ONYO: HATUKWAMISHI JUHUDI ZA RAIS TUNAENDELEA NA ALIZOTUKUTA NAZO

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,058
Kumeibuka Kikundi cha lawama Tanganyika.

Ukiwaza tofauti Na wao unasingiziwa eti unakwamisha Juhudi za rais. Huu ni uzandiki wa hali ya juu Na lazima tuupige vita.

Sisi Juhudi za kuijenga hii nchi tulikuwa nazo tangu kitambo.
Yeye akikomaa na Makinikia nami nikasema naona busara ni kuangalia upya mikataba sikwamishi Juhudi zake bali naendelea Na Juhudi zangu za kutaka uwazi katika mikataba ya madini Na gesi.

Nikisema sivutiwi Dr.Mwakyembe kuongoza wizara ya michezo Na kukosoa uteuzi usiozingatia weledi,historia,taaluma Na maono siyo kwamba nakwamisha Juhudi za Rais bali ni mwendelezo wa Juhudi zangu kutaka teuzi zizingatie vigezo Na tija.

Nikisema demokrasia ni watu Na watu ndiyo sisi wenye haki ya kujumuika Na kukusanyika mikutanoni na kwenye maandamano ya Amani, siyo kwamba nakwamisha juhudi za Rais kutaka watu wachape Kazi...hapana!
Mimi nakuwa naendeleza Juhudi alizonikuta nazo yaani ndoto ya kuona jamii yenye Uhuru,Upendo Na inayoheshimu Uhuru wa kutoa maoni katika mfumo wa vyama vingi.

Kwa mantiki hiyo, sitaki tena MTU anituhumu kizembe ati nakwamisha Juhudi za MTU. Mimi naendelea Na juhudi zangu.

Nini maoni yako?
 
Magufuli akiboronga tutasema,kwa sababu inawezekana kuipenda Tanzania kuliko tunavyompenda Magufuli.
 
Umeandika ukweli sana mkuu , wao waliposema Ndioooo na kugonga meza , sisi tulisema Siyooooo na kuondoka bungeni ili tusiwe sehemu ya laana katika nchi .

Leo wamesahau nini ?
 
Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana.
Wafanya kazi wanakatwa maslahi yao.
Watanzania maisha yao yameongezeka kuwa magumu.
 
Maoni yangu ni
Kumeibuka Kikundi cha lawama Tanganyika.

Ukiwaza tofauti Na wao unasingiziwa eti unakwamisha Juhudi za rais. Huu ni uzandiki wa hali ya juu Na lazima tuupige vita.

Sisi Juhudi za kuijenga hii nchi tulikuwa nazo tangu kitambo.
Yeye akikomaa na Makinikia nami nikasema naona busara ni kuangalia upya mikataba sikwamishi Juhudi zake bali naendelea Na Juhudi zangu za kutaka uwazi katika mikataba ya madini Na gesi.

Nikisema sivutiwi Dr.Mwakyembe kuongoza wizara ya michezo Na kukosoa uteuzi usiozingatia weledi,historia,taaluma Na maono siyo kwamba nakwamisha Juhudi za Rais bali ni mwendelezo wa Juhudi zangu kutaka teuzi zizingatie vigezo Na tija.

Nikisema demokrasia ni watu Na watu ndiyo sisi wenye haki ya kujumuika Na kukusanyika mikutanoni na kwenye maandamano ya Amani, siyo kwamba nakwamisha juhudi za Rais kutaka watu wachape Kazi...hapana!
Mimi nakuwa naendeleza Juhudi alizonikuta nazo yaani ndoto ya kuona jamii yenye Uhuru,Upendo Na inayoheshimu Uhuru wa kutoa maoni katika mfumo wa vyama vingi.

Kwa mantiki hiyo, sitaki tena MTU anituhumu kizembe ati nakwamisha Juhudi za MTU. Mimi naendelea Na juhudi zangu.

Nini maoni yako?: maoni yangu ni kwamba kuna hili jipya la "kuchapa kazi", hili halikuwepo katika utamaduni wa kiTanzania. Watanzania wamezoea kuongea tu na sasa wamepata jipya LA kutaka mikutano na kuandamana! Hivyo raisi wetu akaona bora asisitize kufanya kazi mpaka uwe nao uutamaduni wetu. Japo kuna watu bado wataendelea kupinga tu wakitaka mikutano kutwa kucha, kuandamana, kubeza ukweli. Lakini namtaka aendelee hivyo mpaka tufanye kazi bila shuruti. Nchi zote zinazo jifanya zina demokrasi zilipitia kipindi hiki. Lakini sisi tunataka tuwe sawa na wao wakati bado masikini.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom