Online Puppets: Kumbe Tunao "Puppets" Wengi Kuliko Tunavyojidhania!

Hivi wewe serikali ya USA na Serikali ya TZ vikatolea tamko jambo fulani utaamini tamko ya serikali gani? Be sincere. Kama USA ndiyo ilishinikiza na kusimamia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa nini tusiamini amneno yao kwamba Muungano ulikuwa ratified Zanzibar.

BTW, hivi SMZ inasemaje? sio maneno yako? Tunataka SMZ isema kama Muungano ulikuwa ratified ZNZ au hapana. Kama watakaa kimya as expected tutawaamini Wamarekani.

Pamoja na chuki zako dhidi ya USA lakini USA hawana longolongo kama sisi (Watanzania)!
Bobuk, kwa vile muungano ni Tanganyika na Zanzibar, ratification ni Tanganyika na Zanzibar. Ratification ilifanyika Tanganyika tuu na Zanzibar ilisemwa tuu kuwa imefanyika, lakini in actual haikufanyika!. Hao majasusi wa Marekani CIA, ile kusikia tuu ratification imefanyika, wao ni mbio wakapeleka maumbea kwao kuwa ratification imefanyika na ndio wenzetu wanawaaminia sana hao wamarekani, na wewe unaweza kuwa uu mmoja wao, leo namaliza kazi!.

On the other way, sina chuku na Marekani, nimeishi huko, wife wangu na sehemu ya familia yangu ni residents huko, kila mara nakwenda huko hivyo sina chuki!.

Sipendi kitendo cha wazalendo wenzetu kuwaaminia sana mabeberu hawa kuwa wanachosema wao ndicho!. Hili la ratification nimelitaja mimi humu, hata sijauluzwa ukweli wangu ni upi, nineitwa muongo na mzushi na kushushiwa uthibitisho wa ma CIA wa Marekani waliokuwepo Zanzibar ambao walithibitisha ratification ilifanyika!.

Lengo la thread hii ni kuwatolea angalizo hao wategenea CIA wasije kuwa ni puppets wa Wamarekani dhidi ya nchi yao!.

Muungano wowote ni jambo jema japo una matatizo. Kama zilivyo ndoa, ikiingia kwenye migogoro juhudi za kwanza ni kujaribu kuutatua mgogoro ili ndoa hiyo idumu. Ukiona mtu anashadidia kuivunja ndoa badala ya kuinusuru, juilize malengo yake ni nini ndoa ikishavunjika!.

Hivyo ndivyo ulivyo sasa kwa muungano, jee ndoa hii imeishafikia stage ya "irreperable demage" beyond controll ambayo ni lazima ndoa hii sasa ivunjike? au ni kazi ya puppets tuu kutaka ivunjike kwa manufaa ya hao wanaowafanyia huo u- puppet?!.
 
Kwa kuwa hoja ya Pasco ipo sana kwenye Internationa Treaty ratification : Naomba kuuliza swali.....Je nini viashiria vya kuonyesha kuna ''International Treaty'' ratification nchi mbili zinapoungana.....
Chakarimkopo, jibu litakuwepo kwenye mada yangu kuu ya leo kuhusu ratification!.
 
By Mihango...
Siku tatu baada ya kutiwa sahihi Mkataba huo, Aprili 25, 1965; mabunge ya nchi hizo mbili, (kwa Zanzibar, Baraza la Mapinduzi) kila moja mahali pake, yalikutana kuridhia Mkataba huo wa kimataifa kwa njia ya Sheria za Bunge, zinazojulikana kama “Sheria za Muungano” (Acts of Union), kufanya makubaliano yaliyofikiwa kuwa na nguvu ya kisheria kwa nchi husika na kwa utekelezaji.
Kwa Tanganyika inajulikana kama Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Namba 22 ya 1964; na kwa Zanzibar ni Sheria ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, iliyotangazwa katika Gazeti la Serikali Namba 243 la Mei 1, 1964.

Hapa ndipo ulipolala mzizi wa fitna, imeelezwa uliridhiwa na nchi zote mbili!, ratification ya Tanzania ipo hili tangazo la GN 243 ni ratification ya Tanganyika!, hiyo ya Zanzibar is no where kwa sababu haikufanyika!. Inatajwa tuu kuwa ilifanyika ila kiukweli, haikufanyika!.

Hii ndio mada yangu ya leo!.

Pasco.
 
Pasco, hiyo ni sehemu ya article aliyoandika Mihango. Sasa unataka kutuambia kuwa Mihango ni 'black box' ya muungano au/na wewe ni 'puppet' wa Mihango?

Logically, kama Zanzibar hawaku-ratify huu muungano na kwanini kwa miaka 48 BLM hawajatangaza kuwa muungano ni batili? Na UN walitumia 'nini' kuondoa viti vya Zanzibar na Tanganyika na ku-replace na kiti cha Tanzania kwenye baraza la umoja wa mataifa?
 
Uzalendo ni kutanguliza utaifa mbele ukiwemo heshima na nidhamu kwa viongozi wako. Kama Marekani wamedai rais wako kahongwa suti, Ikulu yako ikakanusha na kusema ni uongo bila hata kuitaka Marekani iwaombe radhi kumchafua rais wao, then mtoto mwenye busara atajua kinachoendelea na uzalendo sio kukubali rais wetu alihongwa suti, bali kuungana na msimamo wa Ikulu yetu, kuwa rais wetu amesingiziwa!.

Hivi kuna mtu hajamuelewa Pasco ni mtu wa level gani??, kwa kifupi Pasco anasisitiza tuwe wanafiki Rais akichemka na akasutwa na mtu wa nje, sisi tuwe upande wake na tuendelee kumuimbia nyimbo za sifa kama nimemuelewa vema hiyo ndiyo definition ya Uzalendo kwake yeye.
 
