Ongezeko la wachina kariakoo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ongezeko la wachina kariakoo...

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mla Mbivu, Dec 9, 2010.

 1. Mla Mbivu

  Mla Mbivu JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wadau miaka miwili kutoka sasa sidhani kama kutakuwa na m-bongo anayefanya biashara kariakoo, sababu nimepita karibuni mitaa miwili nimekuta asilimia 80 ya vibanda vinashikiliwa na wachina, tena wanauza bidhaa reja reja, kazi kwetu watanzania...
   
 2. spartacus

  spartacus JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
   
 3. r

  ryn kets New Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila mtu ana uhuru wakununua vitu anapotaka yeye, sasa kama wabongo wanalalamika waache kununua vitu vyao wataondoka tuu. Tatizo tunatafuta chakulalamikia tu maana tunalamika wakati bei na standard ya vitu tunaikubali. shida sio wachina na bora wao wanatafuta ugali, huku guangzhuo kuna kariakoo ndogo, ni weusi tu sasa uliza wanachofanya...kwa kweli kila mtu anashida ya pesa sasa kama anatafuta ki halali mwache, kabla ya kuwa na utaifa sote ni binadamu
   
 4. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tatizo Wachina wamegundua kwamba viongozi wetu wamelewa na rushwa na ndio wanaruhusu wageni kuingia nchini kiholela na kufanya kazi za wenyeji? halafu tunalalamika ujambazi unazidi, sasa hawa vijana wetu wa Kariakoo wakafanye kazi gani wakati elimu na uwezo wao ni mdogo?
  Huku mbele kwa mbele (nchi zilizoendelea) pamoja na kwamba kuna soko kubwa la ajira lakini hawaruhusu wageni wafanye kazi za wenyeji, wanaruhusu wale high skilled immigrants na sio wamachinga.
  Kama hatukuamka sasa kizazi kijacho kitapata taabu sana.
   
 5. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sheria ipo wazi kabisa
  imeainisha wageni wafanye biashara gani ila kwa biashara za
  kimachinga wageni hawaruhusiwi kufanya kinachoonekana hapo viongozi
  wetu wameshindwa kusimamia sheria na miongozo
   
 6. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni nini? Kwamba ni wachina au? Je wangekuwa wasomali , Wangazija,Wanyarwanda, Wakenya? hiyo ingekuwa sawa?
  Waache wafanye biashara, kama sisi tunashindwa kufanya biashara, au hatuna ubunifu wa kibiashara waache watu wengine waje. Maana wafanyabiashara huendelea kuwepo kama bidhaa/huduma zao zinanunuliwa. Wakishindwa, wataondoka, au wataacha kama sisi. Hebu fikiria, ni kwa kiwango gani tumechangamkia kwenda kuuza hata mitumba nchi za jirani, au zile tulizopigania uhuru wao. We are not aggressive.

  On the other hand, nani anawaruhusu? Kama serikali inawaruhusu basi ni halali na tuache serikali ikusanye kodi hata kidogo, kuliko kutegemea kodi za soda, beer sigara na motor vehicles, kumbuka pia kuwa watz wengi hawalipi kodi labda inakuwa ngumu kwa TRA kuwafuatilia watu weusi (angalia madalali wa nyumba, madereva na makonda wa magari wasivyolipa kodi). Na kama biashara zao sio halali, well.. serikali yako uliyoichagua inatakiwa kuwa imewaona na iwakamate.
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  wachina wamepandisha hata bei ya pango kariakoo!fremu moja imefikia 2m kwa mwezi! pia ktk sekta ya civil engineering,garages ni wachina tuu kila mahali!vijana wetu engineers wanafanya kazi gani siku hizi au kuwa mhandisi wa halmashauri wa wilaya?
   
 8. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Dawa mojawapo ya kuwashinda wafanyabiashara wenzako, ni kutoa huduma nzuri zaidi kuliko wenzako, Watanzania wakiwa serious na biashara hao wachina watakimbia tu. Mbona sasa hivi wahindi na waarabu hawamtishi mtu? Lakini tukikaa tu tunacheza bao na kunywa bia badala ya kufikiria njia za kuboresha huduma katika business zetu wachina watatushinda, pia watakuja hata watu wa mataifa mengine. Hivi umeishawahi kupeleka gari garage za kiswahili? Hawakawii kukuliza, sasa kama mchina au mhindi au mkenya akianzisha garage inatoa huduma nzuri, si lazima atapiga bao tu? Na kama nina garage, ninaajiri mmachinga, anaiba taa za gari la mteja ilhali mchina au mhindi haibi, si nitaendelea kuajiri watu ambao najua si wezi?
   
Loading...