Online Tv zinazofanya mahojiano ya kudhalilishana na kukiuka Maadili ya Nchi kufungiwa

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile, amesema kuwa online TV zote ambazo zinafanya mahojiano ya kudhalilishana na zile zinazokiuka maadili na utamaduni wa nchi zitafungiwa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua za kisheria.
Submitted by Agnes Kibona on Jumanne, 9th Mar, 2021

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 9, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, wakati akizungumzia usajili wa akaunti za Youtube ambao kwa sasa umesitishwa kwa muda hadi pale kanuni mpya zitakapotolewa.

"Kulikuwa na mfumuko wa online TV nyingi sasa mtu anaenda kufanya mahojiano wanaongea vitu vya hovyo sana, sisi kama serikali hatuwezi tukasubiri wanadhalilishana wanaongea vitu ambavyo ni kinyume na maadili na tamaduni zetu za nchi na hizo zote tunaenda kuzifunga zote na kuwachukulia hatua wamiliki wake," amesema Dkt. Ndugulile.

"Tunatambua kuna watu ambao wana YouTube akaunti na zinawaingizia fedha nyingi sana na saa nyingine watu wanaiweka serikali katika nafasi ngumu sana inabidi tupitie tena sababu kuna wasanii walikuwa wanataka kusajili YouTube yao sasa hivi imebidi tusimamishe na tuweke utaratibu mpya," ameongeza.

EATV
Kwahiyo tunao miliki online TV tujiandae sio
 
Back
Top Bottom