ONTARIO'S JF Exclusive Interview: Ujasiriamali na harakati za maisha kwa ujumla

Sijakataa kuona mbali wala sijasema mtoto kuwa na akili za wazazi!

Nazungumzia exposure Mkuu! Yes, Yeye amesema ametoka familia ya kawaida sana! Lakini kumbuka alisomeshwa Kenya primary then akaja St. Thomas kama sijakosea! Huyu mzazi mwenye uwezo wa kujinyima hivi utamfananisha na mzazi ambaye hajawahi kuona idadi ya noti za elfu kumi zinazotengeneza laki moja!?!

Tunaposema mazingira yana determine future ya mtu, anza kufikiri wale watoto ambao huwa unawaona kwenye TV wakishangilia kuona gari kijijini kwao, wakishangaa mtu aliyevaa viatu, wakishangaa mtu aliyechomekea anapotembelea kijijini kwao! Hakika mtu kama huyu kufika level kama ya ONTARIO kwa umri wake na kwa juhudi zake binafsi!?! Kumbuka hana accessibility ya information zaidi ya taarifa ya mashamba ya babu na bibi!? Shuleni kuelewa lugha ya kiswahili tu taabu!

Mtu kama huyu within 21 yrs aweze kujua Forex trade, sijui Forbes, sijui Aggra n.k n. k!?! bila shaka itakuwa muujiza na huyu lazima ataangaliwa kwa jicho la pekee!

You may think kwamba niko negative but hope ukifikiria kwa undani utagundua kuwa kuna tofauti ya mtu wa mjini kusema anatoka familia ya kawaida na familia hiyo ya kawaida uiweke kwenye mazingira ya vijiji vyetu vya ndani ndani utagundua kitu hata usipokubali hadharani!

All in all, kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa huyu dogo bila kudoubt chochote!

Kikubwa kilichonivutia kwake ambacho wengi kina tu-cost ni lack of confidence! Na hii kwa asilimia kubwa husababishwa na lack of knowledge kwa jambo tunalotaka kufanya!

Nimependa anavyojiamini, anavyosoma sana vitabu (hii nimeona hata kwa Masoud Kipanya) na pia alivyo na moyo wa kutaka kuona na wengine wanafanikiwa!

Spirit kama hii lazima nijiforce inaambukize! Huu ni ugonjwa mzuri sana! Watu wanasema hakuna ugonjwa mzuri ila huu ni mzuri! Kama si mimi basi usiku na mchana nita struggle angalau mmoja wa watakaotoka kiunoni pangu augue huu ugonjwa asiee!!
Wewe ni mtu makini sana Uncle Jei Jei, umesema ukweli mtupu.
Hakuna mzazi masikini anaishi tuseme Nyankumbu vijijini (Mkoa wa geita), ata kuwa na uwezo wa kujibana na kumpeleka mwanae Nairobi, ikiwa huyu mzazi hata ile ada ya kipindi kile ya buku teni sijui kwa term kwa shule za day!!?(apa sikumbuki vizuri). Maana hiyo nauli tu ya kwenda shule ni ada tayari ya say, miaka miwili.
Kikubwa hapa cha kujifunza ni kwamba ONTARIO alipata exposure mapema and that he is brilliant to see and grasp opportunities.. Kitu ambacho sio kila mtu anaweza kuwa nacho.

Personally I salute him, for his success and especially at his age. Pengine his dreams and the way he organises his brain in responding to questions around him huwa inajidhirisha kabisa kuwa this is not only a well informed guy but also a very smart one!!!?
Live long ONTARIO,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Big boss Ontario katika kusoma ndo unapata enough knowledge swali kila mtu ana role model(mtu ambaya unatamani uwe kama yeye )nani role model wako ambaye unamadmire na kumfuatilia na ana mchango katika mafanikio yako through kumfuatilia na ana impact kwako.Najua kuna watu humu ushakuwa kama role model kwao kwa kufuata nyayo zako ama kupita pembeni kidogo kujitofautisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
How do you value bitcoin? At least paper currency is backed by serikali zao, or gold is back by the brick. This bitcoin which no one knows how the software behind it works, how can you justify that as a source of investment? why bitcoin is being categorized as cybercrime by many countries
?