By Mihango...
Siku tatu baada ya kutiwa sahihi Mkataba huo, Aprili 25, 1965; mabunge ya nchi hizo mbili, (kwa Zanzibar, Baraza la Mapinduzi) kila moja mahali pake, yalikutana kuridhia Mkataba huo wa kimataifa kwa njia ya Sheria za Bunge, zinazojulikana kama “Sheria za Muungano” (Acts of Union), kufanya makubaliano yaliyofikiwa kuwa na nguvu ya kisheria kwa nchi husika na kwa utekelezaji.
Kwa Tanganyika inajulikana kama Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Namba 22 ya 1964; na kwa Zanzibar ni Sheria ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, iliyotangazwa katika Gazeti la Serikali Namba 243 la Mei 1, 1964.

Hapa ndipo ulipolala mzizi wa fitna, imeelezwa uliridhiwa na nchi zote mbili!, ratification ya Tanzania ipo hili tangazo la GN 243 ni ratification ya Tanganyika!, hiyo ya Zanzibar is no where kwa sababu haikufanyika!. Inatajwa tuu kuwa ilifanyika ila kiukweli, haikufanyika!.

Hii ndio mada yangu ya leo!.

Pasco.
 
Pasco, hiyo ni sehemu ya article aliyoandika Mihango. Sasa unataka kutuambia kuwa Mihango ni 'black box' ya muungano au/na wewe ni 'puppet' wa Mihango?

Logically, kama Zanzibar hawaku-ratify huu muungano na kwanini kwa miaka 48 BLM hawajatangaza kuwa muungano ni batili? Na UN walitumia 'nini' kuondoa viti vya Zanzibar na Tanganyika na ku-replace na kiti cha Tanzania kwenye baraza la umoja wa mataifa?
Tusubiri darasa atukate kiu lakini nadhani litakuwa ni evening class...kwa sasa bado mwalimu anaandaa material...
 
Uzalendo ni kutanguliza utaifa mbele ukiwemo heshima na nidhamu kwa viongozi wako. Kama Marekani wamedai rais wako kahongwa suti, Ikulu yako ikakanusha na kusema ni uongo bila hata kuitaka Marekani iwaombe radhi kumchafua rais wao, then mtoto mwenye busara atajua kinachoendelea na uzalendo sio kukubali rais wetu alihongwa suti, bali kuungana na msimamo wa Ikulu yetu, kuwa rais wetu amesingiziwa!.
Tokea nimejiunga na Jf sijawahi kuguswa kama ilivyo nigusa hii kauli:angry::angry::angry::angry:
 
'' kwanini kwa miaka 48 BLM hawajatangaza kuwa muungano ni batili? Na UN walitumia 'nini' kuondoa viti vya Zanzibar na Tanganyika na ku-replace na kiti cha Tanzania kwenye baraza la umoja wa mataifa?[/QUOTE]

....Kiashiria cha kwanzo hicho......asante sana
 
Mkuu Jasusi,

Uzalendo ni kutanguliza utaifa mbele ukiwemo heshima na nidhamu kwa viongozi wako. Kama Marekani wamedai rais wako kahongwa suti, Ikulu yako ikakanusha na kusema ni uongo bila hata kuitaka Marekani iwaombe radhi kumchafua rais wao, then mtoto mwenye busara atajua kinachoendelea na uzalendo sio kukubali rais wetu alihongwa suti, bali kuungana na msimamo wa Ikulu yetu, kuwa rais wetu amesingiziwa!.
Pasco?? Kijiko ni kijiko,otherwise huu ndio ugonjwa unaoitafuna Tanzania!
 
Pasco Umaskini wetu ndio unaotutafuna, So lazima tukubali yote watakayo tueleza,Umesahau order ya Cameroon?
 
Last edited by a moderator:
Pasco, hiyo ni sehemu ya article aliyoandika Mihango. Sasa unataka kutuambia kuwa Mihango ni 'black box' ya muungano au/na wewe ni 'puppet' wa Mihango?

Logically, kama Zanzibar hawaku-ratify huu muungano na kwanini kwa miaka 48 BLM hawajatangaza kuwa muungano ni batili? Na UN walitumia 'nini' kuondoa viti vya Zanzibar na Tanganyika na ku-replace na kiti cha Tanzania kwenye baraza la umoja wa mataifa?
Mkuu FJM,
Huu muungano wetu ni very unique, baada ya bunge la Tanganyika ku ratify muungano, nchi inayoitwa Tanganyika seazed to exist so do Zanzibar by then jina la Tanzania lilikuwa bado halijapatikana hiyo mwanzo iliitwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika and Zanzibar.

Japo nchi iliyofutika kwenye ramani ya dunia ni Tanganyika, kiutendaji nchi uliyokufa kwenye medani za kimataifa ni Zanzibar na Tanganyika ilibadili tuu jina kuitwa Tanzania.

Hiyo baada ya muungano katika medani za kimataifa Zanzibar doesn't exist anymore mpaka kesho!.

Kitaifa muungano wetu ni wa nchi mbili lakini kimataifa muungano wetu ni wa nchi moja tuu Tanzania, yaani ni unitary union na sio federetion. Hivyo kwenye UN ilipelekwa barua moja tuu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar as there was no any more Zanzibar!.

Kiukweli Nyerere alikuwa na good faith na muungano huu toka moyoni mwake kuwa ni wa nchi moja ya Tanzania ndio maana no one gave a damm kama Zanzibar ikifanya ratification or not.

Kama zilivyo ndoa, ndoa hufungwa kwa tamko tuu la kauli ya "ndiyo" na hati za ndoa husainiwa baadae!.

Ukishatamka "ndiyo" ndoa ni tayari hata kama baadae mke atagoma kusaini hati ya ndoa!. Ndoa itabaki ni ndoa halali isiyo na uhalali wa kisheria!.

Sio kila ndoa ina uhalali wa kisheria ndio maana na void marriages na voidable marriages!.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa mikataba, kuna void contract na voidable contracts. Mkataba wa muungano umekuwa voidable na sio void, zile sababu za zinazoufanya uwe voidable zinarekebishika na mkataba unaendelea.

