ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Taifa linaangamia kwa kukosa wenye maarifa. Ongezeko la matatizo katika taifa hili ni kisahilio cha maafa katika siku za usoni.
Wimbi la kuongezeka kwa watoto wa Mitaani limekuwa likichukuliwa kirahisi mno na jamii yetu. Hivi leo kila kona ya mji unaopita huwezi kukosa kukuta watoto wa mtaani ambao wengi wao wanaonyesha kuwa sugu na maisha magumu. Katika kundi hili la watoto hao, wapo pia ambao wanajihusisha na ukahaba, ukora nk. Hivi leo, karibia kila mji hapa nchi (hata kule kwa wenzetu Zenji) lazima utakutana na maeneo ambayo ni kituo cha makahaba (wauza miili), kuna maeneo ambayo huwezi kuuliza kutokana na umaarufu wa kuzalisha "makahaba". Ukiachilia wale ambao waingia katika biadhara hii kwa hiyari, wapo wale ambao maisha yamewalazimisha kuuza miili yao. Wengi wao ni wale ambao walikumbwa na shida za kifamilia nk.
Pengine najiuliza, kama Serikali inaweza kujenga magereza ya kuhifadhia wafungwa na inatumia fedha nyingi sana kuwahudumia waharifu wakiwa huko magerezani, ni kwa nini isiwe na mpango wa kuwa na vituo maalumu vya kuwatunza watoto ambao tuna wahita watoto walio katika mazingira magumu (lakini hatuwasaidii??). Ikiwa jamii inaweza kuchangishana kwa ajili ya mambo ya kifahari kama harusi nk, ikia runaweza kuwachangia waliopatwa maafa nk, kwa nini watanzania tusione ipo haja sasa ya kuweka mkakati wa kumaliza tatizo la watoto hawa wa mitaani kupitia nguvu sa pamoja na sio kama ilivyo sasa kupitia NGOs amabazo nyingi huwa sinafanya kazi kwa malengo ambayo pengine ni ya Kitapeli au ya kibinafsi?..
Sielewi nini maana ya kuwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii ikiwa mengi ya yale inayopaswa kuyasimamia yanashindikana...