Ingawa mimi si niliyeulizwa ila naweza tuu nikasaidia mawili matatu.

Bitcoin ni virtual currency, tofauti na ilivyo kwa currency nyingine ambazo ni za serikali mbalimbali. Currency za kawaida kuwa zinakuwa backed up na serikali husika, Bitcoin ni tofauti. Bitcoin inakuwa backed up na users. Yaani watumiaji wa bitcoin ndo wanaipa power bitcoin. Kivipi.? Toka izinduliwe na satoshi nakamoto (Hajulikani mpaka sasa huyu mtu ni nani haswa) mwaka 2008, Bitcoin imekuwa ikitumia peer to peer transfer methods hivyo kufanya kutokuwa na central authority inayoicontrol wala mtu anayeicontrol. Hiki kitendo cha kuwa decentralized ndo kinachoipa thamani na power. Kwani ukiwa nayo hakuna anayeweza kuja kukuzuia usiitumie maadam wewe na huyo unayetaka kufanya biashara naye mmekubaliana kutumia bitcoin kama medium of exchange for goods. Na ndiyo ilianza hivyo.

Hii sifa ikavuta attention kubwa sana katika black market na deep web. Kama tunavyojua katika deep webs kuna kila aina ya biashara haramu inafanyika, Na biashara haramu zina turnover kubwa than you can imagine. Shida kwa wafanyabiashara wa deep webs kama silk road na BMR ilikuwa namna ya kulipana pesa. Kwani pesa za kiserikali zilikuwa zinapitia bank na kama tunavyojua katika banks kuna screening ya hali ya juu, hivyo any unusual activities zinapelekewa kufuatiliwa. Lakini kwa bitcoin ni tofauti, unakuwa na wallet yako ambayo ukihitaji unaiweka offline kabisa, na ukiamua kusave bitcoin zako unasave kama files za kawaida. Ukitokea umepoteza key ya wallet, basi ndo umepoteza pesa yako kwani hakuna atakayekusaidia kuretrieve. Ukitaka kuitumia BTC zako unafanya mining unatumia. So kutokana na sifa hii, Deep web traders wakaona hii ni fursa ya kuwa free from federal reserve banks za nchi husika na kuanza kuoperate free from polisi na vyombo vya usalama. At first bitcoin wakati inaanza, exchange rate yake ilikuwa ndogo kwani mwaka 2009, bitcoin 10,000 ziliweza tuu kununua pizza.

Ila kama ilivyokuwa kwa law of demand and supply, na uhitaji wake katika black market, Ilipanda thamani taratibu na kufikia mwaka 2014, 1BTC ilikuwa ikibadilishwa na zaidi ya 1000 USD. Ni kipindi hiki ikaanza kupigwa vita sana na wakuu wa dunia na serikali zao. Katika haya ilipelekea mpaka FBI kuvamia mtandao wa silk road na kuufunga na kumkamata Dread Pirate Robert. Kitendo hiki kilipelekea mamilion ya bitcoin ambayo yalikuwa katika transaction kwa kipindi hiko kupotea na kuwa seized na FBI. Hii haikurudisha nyuma nguvu ya bitcoin bali ilizidi kuipa nguvu, mwishowe mpaka saa hizi baadhi ya bank zimeanza kuikubali, na baadhi ya makampuni yameanza kuikubali kama medium of exchange. Na as we speak kwa sasa 1 BTC ni zaidi ya 4000 USD. So you can imagine the power of it.

So kukujibu kiufupi tuu, BTC inakuwa backed up na user/loyalty. Na kinachoifanya iwe trust worth ni jinsi ilivyokuwa designed, kwani ilikuwa designed katika kuimia kufanya biashara za kuaminiana, Huhitajiki uwepo physicaly sehemu ndo biashara ifanyike, Kwani with normal cash ni lazima utahitajika physicaly sehemu ili kukamilisha biashara yako. kwa maana kama si kukutana na huyo unayefanya naye biasshara, Basi utahitajika bank kwenda kujibu maelezo pesa zilizoingia katika akaunt yako zimetoka wapi. BTC imekuwa na demand kubwa sana kwa sababu major medium of exchange katika dark webs. Na tunavyojua, Dark web ina matumizi makubwa kuliko surface web, na pia no one can shut down dark web so BTC is online to stay. Na hivi sasa kuna ATM mpaka za kutolea hizi pesa.
 