Kama ukishafungishwa ndoa hata bila kusaini cheti cha ndoa, ndoa ipo na as long as unatimiza majukumu yako yote ya kindoa, then there is no complain !.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Zanzibar, hata kama hawakuridhia rasmi hati za muungano na wametekeleza majukumu yote ya muungano bila kipingamizi chochote, then it was presumed ndoa yetu iko ok hadi leo hakuna anayelalamika!.

Tukubali tukatae, tuliuendesha muungano kibabe!. Ndio maana tuliyaongeza mambo ya muungano toka yale 11 hadi 26 bila kushauriana na Zanzibar!.

Hapa kiukweli Tanzania ilitumia mfumo dume kufikia baadhi ya maamuzi kwa kuihesabu Zanzibar kama mke!. Ukishaoa kuna maamuzi unaweza kuyachukua kwa kumshauri mkeo na kuna maamuzi unaweza kuyachukua na kumuarifu tuu atake asitake!.

Mfano baada ya ndoa ya Tanganyika na Zanzibar, mume na mke walikula meza moja kwa mmoja kuwa rais mwingine kuwa makamo. Baadae mume akanote mke ana ghubu sana, akaamua kumfukuza mezani yeye atakuwa akilia jikoni na sio mezani tena kwa kumuengua rais wa Zanzibar asiwe makamo tena hivyo kumreduce into nothing bila ya mashauriano yoyote!.

Wakati wa ndoa Karume alimwambia wewe rais, mimi makamo!, kitendo cha kumfanya rais wa Zanzibar ni nothing ndani ya muungano ni ukiukwaji mkubwa sana wa hati za muungano!.

Zanzibar ni kama mke jeuri, kama bado unampenda sana, huna budi kumshikisha adabu!. Ila ukipata uhakika mkeo amepata bwana mwingine anayemtosheleza kukushinda wewe, ataanza visa ili utoe talaka, kama ni ndoa ya Kiislamu, bora umpe talaka yake muachane kwa amani!.

Kwa taarifa tuu huyu mke wetu anayeleta chokochoko, kapata bwana wa Kiarabu anayemtimizia mambo yale ya Kizanzibari ambayo siye wabara siyo jadi yetu!.

Ndio maana kwenye hili la "let them go, mimi na Mwanakijiji letu ni moja!"!.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Pasco, waMarekani wanaweza kuwa na access ya mambo yetu ya ndani kuliko hata sisi wenyewe tunvyojijua.

Mabomu ya G -Mboto yalipolipuka, serikali wazo lao la kwanza lilikuwa kufanya uchunguzi wa kina, kwa kushirikiana (kusaidiwa?) na "wenzetu" Wamarekani. Hivu unaweza kuimagine Marekani kushirikiana na Russia kuchunguza ghala za kuhifadhia silaha za Kimarekani?

Kwetu sisi hatujawaficha kitu waMarekani, hata siri zetu za Ulinzi na Usalama wamekaribishwa kuzifahamu, halafu wewe unasema jambo dogo kabisa kama Muungano wa Tanganyika na visiwa vyake?
 
'' kwanini kwa miaka 48 BLM hawajatangaza kuwa muungano ni batili? Na UN walitumia 'nini' kuondoa viti vya Zanzibar na Tanganyika na ku-replace na kiti cha Tanzania kwenye baraza la umoja wa mataifa?

....Kiashiria cha kwanzo hicho......asante sana[/QUOTE]
Chakarikamkopo, hakuna aliyesema muungano ni batili!. Muungano sio batili ni halali kabisa ila tuu haukuhalalishwa kwa upande wa Zanzibar!.

Kama ilivyo ndoa, mnaweza kufunga ndoa halili na kama msipo i consumate hiyo ndoa yenu. inakuwa ni voidable marriage inaweza kubatilika mkikubali ku i consumate inakuwa ni ndoa halali na msipo i consumate mmoja wenu hatahitaji kuomba talaka bali ni kuiomba tuu mahakama kuibadilisha ndoa hiyo!.

Muungano ni halali ila kwa vile Zanzibar hawakuuridhia, hawahitaji talaka kutoka ndani ya ndoa hii bali kumjulisha jaji kua hawakuiridhia!.
 
Pasco, hiyo ni sehemu ya article aliyoandika Mihango. Sasa unataka kutuambia kuwa Mihango ni 'black box' ya muungano au/na wewe ni 'puppet' wa Mihango?

Logically, kama Zanzibar hawaku-ratify huu muungano na kwanini kwa miaka 48 BLM hawajatangaza kuwa muungano ni batili? Na UN walitumia 'nini' kuondoa viti vya Zanzibar na Tanganyika na ku-replace na kiti cha Tanzania kwenye baraza la umoja wa mataifa?

Ndio wanatangaza sasa huko zanzibar mkuu!

ukimsoma Mihangwa amequote..(mabunge yalikaa) lakini yeye mwenyewe kwenye zile series ya nakala yake anakiri kuwa Hakuna sehemu yeyote au uthibitisho wowote unaoonyesha bunge la zanzibar lilikaa kukubali

after all muungano uliishsainiwa tangu tarehe 22!!! within an hour karume na timu yake wakakubali kuweka signature zao!!

funny
 
Napenda unavyojenga hoja na kuzitetea, napenda unavyoweza kufikiri na kuwashirikisha wenzako, napenda unavyoheshimu michango ya wenzako. Hakika nakuona kama Mtanzania bora kabisa. Nafurahishwa sana unavyoitumia taaluma ya kisheria katika hoja hii ya muungano. Naamini wewe ni mwanfunzi bora kabisa wa sheria. Mungu akusaidie.

Maelezo ya hoja yako yana ukweli fulani, yapo mazingira ambayo dhana yako ni sahihi na wakati mwingine sio sahihi. Hebu fikiria kidogo, ungekuwa unatamani uwe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia ya kuwakomboa watanzania wenzako ambao wamenyonywa na kudharirishwa kwa muda mrefu. Na mbaya zaidi unanyonyaji unafanywa na watanzania wenzao. Ukiwa katika harakati hizo likatokea kundi ambalo kusema kweli haujui lengo lake lakini linatakakusaidia kuipata hiyo nafasi na unaamini kwamba msaada huo ni dhahiri na utakusaidia. Je, utaukubali msaada huo?

