wanakuachia unaondoka, Ila POLISI wao hawataki DOCOMENT, Kila block utakayokutana nao wanataka milioni moja, ukiwaambia umeshalipa ushuru wao wanakwambia hizo ni za serikali bado zao, na ukibishana nao wanakuambia basi wao hawana neno ila wanakupeleka kwa BEN. Watafanya kila njia ya kukutisha mpaka uwape pesa. ukishawapa unaondoka baada ya kilometa 6-7 unakutana na wengine na hali ni hiyo hiyo , mpaka ufike Tanga mjini tayari ulishafilisika,,

  HII NDIYO SABABU YA KUFA KWA TANGA WALA WASITAFUTE MCHAWI. Pale bandarini Tanga sasa hivi hakuna meli hata moja ya bidhaa inayotia nanga pale, watu wanakufa njaa, bandari mzuri kabisa lakini wameiuwa wenyewe. ONYO KAMA UNA NDUGU YAKO ANAFANYA BIASHARA AU ANATAKA KUANZA KUFANYA BIASHARA MTAHADHARISHE NA TANGA PORT ATAFILISIKA, KULIKO HIYO TANGA YENYEWE
   
 2. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Asante sana; watashughulikiwa!!!
   
 3. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kaka nadhani Nnkupenda. Tafadhalini wakaidi, print this and read. Wajasirimali. someni huu waraka, Huyu ni Major bin Shujaa wa mtukula. Nnapongeza sana kwa ufundi wake wa kuanalyze.
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  T-Scan nawajua saaaaaana. Upuuzi mtupu niliagiza RAv-4 ya 2002 wakaenda kukadiria. ilichukua wiki nzima hawa Wajinga kutoa makadirio. Mimi TRA na Mfumo mzina nauchukia vibaya mnooo ndo maana i wish tungejikuta tupo Afghan au Iraq siku moja tu hawa maafisa uchwara wa TRA na TSCAN unawapeleka wote frontline wakapigane na Taleban km hawajajinyea kesho yake tulirudi bongo watafanya kazi kiufasaha, mxziegkfdbXYux vdtQYECTLERCBWULRBMEC'RO;NVklnc ZAO WOOOTE WANAOWAIBIA WANANCHI PALE tra NA tSCAN.
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Ziko wapi enzi zangu za balaa mitaani!....hakyanani ningepitisha huko maksudi tu!:redfaces:
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  huyu waziri wa mambo ya bandari anaweza kuwa ni rafiki wa Ben? bahati yake hajapewa Magufuli huo ukanda
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  TRA ndio kikwazo cha maendeleo ya mtanzania!yaani hata kulipa kodi uwabembeleze kama vile unatongoza wapuuzi sana!wanakera sana biashara za importation inakatisha tamaa kwa sasa hivyo kupungua kwa mapato
   
 8. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Jamani injii hii imekwisha kabisaa asante kwa kunistua aisee kumbe ndio ilivyo dah tabu tupu
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Mkuu hongera sana. Ile border ya HoroHoro ina tatizo tena kubwa sana. Wana tabia mbaya ya kuongezea ushuru bila kutoa sababu eti kigezo ni kuwa mzigo wenu mme under declare. TRA sijui wanafanyaj kazi. Naona kama mambo yakodi ni suala la maamuzi binafsi ya wafanyakazi wa TRA badala ya kufuata system inayoeleweka. Na wasivyo na huruma kama ni mfanya biashara mdogo wanaweza kukukadiria kodi mpaka ukaifunga na biashara yenyewe. Sasa kama wanafanya hivyo kesho watakusanya wapi kodi.
  Halafu unakuja sikia wafanyabiashara wakubwa wamepewa misamaha ya kodi. Ndio ninapochoka hapo. Duuh!
   
 10. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  holili ndiyo usiseme magari yamejaa hakuna pa kuegesha yote yanasubiri bei toka dar hii nchi inabidi ipate kiongozi mzalendo , mkulo kapita jmosi unajua hali itabadilika ndiyo kwanza anawatetea kuwa ni mfumo mpya. Ulaaniwe utawala usiotatua kero za wananchi
   
 11. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  sasa huyu ben si anatumia formula za tra au hatumii?
   
 12. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Preta, kwani Bandari na TRA zipo kwenye wizara moja? maana nildhani hivi ni vitengo viwili tofauti. Kweli hili jahazi limekwenda mrema.
   
 13. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  vipi umesharudi toka wellington
   
 14. M

  Major JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Mimi niko nje ya TZ, lakini biashara zangu kwa asilimi 80 zipo Tanzania. Mwezi wa nane nilikuwa Tanga, na lengo langu la kwenda pale ilikuwa ni kutaka huhakikisha kama maneno ninayoambiwa na vijana wangu je ni ya kweli?. Amini usiamini,nilikaa pale tanga kwa siku 21,na nilikaa pale horohoro siku tano. kufanya utafiti na uchunguzi, nilichokishuhudia," BROO, NI AIBU"
   