HEBU TUONGEE KIBIASHARA SASA:-

Ukipata nafasi ya kufika kule Mbozi Mbeya, ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na kilimo cha kahawa, kwa kweli unaweza kuhweuka, na kujiona kama mtu uliechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka Mafinga na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na biashara ya miti na mbao, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Pitia maeneo ya Ruaha Mbuyuni kutana na wakulima wa nyanya na vitunguu wakikuonesha coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira kama ulikuwa mwajiriwa

Ukitoka pale ukaenda mpaka Mang'ula na Ifakara Morogoro, ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye mpunga, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, "Nilikua wapi siku, zote hizi?"

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi Kariakoo, kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule China, Uingereza na Dubai. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kufight kupata fremu pale!

Usiende kwanza Zanzibar, bali chukua Fastjet uende chapchap kule Arusha. Hapo kutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. Ukisimuliwa ABC za madini na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana!

Unapoendelea kutafakari, rudi mtandaoni. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa NetworkMarketing utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua mavouge yao, wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Madagascar na Uamerikani, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mipunga ya Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, usiombe ukutane na fursa ya digital currency, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale tunaokinadi kilimo kama dhahabu inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja niuchune kukupeleka kwenye fursa ya samaki kuzitoa Mwanza kupeleka Congo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:-

1. Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.

2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.

3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Ashura. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya networkmarketing, lakini mwingine nature ya networkmarketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwneye mbao, mwaka mmoja mbali unaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung'ang'ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover katika networkmarketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye Kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umejenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.

5. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi, na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja.
*C&P*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Interview nzuri mno sema ilinipita jana,Anyway maswali mengi yameshaulizwa niliyokua na shauku ya kuyajua kupitia Ontario.
Niseme tu huyu kijana ni miongoni wa watu walionifanya nikaingia kwenye kilimo na ufugaji,na tena si kilimo cha heka moja ni kilimo cha heka 10 nakuendelea,amenifunza sana kuthubutu katika nyuzi zake mbalimbali anazozitoa hapa.Na imani mwakani majira kama haya nitatoa ushuhuda wa kazi zangu ninazozifanya! Nashukuru mdau aliyeulizia vitabu ambavyo unarecomend mtu apitie kuhusiana na kilimo, nimeviona nitavitafuta na kufanyia kazi. Asante tena sana kwa Daby na Ontario kwa uzi huu wenye manufaa kwangu nimeusoma wote.
Mkuu na mimi nilikuwa na vihitaji hivyo vitabu naweza kuvipata???

Power of forgiveness
 
Daaaah... Nimekaa hapa masaa matatu na notebook yangu pembeni mpaka njaa imeniuma. Hivi huyu kijana ni binadamu wa kawaida kama mimi? Yaani nimepitia post baada ya post nikajiona nilivyo bwege and useless. Tatizo sie wengine wavivu mno aisee kama mimi sijui nifanyeje akili ichangamke maana hata mbele ya Magu imegoma...au mi mlemavu? Ila leo nimekuwa motivated sana kwa kweli...naomba Mungu huu munkari niliopata hapa uendelee hivihivi ee Mungu nisaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee mkuu. Umesababisha nicheke kwa nguvu hadi watu wana nitumbulia macho
Ha ha haaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9c8bf228ea1816c9108f44f70de4596e.jpg


I came from a poor background, kama nisingeweza kutusua ktk biashara basi watu wa kwanza kubeba lawama ni wazazi wangu. They have been ALWAYS negative to me, they gave been all wet to believe that I can make it in life with entrepreneurship.

Lkn kitu nawashukuru wazazi wangu regardless na hali yao ya kiuchumi walijibana sana nisome best schools around. Nasema walijibana sana sana sana, hata naweza kusema walikua tayari kula nyasi ili tusome.

