Ontario ameshindwa Twitter, kuna wajanja wengi sana kule

Status
Not open for further replies.
Shida ya huyu mdogo wangu Ontario anatumia nguvu mingi sana kuwaaminisha watu kua Anatengeneza pesa kwa Forex ambayo kwa mtanzania wa kawaida anaona ni Scam. Nina mdogo wangu wa kike hana Kazi ako Dar hapo alikua anaona nachezea yale ma Candlestick na natengeneza vijisent kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale akatamani nikaanza mpa intro akaboreka ila mpaka leo sijawaimfundisha zaidi nasema aendelee kula kwa wazazi tu.Kushawishi mtu forex ni real kazi sana hasa Mswahili ambae amezoea kazi ni ile kuamka asubui kwenda mahala ukatoke jasho.Jeff angeendelea kufanya hii kitu bila kutumia nguvu ya kushawishi kama watu wa qnet angetoboa mbali sana sasa mbwembwe nyingi ka anaenda ukweni watu wamekosa imani nae.Haoni mwenzie The Bold(habib) anafanya mambo yake kimya kimya na ni trader mkubwa sana ka sie wa akina sisi na hii corona watu wametengeneza sana pesa kupitia Forex.
ngoja baadae uanze lalamika hapa
 
Tar 11 mwezi wa nane alikuwa alosto hivyo, juzi akafanikiwa kuwajengea wazazi wake nyumba ya kifahari. aisee kapata vichwa vya kuviburuza, vijana wa sikuhizi wanakosa reasoning.
Kusoma ni jambo moja, kuelewa kilicho andikwa ni jambo jingine
 
ngoja baadae uanze lalamika hapa

Nimlalamikie nani niko kwa forex since 2014 naifanya ishantia hasara mwanzon pesa nyingi tu na sikuacha mpaka leo naifanya na nimefanikiwa kuwa na vijisenti kadhaa vya kuzurura hapa chini ya jua na kuishi maisha fulani amazing si mabaya sana wala luxury. Ontario zile class zake nishaenda kushangaa aliwafundisha vizuri sana tatizo ikaonekana forex ni ya wote waliokosa ajira za(white collar Job) wakaenda kichwa kichwa yakawakuta ndio wanalia mpaka leo hawana hamu na Forex.kumbe forex waweza kaa miaka hata 3 bado ujaielewa na uko nayo kil siku
 
Hii hata MIE ninaweza kujitumia SMS bana si kuwa na simu mbili tu zenyewe wozapu majina tofauti ama haiwezekani
kwahiyo nikileta na hizo credentials za account atakayopewa jamaa utakuja na kauli gani?? au kwa mfano nikakutumia namba ya Ontario alieshinda ukampigia simu akawa sie uliedhan utasema nn ?

kwamba hata ww bla bla ?
 
Michezo ya kitoto pelekea wenzako
Ni watu wawil tofauti , sii mtu mmoja, huyo Ontario wa Twitter ni mtu tu kaamua kutumia hilo jina ila Sio mtu mmoja, wote niko nao group moja WhatsApp

ni watu wawili tofaut, hiyo pesa atapewa j5 nitawaletea credentials hapa muingie kwenye accounts muangalie anavyo trade, watu wawil tofauti kabisa

kama issue ingekua "watu wanao juana" somehow ingemake sense, ila sio mtu mmoja huyo
 
Inasikitisha sana kuona watu wazima dizaini yenu kumuandama kijana wawatu miaka yote chochote afanyacho kwenu ni mavi huu uungu munaojipa wakifedhuri ni ujahili wa hali ya juu usije furahia stuation kama hii kama kijana kama jamii ishakuwa yakifedhuri kihasi hiki hata wewe inaweza kukitokea.
kwanini wasiwe wengine awe yeye tuu
isifie mvua tuu
 
Binafsi mimi nafanya pia forex ila sio ile ya kufundishwa na Ontario, hapana.

Nimejifunza kwa muda mrefu lakini hadi sasa sijapata mafanikio yoyote na hii huenda ikatokana na kuwa bado sijakomaa sana kwenye forex(sio trader mzuri). Hivyo nimepata na napata loss, faida mara moja moja sana na baada ya muda narudia tena loss.

Nilichogundua ni kuwa forex ni ngumu inahitaj muda zaidi kujifunza na kuweza kujimudu ku-trade. Ontario kama kawaida yake alianza na stori nzuri nzuri sana kama alivyoanza huku JF. Uzuri kule alifikia hatua hadi ya kuwapa watu pesa 100k kupitia challenges ambazo anaziandaa.

