Ontario ameshindwa Twitter, kuna wajanja wengi sana kule

Status
Not open for further replies.
Hakuna Mtanzania mwenye roho nzuri kiasi cha kuona fursa ya kupiga hela na akaacha kuwavuta ndugu zake ili wapige hela na kukimbilia kuwavuta watu baki asiowajua!! Mtanzania huyo hayupo na bado hajazaliwa, labda kama alikuwepo mara ya mwisho ni 1905!! Ukiona mtu anakuvuta kwenye fursa wewe mtu baki badala ya kuwavuta ndugu/ jamaa zake shtuka na kaa nae mbali, hapo kuna dalili ya KUPIGWA!!

Niwaase Watanzania wenzangu, tujitume kutumia vipawa vyetu, nguvu na uwezo aliotupa Mungu kujitafutia riziki zetu kwani hakuna hela inayopatikana kirahisi kiasi hicho, na hata kama ukiipata kwa kuwaibia wenzio basi nakuacha na maneno haya matatu:
1. Wema hauozi
2. Kila baya/zuri litalipwa
3. Mlipaji hafi daima
 
Nilimuona smart sana ila kwa hili nimemdharau

Ameweza kuwaibia watu wazima na akili zao akashindwa kufikiri watu walio tweeter wapo Jf pia kwamba wataibaini hiyo ID?

Kweli ukishafika mwisho wa zama unatinyanga kizembe sana
Kipato chochote cha dhuluma huwa hufiki mbali..na usipoangalia unaweza kuishia ktk aibu kubwa sana..mioyo ya watu huwa inalia kimya kimya
 
Ni watu wawil tofauti , sii mtu mmoja, huyo Ontario wa Twitter ni mtu tu kaamua kutumia hilo jina ila Sio mtu mmoja, wote niko nao group moja WhatsApp

ni watu wawili tofaut, hiyo pesa atapewa j5 nitawaletea credentials hapa muingie kwenye accounts muangalie anavyo trade, watu wawil tofauti kabisa

kama issue ingekua "watu wanao juana" somehow ingemake sense, ila sio mtu mmoja huyo
Kwa haya maelezo yako hapa, ninaweza kuthibitisha jambo moja kubwa hapa kuwa wewe, Ontario wa twitter na SirJeff wa twitter ni timu mmoja.
Ni miongoni mwa zile ID za .....
 
Ontario A.K.A sirjeff alituanzia mbali na story za kukodi trekta, baadae ikaja forex watu wakaingia jangidi plaza ikaja kufa kibudu, mjifunze hakuna pesa ya bure au rahisi kiasi hicho mtaja achiwa manyoya
Kwa hiyo hiyo TMT ilikufa? Ofisi ya Jangid Plaza nayo ilifungwa?

Kama ni ndiyo, sababu ni nini? Mambo hayakwenda vizuri?
 
Ni watu wawil tofauti , sii mtu mmoja, huyo Ontario wa Twitter ni mtu tu kaamua kutumia hilo jina ila Sio mtu mmoja, wote niko nao group moja WhatsApp

ni watu wawili tofaut, hiyo pesa atapewa j5 nitawaletea credentials hapa muingie kwenye accounts muangalie anavyo trade, watu wawil tofauti kabisa

kama issue ingekua "watu wanao juana" somehow ingemake sense, ila sio mtu mmoja huyo
Sawa tunasubiri huo mrejesho wako, ila elewa ontario fx, hiyo fx inamaanisha forex. Na juzi tu kigogo katoka kumuumbua hadi chumba anachokaa alichokodi kimara kwa 40,000. Watu tumemtaka walau apost hata stakabadhi aliyonunua umeme tu yenye jina lake ameshindwa, ije kuwa kumlipa mtu 200US$
 
Unataka kusemaje..dizain sijakuelewa
 
Hebu angalia account yangu imefunguliwa lini hii?

Sirjeff huyo hapo na Ontario huyo hapoView attachment 1562189
Hii michezo watu tunaijua sana, binafsi nimeshafanya sana facebook kipindi hicho sina dem, nikawa natengeneza account nyingine kwa jina la kike na mpaka picha naweka za kike. Lengo ni kujitxt na kujijibu angalau washkaji wajue nimepata dem.
 
Sawa tunasubiri huo mrejesho wako, ila elewa ontario fx, hiyo fx inamaanisha forex. Na juzi tu kigogo katoka kumuumbua hadi chumba anachokaa alichokodi kimara kwa 40,000. Watu tumemtaka walau apost hata stakabadhi aliyonunua umeme tu yenye jina lake ameshindwa, ije kuwa kumlipa mtu 200US$
Hakuna alicho Umbua bwana Kigogo, hii story aliipost Sirjeff mwenyewe tar 11 mwez wa nane.. ina zaid ya mwezi kule, kigogo kaibeba juzi kapost, kaitoa kwenye page ya Sirjeff pale pale, hakuna alicho umbuliwa
Screenshot_20200907-212533.jpg
Screenshot_20200907-212555.jpg
 