Kama wenye ni "strategist" nadhani utaupokea japo utajiwekea tahadhari fulani ili usije ukatumika vibaya hapo mbeleni. Yawezekana Mwl. Nyerere na hata Mheshimiwa Karume walipambana na upinzani mkubwa na upinzania ambao wakati mwingine ulikuwa unatishia uhai wa mataifa yao! Wakaona watengeneze mfumo utakaoweza kuzinusurisha nchi zao. Na inawezekana wat wa nje walisaidia kwa njia moja au nyingine ili nchi hizi ziungane. Inawekekna walipokea mssada wa hapa na pale. Lakini vile vile inawezekana walifuatilia tu na hawakutoa msaada wowote.Ushahidi wa jamabo hili ni kwamba mfumo/muundo wa muungano wetu niwa kipekee,wa kitanzania na zaidi zaidi ni wa kiafrika.

Kama Muungano wetu umeweza kudumu katika mfumo huu kwa miaka 48, na si gharama kubwa sana ya kuulinda ni dhahili kuwa ubunifu wa wazee wetu hawa, ulikuwa makini sana. Ni jambo la kujivunia kama watanzania. Kuyaona haya hakuwezi kuwa kinyume cha uzalendo.

Lakini kama unvyosema( Pasco), kama kweli kosa la kutoridhiwa kwa Muungano kwa upande wa Zanzibar kisheria( kwa maandishi) lilifanyika, kosa hili linabatilisha muungano hata baada ya miaka 48? Je, Matendo yaliyofuata baada ya hapo, kwa mfano; Mheshimwa Rais Karume kulishwa kiapo/kuapishwa na Mwl. Nyerere kuulinda na kuudumisha muungano akiwa makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukubali kuachia uamiri jeshi mkuu, kupoteza kiti katika umoja wa mataifa, matendo haya hayawezi kufifisha kosa hili na ikachukulia kama ushahidi dhahiri kuwa muungano uridhiwa? Hayati Mzee Karume, (Mungu ampumzishe kwa amani) alikuwa mbumbumbu kiasi hicho, aone amelazimishwa jambo, akae kimiya? Dhana ya kumuona Mzee Karume, hakujua alichokifanya haiwezi ikawa kimejengwa katika msingi wa Uzalendo hata kidogo. Hivi kosa hili linaweza likasahihishwa kwa nija ipi? Kosa hili linabatisha matendo yote yalifanywa huko nyuma? Kosa hili linaresha mipaka ya Tanganyika na Zanzibar?

Dhana ya watu kuamini wamerekani na kutowaamini viongozi na watanzania wenzao; hoja yako inatakiwa kuangalia eneo moja tu, hati alizozionyesha Mzee Mwanakijiji ni hati za kughushi? Zimetoka wapi sio suala la msingi sana. Uhalali wake ndilo suala la kubishaniwa na kwa hiyo, hoja yako ingekuwa kama zipo hati halali ambazo ni tofauti na zile zilizoonyeshwa. Au ushahidi kuwa hati zile ni za kughushi! Jikumbushe sifa ya " kielelezo halali'.

Kwa maisha ya watanzania yalivyo kwa sasa, viongozi wetu wamejima uhalali wa kuaminika. Unakumbuka suala Akaunti ya EPA, Richmond,Kagoda,suala la RADA na mengine mengi ya aina hiyo. Viongozi wetu wamekuwa wa kwanza kubisha nahata kufikia kuwakashifu watoa habari wa kwanza. Lakini baadaye inadhihirika kuwa ni kweli. Hebu fikiria suala la RADA na chenji yake, kama sio waiingereza kushupalia makampuni yao kwenye bunge lao, hiyo chenji ingepatikana kweli. Hata baadhi ya taasisi zetu zimejinyima uhalali na mazingira ya kutoaminika.

Tunayo sababu ya kujijenga upya na kusahihisha tabia zetu ili tuwezekuamniwa tena.
 
Mkuu FJM,
Huu muungano wetu ni very unique, baada ya bunge la Tanganyika ku ratify muungano, nchi inayoitwa Tanganyika seazed to exist so do Zanzibar by then jina la Tanzania lilikuwa bado halijapatikana hiyo mwanzo iliitwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika and Zanzibar.

Japo nchi iliyofutika kwenye ramani ya dunia ni Tanganyika, kiutendaji nchi uliyokufa kwenye medani za kimataifa ni Zanzibar na Tanganyika ilibadili tuu jina kuitwa Tanzania.

Hiyo baada ya muungano katika medani za kimataifa Zanzibar doesn't exist anymore mpaka kesho!.

Kitaifa muungano wetu ni wa nchi mbili lakini kimataifa muungano wetu ni wa nchi moja tuu Tanzania, yaani ni unitary union na sio federetion. Hivyo kwenye UN ilipelekwa barua moja tuu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar as there was no any more Zanzibar!.

Kiukweli Nyerere alikuwa na good faith na muungano huu toka moyoni mwake kuwa ni wa nchi moja ya Tanzania ndio maana no one gave a damm kama Zanzibar ikifanya ratification or not.

Kama zilivyo ndoa, ndoa hufungwa kwa tamko tuu la kauli ya "ndiyo" na hati za ndoa husainiwa baadae!.

Ukishatamka "ndiyo" ndoa ni tayari hata kama baadae mke atagoma kusaini hati ya ndoa!. Ndoa itabaki ni ndoa halali isiyo na uhalali wa kisheria!.

Sio kila ndoa ina uhalali wa kisheria ndio maana na void marriages na voidable marriages!.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa mikataba, kuna void contract na voidable contracts. Mkataba wa muungano umekuwa voidable na sio void, zile sababu za zinazoufanya uwe voidable zinarekebishika na mkataba unaendelea.

