Online Puppets: Kumbe Tunao "Puppets" Wengi Kuliko Tunavyojidhania!

Pasco heshima mbele! Kuhusu ratification ! Kila nchi duniani ina utaratibu wake mfano Ni Ireland ambayo maamuzi ya mikataba ya EU Ni lazima yapigiwe kura na wananchi maana ndivyo Katiba Yao inavyoshauri au kulazimu!

Katika international law hakuna sehemu yeyote ijayo lazima nchi moja kufuata utaratibu Fulani Wa ratification unayoizungumzia pasco! Unichukulia definition ya international law na sources zake utagundua Ni practise , customs, regulations etc!

Tukirudi kwa Zanzibar , kumbuka kwamba ilikuwa Ni serikali ya mapinduzi na kwa maana hiyo nafikiri hata katiba ilikuwa suspended na sijui Ni Katiba gani wana
Mapinduzi Kama Karume waliyokuwa wanatumia ! Kwa kuwa wanzibar hawakuwapinga na Kuyapinga mapinduzi hadi wakati huu niandikao, kwa kuwa SMZ imeapa kuyalinda mapinduzi hayo, na kwa kuwa walichokifanya akina Babu na Karume ilikuwa kwa niaba ya watu wote Wa Zanzibar na serikali ile, basi Leo hii hairier kutokea serikali ile ile iliyoapa kuyalinda mapinduzi,watu wale wale walio iweka serikali hiyo madarakani waje waseme tena hadharani kwamba hawautambui muungano!

Tafsiri rahisi Ni kwamba hawaikubali serikali walio iweka madarakani, serikali ile ile iliyo kubali kuungana na tanganyika na serikali ile ile iliyoapa kuyalinda mapinduzi hadi dakika
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hii! Kinachotakiwa Ni kuiondosha kwanza madarakani kwa namna yeyote ile ba kusema hawatambui mambo iliyoyafanya kabla ya kupinga muungano
 
SMZ ikisha ondolewa ndio sasa serikali nyingine itajadili mfumo, kuwepo au muungano Wa namna gani unaotakiwa!

Vinginevyo kinachofanywa UAMSHO na wengine Ni uhaini kwa maana halisi ya neno Hilo na zake !

Zanzibar inataka kuihangaisha tanganyika kwa mambo Yao wenyeewe kama wa ratify au la! Tanganyika walikuwa na katiba Yao iliyowataka kufanya hivyo na Zanzibar walikuwa na namna yao
 
Umesomeka mkuu, ingawa unasema hatudiscuss people, ila puppet mkuu ameshafahamika! hatuwezi kuzunguka mbuyu tumeshamjua sma kakimbia jukwaa, hata kule alipoanzisha post yake kakimbia labda anatafuta reference..........
 
Kama na wewe si mtumwa mbona umeanzisha uzi kwa kuchanganya na lugha ya kitumwa?? Tueleweje?? kwani hakuna maneno ya kiswahili ya kuelezea ulichotaka kutuambia mpaka uchanganye na lugha ya kitumwa???? Hilo linakufanya na wewe kuwa mtumwa pia........... Tubadilike Wabongo, fikra sahihi huja kwa lugha sahihi.
 
Pasco,
Ulikuwa umeanza kunikonga mpaka pale uliposema Kikwete kununuliwa suti ni uwongo. Mbona hilo mimi nimelifahamu siku nyingi kabla hata ya Wikileaks kulitaja? Top management wote pale Kempiski wanalijua hilo na wala si siri.
 
Waisrael wakali sana aisee. Waliuvamia uwanja wa ndege wa Entebbe na wakawaokoa raia wao bila shida yoyote!

LMAO....ukali wa Israel unapimwa kwa raid on Entebbe.....teh teh teh! Kaazi kweli kweli.
 
Whom would you call the one who provides your daily bread (and a little butter to top it up) and shelter you from the cold and miserable street conditions of the US?

Master!

kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Na tutapata siri nyingi tu toka kwa Wamarekani kuhusiana na nchi yetu. Unlike in the past thesedays internet gives us information in the comfort of our own homes
 
Pasco, dunia ilishakuwa kijiji sasa. Mawazo ya wamarekani yanaweza kuwa sahihi kuliko ya mmatumbi mwenzangu...
Mkuu Tuko, tuko pamoja, mawazo ni kitu kimoja na matendo ni kitu kingine!.

Hoja ya msingi hapa ni process ya "ratification" kwa bara ilifanyika, kwa Zanzibar haikufanyika!. Hiyo ratification hufanyika kwa maandishi na sio kwa kauli!.

Nimeleta hoja kuwa hakuna andiko lolote bara wala visiwani linalothibitisha ratification ilifanyika!. Leo tumeletewa andiko la Mmarekani kuwa ratification ilifanyika!.

Waliokuwepo Zanzibar ndio wanaosema hakukufanyika any ratification, waliokuwa wajumbe wa BLM ambao ndio wange ratify hizo articles wao hawakuziratify bali Karume alisema kwa kauli tuu kuwa wajumbe wote wamekubali!. Nikauliza kauli ile ndio ratification?!.

Imekuwa ni mazowea mtu kudharau chake na kuthamini cha mwenzie!. Hao Wamarekani waliopeleka umbeya kwao kuwa BLM waliratify muungano nao ni watu wa kuambiwa tuu, wajumbe wenyewe wa BLM ndio wanaosema hawakuratify lakini kwa vile Mmarekani aliripoti kwao kuwa wameratify, then ndio tuwaaminie wao?!.

Hakuna ubaya kuamini cha mwenzio as long as ndio ukweli halisi!. Mmarekani alidanganywa naye akatuma huo uwongo kule kwao sasa ndie anaaminika kuliko hata wakweli wenyewe wa Zanzibar!.
 
Wanabodi, ....Angalizo: "Great Minds" don't discuss people!, hiyo ni kazi ya "Simple Mind" hii thread, hatu discuss watu, tuna discuss idea ya wenzetu humu kuwa puppets chini ya mental slavery ya kuwaaminia sana Wamarekani!, hivyo nawaombeni sana tusianze kutaja taja majina nani ni puppet na nani sio!. Jadili tuu kama unawaamini Wamarekani kuliko tunavyojiamini wenyewe!

Natanguliza shukrani.

Pasco.
Kwa hiyo wewe Pasco watu wakitofautiana na wewe kwa misingi ya kuwa na facts kuhusu topic ambazo pengine wewe huzijui au umeshindwa kuzitafuta for one reason or the other watu hao wanakuwa PUPPETS, MENTAL SLAVES?!
Sikubaliani na wewe kwa hilo; usiwe mvivu wa kusoma na kuanza kuvurumisha kebehi; kaza buti ARGUE dont SHOUT, wakinzani wako wakiona una facts solid watakubaliana na wewe; usipende wakinzani wako wafe ili wewe ushinde hoja.
 
Mungi. Pasco katoa angalizo tusitajane majina tujadili JF na Puppets!
ritz, Ni kweli Pasco ametoa angalizo juu ya kutotaja mtu bali ijadiliwe mada, lakini kwa yeyote ambaye anajua ulipoanzia huu uzi, direct atakuwa kashapata jibu kuwa hata yeye Pasco kashamtaja mtu tayari. Huu mjadala haujaanzia hapa, kuna sehemu ambapo ulianzia na Pasco kaamua kuuleta huku kivingine ndo maana kuna mchangiaji mmoja hapo juu anaitwa FJM ameandika ''kwa nini tuamini unayosema wewe na sio hayo yaliyosemwa na 'mwana JF' ambaye wewe unampinga? Lakini pia unaweza kuweka wazi uzi unaopinga badala ya ku-assume kila mtu yuko kichwani mwako?''. Ni vyema Pasco akaweka huo uzi ili watu wajue ni kitu gani huyo anayeitwa pupppet amezungumza na kama ni kweli anastahili kuitwa hivyo au kaonewa kuitwa hivyo. kwa mtazamo wangu jamaa siyo puppet bali wametofautiana tu msimamo na Pasco, pia sio lazima lile unaloona wewe ni sahihi mwenzio nae alichukulie hivyo hivyo.
 
nadhani cha msingi ni kuongea kwa evidence. Si sahihi kusmea "niamini mimi kwa sababu mimi ni mtanzania" au "usimuamini yule kwa sababu yeye ni mmarekani". Jamani knowledge has no owner!!! Leteni evidences tujadili uzito wake, hatujali uraia wa mleta hoja.
 
Wanabodi, ...Angalizo: "Great Minds" don't discuss people!, hiyo ni kazi ya "Simple Mind" hii thread, hatu discuss watu, tuna discuss idea ya wenzetu humu kuwa puppets chini ya mental slavery ya kuwaaminia sana Wamarekani!, hivyo nawaombeni sana tusianze kutaja taja majina nani ni puppet na nani sio!. Jadili tuu kama unawaamini Wamarekani kuliko tunavyojiamini wenyewe!

Natanguliza shukrani.

Pasco.
ujumbe huu umeletwa kwenu KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI WAKISHIRIKIANA NA PASCO WA JF a.ka. Expeted compaign manager wa Lowasa.
 
Back
Top Bottom