Hii michezo watu tunaijua sana, binafsi nimeshafanya sana facebook kipindi hicho sina dem, nikawa natengeneza account nyingine kwa jina la kike na mpaka picha naweka za kike. Lengo ni kujitxt na kujijibu angalau washkaji wajue nimepata dem.
Pole.. angalia saiv ni saa ngapi na screenshot nimepiga mda gan.. na hiyo editing nimeifanyia kwenye status nika screenshot hapo
 
Amemuumbua kwa maana hata humu JF hakuna aliekuwa anamfahamu Ontario kwa sura, licha ya kuwaliza watu wengi.
Insta ina follower zaid ya elfu 20, YouTube channel follower elfu 25 , hakuna aliekua anamjua kwa sura?? unajua maana ya kuumbua ?

hiyo story asingeileta yeye akaileta kigogo hapo kidogo ingemake sense ila kaileta mwenyewe utasemaje kaumbuliwa???
 
Binafsi mimi nafanya pia forex ila sio ile ya kufundishwa na Ontario, hapana.

Nimejifunza kwa muda mrefu lakini hadi sasa sijapata mafanikio yoyote na hii huenda ikatokana na kuwa bado sijakomaa sana kwenye forex(sio trader mzuri). Hivyo nimepata na napata loss, faida mara moja moja sana na baada ya muda narudia tena loss.

Nilichogundua ni kuwa forex ni ngumu inahitaj muda zaidi kujifunza na kuweza kujimudu ku-trade. Ontario kama kawaida yake alianza na stori nzuri nzuri sana kama alivyoanza huku JF. Uzuri kule alifikia hatua hadi ya kuwapa watu pesa 100k kupitia challenges ambazo anaziandaa.

Anaweza kuamka tu na kusema leo atayefanya hivi nampa laki. Baadae akaanza kusimulia yote yaliyotokea hadi TMT kufa(one side story).

Kila aliyefatilia aliona kuwa huyu kijana ana kitu kikubwa ndani yake, akaongeza followers wengi kwa muda mfupi kwa jinsi anavyoelezea angle zote za biashara zilivyo na haswahaswa hii forex.

Mwanzoni alianza kukataa katakata kwa kusema atafundisha vyote ila sio forex (ilikuwa trick watu waone forex it's a big deal).

Ghafla bin vuu, akaanza kuponda fani za watu na pia kujionyesha sana kuwa ni moja wa successful traders na yupo vizuri financially, watu wakawa wengi kufatilia ( kama kawaida wabongo tunapenda sana shortcut).

Baadae akaanza kusema yupo tayari kusaidia watu waijue forex na hatimaye waanze kudownload pesa. Ila aliweka masharti ya hapa na pale, kikubwa kuchanganyachanganya watu na hatimae waone hana shida sana ya kufundisha watu forex.

Alikuwa tayari kishaplan kuanza kutrain tena watu forex, baada ya watu wengi kuonyesha wana interest ya kuijua forex. Ila kuna watu baadhi kule wana akili sana, maswali yalikuwa mengi sana kwake kuliko majibu na kuishia kuanza ku-block watu ili abaki na wale tu ambao wapo tayari shingo zao kupita kwenye kisu.

Ghafla bin vuu, lile kundi kubwa likapata support kutoka kwa watu wengine na kuambiwa "shtukeni mnaenda kupigwa, hana lolote huyo. Hapo kinachotafutwa ni pesa za kiingilio kwenye training. Na baadae mkionyesha mnaliwa sana wakati wa kutrade mtambiwa "forex is not for everyone". Cha kushangaza sasa hivi hawaambiwi forex is not for everyone, wanakaribishwa vizuri sana.

Ila watu wa kule wengi wana akili, wanajua kabisa 1+1=2 , wamempa mtihani mdogo sana " nunua umeme hata wa buku(1000) alafu tutumie hayo malipo" lengo hapo waone kama hata anamiliki kibanda.

Kwanini wanamuambia hivyo? Kwa sababu ya approach zake alizoanza nazo huko za kujionyesha ana pesa sana.

Twitter kuna watu wengi sana wana akili, bado wale wa Instagram
Yule dogo wa South Africa mbona anavuna utajiri kupitia forex amewezaje?
 
Inasikitisha sana kuona watu wazima dizaini yenu kumuandama kijana wawatu miaka yote chochote afanyacho kwenu ni mavi huu uungu munaojipa wakifedhuri ni ujahili wa hali ya juu usije furahia stuation kama hii kama kijana kama jamii ishakuwa yakifedhuri kihasi hiki hata wewe inaweza kukitokea.
 
Insta ina follower zaid ya elfu 20, YouTube channel follower elfu 25 , hakuna aliekua anamjua kwa sura?? unajua maana ya kuumbua ?

hiyo story asingeileta yeye akaileta kigogo hapo kidogo ingemake sense ila kaileta mwenyewe utasemaje kaumbuliwa???
Tunasubiri ushuhuda wako kuwa Ontario sio Sir_JeffDenis
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom