Only in Kenya this can happen, viwanja vya ndege vina mashimo.

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
26,117
46,613
Wakati mkinya mmoja aliyetembelea Tanzania ameandika kwa undani jinsi alivyopendezwa na miundombinu ya Tanzania ikiwemo barabara, alifurahishwa sana kuona kwamba hakuna mashimo(potholes) katika barabara za Tanzania, ukilinganisha na barabara za Kenya zenye mashimo kama karai za kupikia vitumbua.

Kumbe hakujua kwamba, hata katika viwanja vya ndege vya Kenya pia kumejaa mashimo katika njia za kuruka na kutua ndege. Ndege ya Fly 540 almanustra kupata ajali katika kimoja wapo ya viwanja vya ndege huko Kenya, baada ya gurudumu lake moja kutumbukia katika shimo linalokisiwa kuwa na kina cha 30cm, na kusababisha taharudi kwa abiria 36 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
 
Back
Top Bottom