Kama ukishafungishwa ndoa hata bila kusaini cheti cha ndoa, ndoa ipo na as long as unatimiza majukumu yako yote ya kindoa, then there is no complain !.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Zanzibar, hata kama hawakuridhia rasmi hati za muungano na wametekeleza majukumu yote ya muungano bila kipingamizi chochote, then it was presumed ndoa yetu iko ok hadi leo hakuna anayelalamika!.

Tukubali tukatae, tuliuendesha muungano kibabe!. Ndio maana tuliyaongeza mambo ya muungano toka yale 11 hadi 26 bila kushauriana na Zanzibar!.

Hapa kiukweli Tanzania ilitumia mfumo dume kufikia baadhi ya maamuzi kwa kuihesabu Zanzibar kama mke!. Ukishaoa kuna maamuzi unaweza kuyachukua kwa kumshauri mkeo na kuna maamuzi unaweza kuyachukua na kumuarifu tuu atake asitake!.

Mfano baada ya ndoa ya Tanganyika na Zanzibar, mume na mke walikula meza moja kwa mmoja kuwa rais mwingine kuwa makamo. Baadae mume akanote mke ana ghubu sana, akaamua kumfukuza mezani yeye atakuwa akilia jikoni na sio mezani tena kwa kumuengua rais wa Zanzibar asiwe makamo tena hivyo kumreduce into nothing bila ya mashauriano yoyote!.

Wakati wa ndoa Karume alimwambia wewe rais, mimi makamo!, kitendo cha kumfanya rais wa Zanzibar ni nothing ndani ya muungano ni ukiukwaji mkubwa sana wa hati za muungano!.

Zanzibar ni kama mke jeuri, kama bado unampenda sana, huna budi kumshikisha adabu!. Ila ukipata uhakika mkeo amepata bwana mwingine anayemtosheleza kukushinda wewe, ataanza visa ili utoe talaka, kama ni ndoa ya Kiislamu, bora umpe talaka yake muachane kwa amani!.

Kwa taarifa tuu huyu mke wetu anayeleta chokochoko, kapata bwana wa Kiarabu anayemtimizia mambo yale ya Kizanzibari ambayo siye wabara siyo jadi yetu!.

Ndio maana kwenye hili la "let them go, mimi na Mwanakijiji letu ni moja!"!.

Pasco, hapo zamani za kale..... listen mate, I expected something more substantive than what you've just posted here. And reading your response naona kama umeungaunga story. Kumbuka tunajadili 'legitimacy' ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar. Kama issues za muungano zilibadilika toka 11 kwenda 20 26, 50, 110 or whatever number au Rais wa Zanzibar alikuja kuwa makamo wa rais wa muungano, au hakuwa hiyo siyo issue hapa, issue ni uhalali wa muungano wenyewe.

Jana ulisema hivi: "international treaties", zilisisitiza, lazima ziwe "ratified"kwenye nchi husika ili zipate uhalali wa kisheria (legitimacy).

Sasa nikuulize tena, kama muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar haukuwa retified na Zanzibar na kwa maana hiyo ni batili, kwanini kwa miaka 48 BLM ambayo imeapa kulinda Mapinduzi matakatifu imekaa kimya bila kusema muungano ni batili?

And this time around please try to come up with whatever paper you can get your hands on. Hizi stories za mara Karume alisema hili, mara Nyerere alikuwa mbabe, au mke jeuri, tumeshiba. Tunataka evidence hata kama utapata toka Kenya au kwa Joseph Kabila, and we will not call you a puppet maana unatafuta ukweli. Ukweli ni ukweli hata kama unasemwa na jirani.
 
By Mihangwa:
Hebu someni hii, kwa hisani ya mtu wa Tanganyika!

ASUBUHI ya Aprili 22, 1964, Rais wa iliyokuwa Tanganyika (sasa Tanzania), Mwalimu Julius Nyerere alitua Zanzibar akiwa na hati maalumu mkononi, iliyoandaliwa kwa Kiingereza; akampatia Rais wa Zanzibar Abeid Amani Karume, naye akaiangalia; kisha kwa ushauri wa wasaidizi wake, akachukua kalamu na kutia sahihi. Mwalimu akafanya vivyo hivyo, kuhitimisha na kuthibitisha kile kilichokusudiwa ndani ya hati hiyo na akarejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo.
Walichotia sahihi viongozi wa nchi hizo mbili, kinaitwa "Hati ya Mkataba wa Muungano" kati ya Tanganyika na Zanzibar iliyozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siku tatu baada ya kutiwa sahihi Mkataba huo, Aprili 25, 1965; mabunge ya nchi hizo mbili, (kwa Zanzibar, Baraza la Mapinduzi) kila moja mahali pake, yalikutana kuridhia Mkataba huo wa kimataifa kwa njia ya Sheria za Bunge, zinazojulikana kama "Sheria za Muungano" (Acts of Union), kufanya makubaliano yaliyofikiwa kuwa na nguvu ya kisheria kwa nchi husika na kwa utekelezaji.
Kwa Tanganyika inajulikana kama Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Namba 22 ya 1964; na kwa Zanzibar ni Sheria ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, iliyotangazwa katika Gazeti la Serikali Namba 243 la Mei 1, 1964.
Aprili 26, 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitangazwa rasmi; umma wa nchi hizi mbili ukazizima kwa furaha yenye hofu na shaka; wengi wakihoji ni lini wapi na kwa vipi Muungano huo uliweza kutungiwa mimba na kuzaliwa ghafla kiasi hicho.
Kulikuwa na usiri mkubwa kati ya Nyerere na Karume tangu kuasisiwa hadi kutiwa sahihi kwa Mkataba wa Muungano huu. Kama kuna watu wengine mbali na wao waliojua, basi watakuwa ni Rashidi Kawawa na Oscar Kambona, kwa Tanganyika na Abdullah Kassim Hanga na Salim Rashid kwa Zanzibar.

