Online storage -wapi ni bei rahisi?

rakeyescarl

JF-Expert Member
Dec 9, 2007
481
145
Waheshimiwa,
Natanguliza shukurani na salaam.
Naomba kujua wapi naweza kupata online storage kwa bei rahisi 1TB inanitosha kabisa,nikipata ambayo naweza kutumia kwa computer 2 ningeshukuru, asanteni.
 
1TB ni nyingi sana mkuu, unaweza kuangalia Amazon S3 hawa wanacharge kwa matumizi ila kuna learning curve kidogo itakukost kama $140 kwa mwezi for 1 TB, highly reliable hawajawahi kupoteza file.

Kuna hizi ambazo wanasema ni unlimited kama Back Blaze (Easiest Online Backup Service - Backblaze) ila ni unlimited kwa file ambazo ziko kwenye harddrive yako ukidelete file kwenye PC na wao wanaidelete kwenye server zao. Hii ni backup service ambayo inakuja na software yake inabackup automatically. $4 kwa mwezi. Kuupload 1TB inaweza ikakuchukua miezi.

Natumiaga iDrive.com 150GB ila ni true backup hawadelete kitu.

Kama unafanya backup ningekushauri kuangalia ni vitu gani hasa vinahitaji backup, vitu ambavyo hauwezi kuvipata tena vikipotea picha zako, documents etc hakuna haja ya kubackup movie uliyodownload au DVD ya Windows, utaokoa gharama.

Nimegoogle nimekutana na hii wanadai 2TB for $16/mwezi sijawahi kuisikia before http://www.livedrive.com inaonekana too good to be true.
 
Back
Top Bottom