Anaweza kuamka tu na kusema leo atayefanya hivi nampa laki. Baadae akaanza kusimulia yote yaliyotokea hadi TMT kufa(one side story).

Kila aliyefatilia aliona kuwa huyu kijana ana kitu kikubwa ndani yake, akaongeza followers wengi kwa muda mfupi kwa jinsi anavyoelezea angle zote za biashara zilivyo na haswahaswa hii forex.

Mwanzoni alianza kukataa katakata kwa kusema atafundisha vyote ila sio forex (ilikuwa trick watu waone forex it's a big deal).

Ghafla bin vuu, akaanza kuponda fani za watu na pia kujionyesha sana kuwa ni moja wa successful traders na yupo vizuri financially, watu wakawa wengi kufatilia ( kama kawaida wabongo tunapenda sana shortcut).

Baadae akaanza kusema yupo tayari kusaidia watu waijue forex na hatimaye waanze kudownload pesa. Ila aliweka masharti ya hapa na pale, kikubwa kuchanganyachanganya watu na hatimae waone hana shida sana ya kufundisha watu forex.

Alikuwa tayari kishaplan kuanza kutrain tena watu forex, baada ya watu wengi kuonyesha wana interest ya kuijua forex. Ila kuna watu baadhi kule wana akili sana, maswali yalikuwa mengi sana kwake kuliko majibu na kuishia kuanza ku-block watu ili abaki na wale tu ambao wapo tayari shingo zao kupita kwenye kisu.

Ghafla bin vuu, lile kundi kubwa likapata support kutoka kwa watu wengine na kuambiwa "shtukeni mnaenda kupigwa, hana lolote huyo. Hapo kinachotafutwa ni pesa za kiingilio kwenye training. Na baadae mkionyesha mnaliwa sana wakati wa kutrade mtambiwa "forex is not for everyone". Cha kushangaza sasa hivi hawaambiwi forex is not for everyone, wanakaribishwa vizuri sana.

Ila watu wa kule wengi wana akili, wanajua kabisa 1+1=2 , wamempa mtihani mdogo sana " nunua umeme hata wa buku(1000) alafu tutumie hayo malipo" lengo hapo waone kama hata anamiliki kibanda.

Kwanini wanamuambia hivyo? Kwa sababu ya approach zake alizoanza nazo huko za kujionyesha ana pesa sana.

Twitter kuna watu wengi sana wana akili, bado wale wa Instagram
Yule jamaa anazngua anataka kujifanya Tz nzima ye ndo genious anaona wa Tz malofa fulani, inaingiaje akilini mtu umeotea fursa ya kuvuna pesa uanze kuwastua watu si uvune kimya kimya uwe kama wakina Jeff Bezos, Elon musk ,jamaa pia analeta challenge kwenye professionalism za watu kwa kuwapa challenges kama vile ye ndo teacher , hapa duniani ushasikia billionaire yoyote anatoa challenges ili atoe hela, ili upate hela lazima mtu ufanye kazi , jamaa kama ana pesa si aanzishe Foundation atoe misaada
 
Kijana wako CCNP ENGINEER baada ya kumpa ukweli wa maisha amepotea kimoja. Karibu sana
Juzi CCCNP Engineer alinisalimu Twitter... Nilicheeeka saaana.

Sasa hivi Ni washkaji tu.
154807771.jpg
 
Shida ya huyu mdogo wangu Ontario anatumia nguvu mingi sana kuwaaminisha watu kua Anatengeneza pesa kwa Forex ambayo kwa mtanzania wa kawaida anaona ni Scam. Nina mdogo wangu wa kike hana Kazi ako Dar hapo alikua anaona nachezea yale ma Candlestick na natengeneza vijisent kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale akatamani nikaanza mpa intro akaboreka ila mpaka leo sijawaimfundisha zaidi nasema aendelee kula kwa wazazi tu.Kushawishi mtu forex ni real kazi sana hasa Mswahili ambae amezoea kazi ni ile kuamka asubui kwenda mahala ukatoke jasho.Jeff angeendelea kufanya hii kitu bila kutumia nguvu ya kushawishi kama watu wa qnet angetoboa mbali sana sasa mbwembwe nyingi ka anaenda ukweni watu wamekosa imani nae.Haoni mwenzie The Bold(habib) anafanya mambo yake kimya kimya na ni trader mkubwa sana ka sie wa akina sisi na hii corona watu wametengeneza sana pesa kupitia Forex.
Toka zako hapa halafu we kabinti kiherehere sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom