Online Tv zinazofanya mahojiano ya kudhalilishana na kukiuka Maadili ya Nchi kufungiwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile, amesema kuwa online TV zote ambazo zinafanya mahojiano ya kudhalilishana na zile zinazokiuka maadili na utamaduni wa nchi zitafungiwa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua za kisheria.
Submitted by Agnes Kibona on Jumanne, 9th Mar, 2021

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 9, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, wakati akizungumzia usajili wa akaunti za Youtube ambao kwa sasa umesitishwa kwa muda hadi pale kanuni mpya zitakapotolewa.

"Kulikuwa na mfumuko wa online TV nyingi sasa mtu anaenda kufanya mahojiano wanaongea vitu vya hovyo sana, sisi kama serikali hatuwezi tukasubiri wanadhalilishana wanaongea vitu ambavyo ni kinyume na maadili na tamaduni zetu za nchi na hizo zote tunaenda kuzifunga zote na kuwachukulia hatua wamiliki wake," amesema Dkt. Ndugulile.

"Tunatambua kuna watu ambao wana YouTube akaunti na zinawaingizia fedha nyingi sana na saa nyingine watu wanaiweka serikali katika nafasi ngumu sana inabidi tupitie tena sababu kuna wasanii walikuwa wanataka kusajili YouTube yao sasa hivi imebidi tusimamishe na tuweke utaratibu mpya," ameongeza.

EATV
 
Submitted by Agnes Kibona on Jumanne , 9th Mar , 2021
Kuna online TV ni nyimbo za matusi na ngono kwakwenda mbele, zinatuharibia sana utamaduni wetu
 
Nilishawahi kusema hii wizara na huyu waziri wamewekwa pale kudhibiti mitandao ya kijamii kama walivyofanya kwa tv na magazeti ya nchi.

Jiwe alikwisha omba malaika washuke na kuzifungia social media zote.

Kazi imeenza kwani Ndugulile anakumbuka kilicho mfika alipo acha kusifu na kuabudu "hekima"😷za Meko.
 
Mitano tena! yaani watawafikia hata wasoma magazeti kuwa lazima ununue zile takataka za kina Musiba.
 
Hongera zake Waziri. Ni jambo jema. Kwani mahojiano mengine yalikuwa ni ya hovyo kabisa.

Tatizo watu wa "maana" hawataki kutumia au kuhojiwa na online TV.

Mfano kuna maudhui mengi ya kuongelewa na "watu-wa-maana" iwe masuala ya burudani, utamaduni, historia, safari za mabaharia wa nchi kavu na majini, elimu, uchumi, siasa n.k lakini hawajitokezi wa kuhojiwa wala kuanzisha channels zao.

Tatizo ni nini ? Ni mfumo gandamizi wa mamlaka za serikali kupitia ada, kodi,usajili na tozo, hofu au ni suala la "kiutamaduni" kuwa kila kitu chetu tunafanya siri iwe ni "uganga", elimu, habari na uzoefu wa maisha ulionao ni jadi yetu kuificha.

Huwezi kuona makala au mahojiano ya maprofesa wetu wa vyuo vya ya elimu ya mitandaoni iwe ni katika fani ya ulozi , uchumi, afya, muziki, diplomasia n.k.

Ombwe hilo kukosekana mahojiano na watu wa "maana" wanaoongelea masuala mengine limezingirwa / jazwa na wahubiri dini mitandaoni masuala ya udaku, sherehe za birthday, mazishi na "uchambaji".

Si kwamba kusheheni kwa mambo hayo ya udaku n.k ni kubaya mitandaoni kwa taswira ya Tanzania bali Wizara sasa iwahimize hao wengine watu wa "maana" wajitokeze ku-'share' kwa wingi mambo yao kwa serikali kuandaa sera nzuri na rafiki isiyo na gharama kubwa au kutiwa hofu ili content / maudhui mengine pia yajae mitandaoni.

Nchi zingine raia wao mitandaoni wamejaza kila aina ya maudhui / contents kiasi huwezi kuona habari zao za mitandaoni kama zimeelemea upande wa u freemasons, udaku, ulozi na ngono. Nini siri ya watu wa Mataifa mengine kuwa na mchanganyiko wa maudhui mtandaoni?

Nafikiri nchi hizo zingine zimefanikiwa kuwa na mchanganyiko wa habari mbalimbali kutoka makundi mbalimbali ya kijamii kutokana na kujengeka uhuru wa kutoa na kusambaza habari na mwishowe hakuna habari za aina moja zika trend kupitiliza kuliko zingine kwa muda wa saa 24 ya siku, wiki, mwezi, robo mwaka , nusu mwaka na mwaka mzima labda tu kunapotokea jambo zito ktk jamii basi lita-trend kwa muda kabla ya kupoa au kupotea.

Mwisho ni wakati wa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile na taasisi zilizo chini yake pamoja na serikali waje Jamiiforums na kujifunza vipi mtandao huu umesheheni habari za kila aina kuanzia burudani mpaka mambo ya kitaalamu na watu wanafurahi hali hii ya maudhui kibao Jamiiforums labda serikali tu ndiyo kidogo inachukia kukosolewa au kupewa ushauri kuhusu siasa na utawala bora.
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile, amesema kuwa online TV zote ambazo zinafanya mahojiano ya kudhalilishana na zile zinazokiuka maadili na utamaduni wa nchi zitafungiwa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua za kisheria.
Submitted by Agnes Kibona on Jumanne, 9th Mar, 2021

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 9, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, wakati akizungumzia usajili wa akaunti za Youtube ambao kwa sasa umesitishwa kwa muda hadi pale kanuni mpya zitakapotolewa.

"Kulikuwa na mfumuko wa online TV nyingi sasa mtu anaenda kufanya mahojiano wanaongea vitu vya hovyo sana, sisi kama serikali hatuwezi tukasubiri wanadhalilishana wanaongea vitu ambavyo ni kinyume na maadili na tamaduni zetu za nchi na hizo zote tunaenda kuzifunga zote na kuwachukulia hatua wamiliki wake," amesema Dkt. Ndugulile.

"Tunatambua kuna watu ambao wana YouTube akaunti na zinawaingizia fedha nyingi sana na saa nyingine watu wanaiweka serikali katika nafasi ngumu sana inabidi tupitie tena sababu kuna wasanii walikuwa wanataka kusajili YouTube yao sasa hivi imebidi tusimamishe na tuweke utaratibu mpya," ameongeza.

EATV

Ni ujinga wa ajabu maana mtu yeyote anaweza kutuma video youtube tofauti ni kwamba mkizuia hizo kampuni hamtapata kodi lakini habari zitatoka tu tupende tusipende.
 
Tatizo watu wa "maana" hawataki kutumia au kuhojiwa na online TV.

Mfano kuna maudhui mengi ya kuongelewa na "watu-wa-maana" iwe masuala ya burudani, utamaduni, historia, safari za mabaharia wa nchi kavu na majini, elimu, uchumi, siasa n.k lakini hawajitokezi wa kuhojiwa wala kuanzisha channels zao.

Tatizo ni nini ? Ni mfumo gandamizi wa mamlaka za serikali kupitia ada, kodi,usajili na tozo, hofu au ni suala la "kiutamaduni" kuwa kila kitu chetu tunafanya siri iwe ni "uganga", elimu, habari na uzoefu wa maisha ulionao ni jadi yetu kuificha.

Huwezi kuona makala au mahojiano ya maprofesa wetu wa vyuo vya ya elimu ya mitandaoni iwe ni katika fani ya ulozi , uchumi, afya, muziki, diplomasia n.k.

Ombwe hilo kukosekana mahojiano na watu wa "maana" wanaoongelea masuala mengine limezingirwa / jazwa na wahubiri dini mitandaoni masuala ya udaku, sherehe za birthday, mazishi na "uchambaji".

Si kwamba kusheheni kwa mambo hayo ya udaku n.k ni kubaya mitandaoni kwa taswira ya Tanzania bali Wizara sasa iwahimize hao wengine watu wa "maana" wajitokeze ku-'share' kwa wingi mambo yao kwa serikali kuandaa sera nzuri na rafiki isiyo na gharama kubwa au kutiwa hofu ili content / maudhui mengine pia yajae mitandaoni.

Nchi zingine raia wao mitandaoni wamejaza kila aina ya maudhui / contents kiasi huwezi kuona habari zao za mitandaoni kama zimeelemea upande wa u freemasons, udaku, ulozi na ngono. Nini siri ya watu wa Mataifa mengine kuwa na mchanganyiko wa maudhui mtandaoni?

Nafikiri nchi hizo zingine zimefanikiwa kuwa na mchanganyiko wa habari mbalimbali kutoka makundi mbalimbali ya kijamii kutokana na kujengeka uhuru wa kutoa na kusambaza habari na mwishowe hakuna habari za aina moja zika trend kupitiliza kuliko zingine kwa muda wa saa 24 ya siku, wiki, mwezi, robo mwaka , nusu mwaka na mwaka mzima labda tu kunapotokea jambo zito ktk jamii basi lita-trend kwa muda kabla ya kupoa au kupotea.

Mwisho ni wakati wa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile na taasisi zilizo chini yake pamoja na serikali waje Jamiiforums na kujifunza vipi mtandao huu umesheheni habari za kila aina kuanzia burudani mpaka mambo ya kitaalamu na watu wanafurahi hali hii ya maudhui kibao Jamiiforums labda serikali tu ndiyo kidogo inachukia kukosolewa au kupewa ushauri kuhusu siasa na utawala bora.
Asilimia kubwa ya watanzania wanapenda kufatilia mambo ya kimbea+upuz
Ndomana hawa wenye online tv habari zao zimejaa mambo hayo

Ova
 
Yatakuwa yale mahojiano ya PLO Lumumba yamewatibua nyongo. Ngoja tuone Mapuli kama watamvisha kipuli.
 
Back
Top Bottom