Madhumuni na namna Muungano huu ulivyofikiwa bado ni jambo la kukanganya na lenye kuzua maswali mengi kuliko majibu. Wapo wanaodai kwamba Muungano huo ni matokeo ya vita baridi kati ya nchi za Kikomunisti (Uchina na Urusi) za kundi la Mashariki, na nchi za Kibepari za Magharibi (Marekani na Uingereza), katika kuwania maeneo ya himaya (sphere of enfluence) ziweze kuendesha ukoloni mamboleo ukanda huu wa Afrika.

Hapa inaelezwa kwamba, nchi za Kikomunisti, ziliitaka Zanzibar huru kiwe kituo chake zikitumie kama kitovu cha kueneza propaganda na mikakati ya kivita dhidi ya kambi ya Magharibi, kama ilivyokuwa tu Cuba kwa propaganda na mikakati ya kivita kwa ajili ya Urusi dhidi ya Marekani.

Lakini, kwa upande wa pili, inaelezwa kwamba, nchi za Magharibi, zikiwakilishwa na Marekani na Uingereza, zilipendelea kuona Zanzibar ikiungana na Tanganyika ya Nyerere, yenye mrengo wa siasa za Magharibi, lakini isiyofungamana na kambi yoyote katika Vita Baridi, ili Zanzibar isiwe tishio kwa nchi za Magharibi kwa kumezwa ndani ya tumbo kubwa la Tanganyika, isiweze kufurukuta.
Hii inathibitishwa na Nyerere mwenyewe, wakati akihutubia Bunge mwaka 1965, aliposema: "Muungano wetu ulifikiwa kwa shabaha za umoja wa Afrika; haukuhusiana na siasa za Mataifa makubwa! Hakuna sababu nyingine; umoja katika bara letu hauna lazima ya kutengenezwa kutoka Moscow, au kutoka Washington".

Kuna ukweli gani ndani ya maelezo hayo ya Nyerere?. Je, huo ndio uliokuwa mtizamo wake juu ya Muungano wa Afrika?. Kwa nini aligeukia Muungano mdogo huo siku nne tu baada ya juhudi zake za kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki kushindwa hapo Aprili 18, 1964?

Afrika haijasahau ugomvi wa kurushiana kejeli kati ya Rais wa kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah na Nyerere juu ya njia sahihi ya kufikia Muungano wa Afrika, kwenye Mkutano wa Pili wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU), mjini Cairo, Julai 1964.
Wakati Nkrumah alitaka nchi za Kiafrika ziungane mara moja kabla viongozi wake hawajanogewa au kulewa madaraka, wasiweze kuyaachia kwa serikali moja ya Afrika, Nyerere alimkoromea akidai, njia sahihi ni kuanza na miungano ya nchi kwa kanda kwa njia ya shirikisho, kabla ya kufikia Umoja wa Bara zima; akatoa mfano wa juhudi zake za kuona Tanganyika, Kenya, Uganda na Zanzibar zinaunda Shirikisho la Afrika Mashariki. Nyerere aliwahi kutamka mapema pia kwamba, alikuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika hadi Kenya na Uganda zipate uhuru, ili ziweze kushiriki kuunda shirikisho.

Na katika moja ya mikutano ya kuzungumzia shirikisho kati ya nchi hizi huru, Desemba 3, 1963, ambapo Zanzibar ilishiriki kama mtazamaji, iliwekwa wazi kwamba, nchi hiyo ingeweza kujiunga baada ya kupata uhuru uliotarajiwa Desemba 9, 1963.
Katika juhudi zake zote za kuanzishwa Shirikisho la Afrika Mashariki, tangu uhuru wa Tanganyika (1961) na siku nne tu kabla ya Muungano wa Tanzania, Aprili 26, 1964, hakuna mahali Nyerere alipowahi kunukuliwa au kuashiria kutaka au kupendelea Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mbali na Shirikisho la Afrika Mashariki, na hatimaye Muungano wa Afrika.

Kwa mfano, akizunguma na Karume, aliyekwenda kumwona Ikulu Dar es Salaam, Machi 1964 (mwezi mmoja tu kabla ya Muungano), kujadili juu ya namna kukabili vitisho vya Field Marshall John Okello Visiwani kwa Karume, Nyerere alikuwa bado akizungumzia Shirikisho la Afrika Mashariki, na si Muungano wa Zanzibar na Tanganyika; alimwambia Karume: "Tazama (Karume), nimewaeleza Waziri Mkuu (Jomo) Kenyatta na Waziri Mkuu (Milton) Obote, kwamba wao wakiwa tayari kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki, sisi (Tanganyika) tuko tayari".

Kisha akamwambia, "Na sasa nakwambia na wewe (Karume); mtakapokuwa tayari kuunda Shirikisho, sisi tuko tayari".
Naye Karume akajibu haraka, "Kwa nini tusifanye hivyo! Ita waandishi wa habari; sasa hivi; niwaambie, sisi (Zanzibar) tupo tayari kuunda Shirikisho".

Kisha Mwalimu amenukuliwa mahali fulani akisema, "Lakini Machi (1964) tulikuwa tumeendesha mfululizo wa mikutano na nchi nyingine za Afrika Mashariki, na ulikuwako uwezekano wa kuanzisha Shirikisho. Kwa hiyo, Zanzibar na Tanganyika tukangoja; ni dhahiri ingechukua muda" (Soma, Crawford Pratt: The Critical Phase in Tanzania).

Maelezo ya Nyerere yako wazi; kwamba kwa mwezi wote wa Machi, na pengine kwa sehemu kubwa ya Aprili 1964, yeye na Karume hawakuwa na wazo la kuunganisha nchi kwa Muundo wa Muungano wa sasa; fikra zao zilielekezwa kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki kuelekea Muungano wa Afrika.