 15. M

  Major JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Kuna matukio kama 10 hivi niliyaona ambayo yalinitisha, na kuna baadhi picha za ushahidi ninazo, naomba twende taratibu nitakufahamisheni moja moja, Kuna jamaa nilimkuta pale horohoro, yeye alikuwa amefuatilia gari yake, kama kawaida pale wafanyabiashara wote huwa wanakaaga sehemu moja kwa ajili kupiga story wakati wakisubiri hatma ya hukumu zao, kutoka kwa waheshimiwa wa TRA, sasa yeye alikuwa amekaa kinyonge sana, Nikaona nimuulize kulikoni? Jamaa alinijibu kama vile anataka kulia, Anasema, bro, mimi leo ni siku ya 7 niko hapa, gari yangu nimeambiwa nimedanganya mwaka,Mikanda ya gari inaonyesha ni ya mwaka 1998, lakini cheses ya gari inaonyesha ni ya mwaka 2004. wenyewe walioniuzia hii gari wapo japani na nimewaeleza hili tatizo, wakaniambia hawa jamaa ni wapumbavu kabisa, tena angalia na fax waliyotuma kwangu na nimeshawapa lakini hawaelewi kitu, jamaa wanataka laki 5 na mimi sina. Kwa kuwa mimi nina elimu ya kunitosha, nilisoma docoment, kwa kweli kila kitu kilikuwa sawa kabisa. Mimi kwa huruma niliingia ndani kwa incharge, nikamwuliza kwanini wananyanyasa watu namna hii?. Jamaa akanijibu, kwani wewe ni nani!! kwa hasira, tena naomba usiingilie shughuli za watu! na toka ofisini kwangu!, mimi sikutoka ila nikamuuliza, HIVI KWELI WEWE UMESOMEA HII KAZI AU UMESAIDIWA, KTK ULIMWENGU WA LEO HIVI KUNA MTU ANAWEZA KUDANGANYA MWAKA WA GARI? GARI YOYOTE DUNIANI SASA HIVI UKIINGIZA TU CHASES NAMBA INAKUPA KILA KITU, MWAKA WA MKANDA WA GARI HAUWEZI KUWA NDIYO KIELELEZO CHA MWAKA WA GARI HATA SIKU MOJA DUNIANI KOTE. Mimi nilikasirika nikaingia kwenye vile vibanda pale nikapiga bia zangu 2 nikaondoka zangu tanga, nina hasira mbaya sana hasa nikiona mtu anaonewa mbele yangu, maana ningeweza kumuua yule bosi wa TRA pale. Kesho yake jioni nilikutana na jamaa mwenye gari pale Nyinda hotel, jamaa alinishukuru sana, akanionyesha gari yake kwamba walimpa na hakutoa chochote sababu ya maneno yangu makali,.Hiyo ni siku ya kwanza tu nilipofika pale horohoro. Jamani muda wa kwenda mzigoni umefika, tutaonana kesho, ila msichoke kufuatilia hiki kisa cha Tanga maana mimi nilikufa moyo maana sikudhani kama ktk dunia ya leo bado kuna mambo ya hovyo kama ya tanga, Juzi nilikuwa nasoma gazeti moja la kibongo, ati kuna huyu mkuu wa mkoa anaitwa Meja kalembo kama sikosei, eti ameitisha kikao cha kujadili, "KWA NINI MKOA HUU UNAKUFA TARATIBU KILA SIKU.
   
 16. M

  Mwera JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tumieni bandari ya zanzibar hakuna zengwe ndani ya siku2 tu unatoa mzigowako tena ukiwasalama kabisa,unachotakiwa nikufata taratibu nakulipia ushuru,tokea imeingia serikali mpya yamseto 2010 amini usiamini rushwa imeondoka zenj kwa asilimia 80,na after 3 month zenj itakua mfano wakuigwa dunian kwa kutokua na ubabaishaji naula rushwa,ukitoa mzigo wako unaupeleka dar unaonesha document kuna process kidogo badae unapeleka popote upendapo ktk tanganyika au popote kule,juzitu kuna meliyamchele mbovu imerudishwa ilikotoka na maalim seif amesema wazi zenj sio jalala lakuleta bidhaambovu,kama hamuamini nendeni zenj mkajionee hata hospital za serkal kuna mabadiliko makubwasana yakiutendaji
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe Zanzibar nimepitisha mizigo yangu miwili hadi sasa huwezi amini sijahonga hata sumni na wala kuibiwa kitu lakini nilipokuwa nashusha mombasa na dar hatari tupu ilibidi niweke pesa ya rushwa na wizi. Sipitishi tena mombasa na dar ni hasara tupu haki ya mungu.
   
 18. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Tafuta tape recorder na watepu wanavyo omba pesa halafu ilete hiyo tepu hapa mtaandaoni
   
 19. M

  Major JF-Expert Member

  #19
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Bora angalau pesa wanazoibia watu wangejenga japo huo mji wenyewe, yaani ni choka mbaya, hakuna gest ya wageni hata moja, iliyokuwe ni ya mpare mmoja ambayo ni chafu, hizo shuka hata mbwa wangu hawezi kulalia. Kuna mzee mmoja wa kikuria ambaye alikuwa anafanya kazi pale TRA, akadunduliza vipesa vyake, akaanza kujenga kahoteli kadogo tu lakini ka kisasa,Ben kuona nyumba inanyanyuka, akamtimulia mbali, sasa mzee ameshindwa kukamalizia masikini, HAKUNA CHOO WALA MAJI YA BOMBA MJI MZIMA, HAPO TRA NI VUMBI KALI HUWEZI AMINI KAMA NI SEHEMU YA SERIKALI YA KUKUSANYIA MAPATO, IT'S REAL SHAME.
   
 20. M

  Major JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Hii ni lunga lunga border, ya kenya.Kutoka hapa mpaka boda ya Tanzania ni kama hatua 100 tu za mtu mzima. SASA NAJIULIZA HATUONI AIBU, na hapa Kenya border urasimu ni sifuri
   
Loading...