Uchaguzi 2020 Ongezeko la watia nia CCM 2020 mfano jimbo la Rorya

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kipindi kinachohusu somo hilo hapo juu kinarushwa muda huu na katika mahojiano yao wametoa mfano wa Jimbo la Rorya kuwa na Watia nia zaidi ya 60.

Mimi nijikite kwenye ongezeko la watia nia katika Jimbo la Rorya. Jimbo la Rorya Mbunge wetu ni Lameck Airo kwa kifupi Lakairo. Nitatoa sababu kadhaa ni kwa nini watia nia wamekuwa wengi.

(1) Mhe. Lakairo ahudhurii vikao vya Bunge. Mara nyingi yupo kwenye shughuli zake au Jimboni kwa sababu zisizoeleweka.

(2) Mhe. Lakairo ana miaka kumi Bungeni hata siku moja hajauliza swali Bungeni au kuchangia mjadala wowote katika vikao vya Bunge.

(3) Uelewa wake kwa mambo mengi ya siasa, uchumi, takwimu n.k ni mdogo na hivyo wanaona hasaidii Jimbo.

(4) Miradi mingi aliyoanzisha Prof. Sarungi haijakamilishwa. Mfano barabara ya lami ya kutoka Mika mpaka mpakani mwa Tanzania na Kenya ambayo ina miaka 20 haijakamilika. Imekamilika kwa asilimia tano tu tofauti na Majimbo mengine.

(5) Kupita kwake kwa awamu hizi mbili kumekuwa na walakini jambo ambalo linafahamika kwa wote.

(6) Elimu yake inatia shaka. Watia nia wanaona kwa sasa ni aibu kuwa ni Mhe. Mbunge wa darasa la saba ingawaje wengine wanafanya vizuri kama Msukuma wa Geita Vijijini.

(7) Anabebwa na viongozi wa Chama. Mfano Mwenyekiti wa Chama Mkoa, Wilaya ni marafiki zake hivyo chochote anachosema viongozi hao hawapingi.

Kwa hitimisho, mimi sijatia nia lakini kwa zama za sasa Mhe. Lakairo HAFAI kuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya. Nitawashangaa wanaopitisha majina ya wagombea ubunge kumrudisha Lakairo.

Jimbo la Rorya lina Maprofesa, Phds, Masters, Bachelors ambao wametia nia hivyo ni vema kupata Mhe. Mbunge mwenye uelewa mpana katika masuala ya siasa, uchumi na takwimu.
 
Back
Top Bottom