Primary school nilisoma mwisho darasa la 6 hawakua na uwezo kumaliza ada nisome hadi darasa la 8 (nilisomeshwa Kenya - Kajiado na Nakuru), then O'level nilisoma St. Anthony's Mbagala... high school mambo hayakua mazuri nikasomeshwa Ihungo Boys (Bukoba)
Kumbe yule dogo mwembamba mwembamba ST ndo wewe jamaa hahahaha duuh
 
Ama kweli leo ndio nimekuja kuamini na kufahamu kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya KWENDA SHULE na KUELIMIKA.
Maelezo yakini, majibu makini na ushahidi wa wazi wa mkuu ONTARIO vyote kwa pamoja vyanifanya niseme asante sana sana na ninakuombea kwa Mungu akupe uhai, afya na fanaka tele wewe na kizazi chako.

Bila ya kumsahau Mkuu DABY hongera sana kwa wazo na interview makini mmenifanya nisijutie kukesha siku ya leo.
 
Business Name Doesn't matter? real?

Hahaaa haoa unajinasibu ni mfanya biashara mkubwa tena jina la Biashara linafichwa?

KWA NINI UNAFICHA JINA LA BIASHARA YAKO?

Biashara halali jina lina fichwa?

BADO HUJANIJIBU KITU HAPA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ubishi wako wa kiha mzee baba, kama wewe uko makini post za mwanzoni ameweka picha ona jina lake na pia kampuni ya agribusiness kwanini usiangalie na ukagoogle ukamjua zaidi? kama amefanya interview cnn,bbc obviously taarifa zake zitakua mitandao badala ya kung'ang'ania akwambie wakati anataka kumaintain privacy yake...ndo nyinyi msioweza take advantage ya teknolojia
 
Kujiuliza na kujijibu... huku ni sawa na kujitekenya

●What keeps me motivated...
Kitendo cha kuwa hai, naishi na ninapumua kinanipa munkari all the time. We are on earth for a specific reason (labda kama haujatambua hiyo reason) so nikiwa less motivated nakumbuka kua I am still breathing (sijafa) so I have a chance to do it in a better way, so I keep it real again. Tangu nimeshtuka usingizini when I was 16, kila nikijiona nina uhai nakua motivated.
●Dealing with my enemies...
I hate negative people around me, I HATE negativities. If you throw shades to, mwanzo nitakusamehe na nitanyamaza... mara ya pili I will find a way to prove you wrong in front of your eyes. Ukizidi kuonesha hatred unatakua umefika stage ya kutafuta vita. Now ninamwajiri personal lawyer, watu wanaoniletea upupu sitakua nadeal nao mimi, mahakama itaamua.

●my best advice ever...
Maneno ambayo mama'ke mfalme Lemuel alimwambia mwanae katika kitabu cha Methali 31.

1 These are the solemn words which King Lemuel's mother said to him:

2 “You are my own dear son, the answer to my prayers. What shall I tell you?

3 Don't spend all your energy on sex and all your money on women; they have destroyed kings.

4 Listen, Lemuel. Kings should not drink wine or have a craving for alcohol.

5 When they drink, they forget the laws and ignore the rights of people in need.

6 Alcohol is for people who are dying, for those who are in misery.

7 Let them drink and forget their poverty and unhappiness.

●My biggest regret...
Hivi kwanini nilisoma chuo?? Waste my precious time which I'd otherwise do a meaningful thing. Daaamn! Najilaumu sana alooh.

●My belief in God...
It's complicated, am Christian. But but...
Boom ulilolipata chuo lime play part kubwa kufika hapo ulipo au ungeweza kupata source ya kapital sehemu ingine?
 
Mkuu na mimi nilikuwa na vihitaji hivyo vitabu naweza kuvipata???

Power of forgiveness
Bado sijavitafuta kwenye bookshop,ngoja weekend nikipata mda nitaenda kucheki,au pia nikipata wasaha wakuperuzi deep online nikiviona ntashare nawe softcopy
 
Duuuh the guy is really inspirational....
Recently nmekua more interested na financial markets na nmekua mtumiaji mzuri wa internet, websites zipi apart from books unaweza kutushauri to get more info on financial markets
 
Back
Top Bottom