Je, kitu gani kilichowabadili mawazo ghafla wao au mmoja wao, kuelekeza juhudi zao kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, badala ya Shirikisho la Afrika Mashariki? Je, wiki moja au siku nne ni muda tosha kwa nchi kuweza kubuni na kuingia Muungano wa maana, kama walivyofanya waasisi hawa wa Muungano wa Tanzania? Haraka yote hii ilikuwa ya nini, kama hapakuwa na shinikizo nyuma? Nini kilichosukuma kuundwa kwa Muungano huu? Kwa nini viongozi hawa walitelekeza wazo la shirikisho dakika za mwisho?.
Ili kupata majibu ya maswali haya, na juu ya chimbuko na sababu za Muungano wetu, hatuna budi kuangalia kwa ufupi mazingira ya wakati huo wa kuundwa kwa Muungano.

Kwa kipindi chote, tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964 hadi siku ya Muungano, Serikali ya Karume ilikuwa na wasiwasi mkubwa wa aina mbili: Kwanza ni hofu ya Okello, kichaa na mmoja wa wapiganaji walioongoza Mapinduzi ya Januari 12, 1964, kurejea na kuongoza mapinduzi mengine dhidi ya Karume, baada ya kufukuzwa Visiwani. Hofu hii iliambatana pia na uwezekano wa Sultani kukusanya nguvu dhidi ya Serikali dhaifu ya Karume ili kurejea madarakani.

Pili, ni hofu ya kupinduliwa na wanaharakati wa siasa za mrengo wa kushoto (Wakomunisti) waliokuwa ndani ya Serikali yake, ambao walianza kuona dhahiri udhaifu wa Karume wa kuongoza Serikali iliyoingia madarakani kwa njia ya Mapinduzi.
Hili la pili lilikuwa jambo lililo dhahiri; kwamba, kwa sababu ya upeo mdogo kielimu, Karume hakuwa na njia, ila kuwasikiliza vijana hao waliopata elimu ya Kikomunisti.

Naomba niwataje baadhi yao: Othman Sharrif, Abdulrahman Mohamed Babu, Khamis Abdallah Ameir, Ali Sultan, Kanali Ali Mahfoudh, Salum Rashid, Badawi Qualletein; wengi kati ya hawa wakiwa wanaharakati wa Chama cha "Umma Party" cha Babu, kilichofutwa.
Wengine (kutoka ASP) walikuwa ni Hanga, Abdulaziz Ali Twala, Hassan Nassoro Moyo na wengine. Hofu zote mbili, zilimfanya Karume aombe msaada kutoka kwa Nyerere kuweza kujenga utawala wake usimezwe na vyama vingine vya kimapinduzi, na pengine kupinduliwa.

Kwa sababu hiyo, Nyerere alikubali kupeleka askari 300 kutoka Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), wakaendelea kukaa Visiwani kwa muda mrefu. Hali hii ilimfanya Karume awe tegemezi na mnyenyekevu kwa Nyerere; kwani, kama (Nyerere) angeamua kundoa askari wake 300, ingebadili nguvu ya Karume Visiwani. Hatua hii ndiyo iliyomfanya Karume akubali shinikizo la Nyerere la kuunganisha nchi na asiweze kutumia uhuru wake wa kuhoji wala kukataa shinikizo.

Tuangalie jinsi Wakomunisti hao walivyoshika hatamu za Serikali ya Karume na kuwa tishio. Mara tu baada ya Mapinduzi, Serikali mpya ya Zanzibar ilitambuliwa haraka na nchi za Kikomunisti za China, Urusi, Ujerumani Mashariki, Bulgaria, Albania, Czeshoslovakia na Cuba. Nchi ya Cuba ndiyo iliyotoa mafunzo ya kijeshi kwa baadhi ya Wapiganaji wa Umma Party, walioshiriki Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Muda mfupi tu baada ya hapo, Urusi ilileta meli iliyojaa magari, mizinga, bunduki kubwa kubwa za kupiga ndege, vifaru na silaha nyingine.
Mwishoni mwa Februari 1964, Waziri wa Mambo ya Nje, Abdulrahman Babu, aliitangazia dunia kwamba, Zanzibar ilitarajia kupokea sh. 10,000,000/= kutoka China, akijitapa kwamba, "huo ulikuwa mwanzo tu".
Majina ya Kikoloni Visiwani, yalibadilishwa, badala yake yakawekwa majina ya Kikomunisti: Uwanja wa Mpira wa Taifa uliitwa "Mao-Tse-Tung"; shule moja iliitwa "Fidel Castro"; hospitali ya Taifa ikaitwa "V.I. Lenin"; madaktari wa Kichina wakafurika, askari wa Ki-mashariki nao wakaongezeka Visiwani.

Akipokea vitambulisho vya Balozi wa China, Meng Yi, siku chache baada ya Mapinduzi, Rais Karume alisema: "Zanzibar inaitegemea China si kama rafiki, bali kama ndugu kabisa", tamko ambalo lilizitia hofu nchi za Magharibi.
Tena Februari 1964, Karume, kwa kukasirishwa na Marekani na Uingereza kutokana na kutoitambua Serikali yake, aliwatimua mabalozi wa nchi hizo kwa notisi ya saa 24. Lakini agizo hilo lilifutwa mara moja baada ya Tangazo la kuitambua; Marekani wakampeleka Frank Carlucci, jasusi mkubwa wa Shirika la Kijasusi la Marekani - CIA, kuwa balozi mdogo akitokea Congo yenye misukosuko.

Aprili 1964, Karume aliwaamru Wamarekani kufunga kituo cha ujasusi (satelite station) kilichokuwa Tunguu, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni cha kuzinyima Marekani na Uingereza fursa na uwezo wa kuelewa yanayotendeka ukanda wa Afrika Mashariki, hasa Zanzibar, na kutoa nafasi kwa Urusi na China kutamba.

Kufikia hapo, Marekani ilikosa subira; ikaazimia kuiadhibu Zanzibar ya Kikomunisti kutokana na kutoheshimu sera za kutofungamana na upande wowote, huku Babu akielezewa kuwa ni mtu hatari kwa maslahi ya nchi za Magharibi.
Ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inadhibitiwa isiangukie mikononi mwa nchi za Kikomunisti, hasa kufuatia juhudi za Nyerere za kuundwa Shirikisho la Afrika Mashariki kushindwa, Marekani na Uingereza zilileta manowari za kivita kwenye Bahari ya Hindi, tayari kukabiliana na "chokochoko" za Wakomunisti, na kuhakikisha kuwa Zanzibar inaungana na Tanganyika kwa vyovyote vile.

Tutaona baadaye katika makala haya, jinsi nchi hizo zilivyosimamia kwa njia ya doria za kijeshi na kisiasa, zoezi zima hadi Muungano ulipofikiwa. Tutaona pia jinsi hila na ujanja wa ziada, ulivyotumika kukizidi akili na kete kikundi cha Babu kilichopania kuiondoa Zanzibar kutoka siasa za kutofungamana na upande wowote, kuingia kwenye kambi ya Kikomunisti; na jinsi Nyerere na Karume walivyoingizwa katika njama za nchi za Magharibi.

Aprili 11, 1964, ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya mazungumzo juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki lililoshindwa, ambalo Marekani ilitarajia Zanzibar ingeweza kujiunga na kumezwa ndani ya Shirikisho pana kuepuka makucha ya Ukomunisti.
Aprili 19, 1964, Mwalimu Nyerere alimwita Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanganyika, Roland Brown, akamwambia: "Nataka unifanyie kazi ya siri; wananchi wa Zanzibar wanataka kuungana na Tanganyika". Akamwomba afikirie utaratibu ambao ungeweza kutimiza lengo hilo.

Brown aliandaa rasimu ya Muungano kwa muundo wa "Uhusiano kati ya Uingereza na Ireland"; muungano wenye kuhusisha mambo kumi na moja tu kwa Serikali ya Muungano, na ambapo Serikali za Tanganyika na Zanzibar zingeendelea kusimamia mambo mengine yote yasiyo ya Muungano.

Aprili 21, Nyerere alimwalika Karume Dar es Salaam; naye akaondoka Zanzibar kwa siri. Na aliporeja Zanzibar siku hiyo jioni, alimwagiza Mkuu wa Itifaki, Ali Mwinyigogo, kuandaa mapokezi ya Mwalimu Nyerere kesho yake, Aprili 22, 1964, kwa shughuli iliyoelezwa mwanzoni mwa makala haya. Nini kilitokea Aprili 22, 1964 na baada ya hapo?

Tuhitimishe sehemu hii ya kwanza ya makala kwa muhtasari kwamba: Tumeona juhudi za Mwalimu Nyerere za kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki zilivyoshindwa katika mazungumzo ya mwisho, Aprili 11, 1964, ambapo Zanzibar ingekuwa mwanachama; badala yake akamtaka Karume waungane. Karume mwanzini alisita lakini baadaye alikubali. Ndipo Nyerere akapata nafasi ya kuandaa Mkataba wa Muungano aliotua nao Zanzibar Aprili 22, 1964.

Tumeona pia jinsi hatua ya Zanzibar ya kukumbatia nchi za Kikomunisti, ilivyoziudhi Marekani na Uingereza, zikaungana na Nyerere katika hoja ya kuziunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kudhibiti kasi ya kuenea kwa Ukomunisti kanda ya Afrika Mashariki na Afrika. Tujiulize, je, mchakato wa Muungano huo ulikuwa wa hiari au shinikizo?
Muungano ulikuwa wa hiari kwa maana ulikuwa suluhisho la matishio ya vita baridi.
 
Pasco, waMarekani wanaweza kuwa na access ya mambo yetu ya ndani kuliko hata sisi wenyewe tunvyojijua.

Mabomu ya G -Mboto yalipolipuka, serikali wazo lao la kwanza lilikuwa kufanya uchunguzi wa kina, kwa kushirikiana (kusaidiwa?) na "wenzetu" Wamarekani. Hivu unaweza kuimagine Marekani kushirikiana na Russia kuchunguza ghala za kuhifadhia silaha za Kimarekani?

Kwetu sisi hatujawaficha kitu waMarekani, hata siri zetu za Ulinzi na Usalama wamekaribishwa kuzifahamu, halafu wewe unasema jambo dogo kabisa kama Muungano wa Tanganyika na visiwa vyake?
Zimme, kwani puppets wakuu ni akina nani?. Kwani ulisikia Tanzania ikilaani uvamizi wa Iraq au Libya zaidi ya Membe kulia machozi ya mamba too late?.

Tanzania tuna siri gani za ulinzi zaidi ya jinsi ya kutegeneza gobore?.

Hiyo ratification hufanyika kwa uwazi, Marekani kadanganywa kuwa ilifanyika naye kadanganya huko kwao halafu ripoti yao ya udanganyifu imeletwa hapa na watu ndio wanaiaminia kuliko waliokuwepo kwenye hayo mapinduzi yenyewe na ndio waliosema hakukuwepo any ratification ya aina yoyote!.

Hili la blind faith kwa mgeni na kutomuamini mwenyeji ndiko ninakokuita "puppeteering" humu tunao wengi kuliko unavyodhania na wewe unaweza kuwa uu mmoja wao!.
 
Pasco, hapo kwenye red, kama nimekuelewa vizuri ni kwamba 'puppets' za marekani wako wengi tena wengine ni viongozi wakubwa serikalini. Na pia 'ukimya' wa Tanzania kuhusu uvamizi Iraq na Libya ni kwa sababu ya u-puppet. Sasa kwa maoni yako, nani alitakiwa kutoa kauli ya kulaaani uvamizi kwa nchi hizi mbili kwa niaba ya Tanzania? Kiongozi wa nchi, IGP, katibu wa tafara au nani hasa?

Lakini kubwa, kama hao/huyo aliyoacha kulaani uvamizi wa Iraq & Libya kwa sababu ya u-puppet wake, bado unataka wananchi waendelee kuwaunga mkono kwa kila wanachosema ili kuonesha uzalendo wao (kwa puppet?)? Hapa narejea kauli yako kuhusu suti na uzalendo.

NB: Tunanyemelea saa 11 jioni, tafadhali tupe mwongozo wa hii thread.
 
Back
Top Bottom