Ongezeko la vituo vya kurudia mitihani

kiraremapojoni

JF-Expert Member
Nov 30, 2018
391
512
Habari wana jamvi? Nimefanya kautafiti fulani juu ya ongezeko la vituo vya kufundishia wanafunzi ambao wanarudi amitihani ya kidato cha nne (CSEE) pamoja na wale wa maarifa (QT). Kitu kikubwa cha kujiuliza ni kitu gani sana ambacho kinasababisha kuongeza kwa hivi vituo. Binafsi nimegundua haya yafuatayo.

1: Matokeo mabaya. Wanafunzi wengi na hasa wa shule wa kutwa wanakuwa wanafeli sana mitihani yao ya shule (School Candidate) na suluhisho lao kwa kufanya vizuri mitihani hiyo ni kurudia, ila swali la kujiuliza ni kwamba kama umeshindwa kwenye ulingo utaweza nje ya ulingo? Ingawa inasemekana lakini sina hakika hata maksi pia zinatofautiana kati ya mtahiniwa wa shule (school Candidate) dhidi ya mtahiniwa wa kujitegemea (Private Candidate)?

2: Hitaji la wazazi: Kijana au binti anapofeli mara nyingi wazazi huwa hawafurahishwi na hii hali na wanaamua kumpa mwanafunzi nafasi ya upendeleo ili aweze kusahihisha matokeo yake ambayo aliyapata kwa mara ya kwanza akiwa kama mtahiniwa wa shule. Swali je mwanafunzi yuko yatari kurusiamtihani akiwa na shauku ya kufuta yale matokeo yasiyoridhishwa akiwa kama mtahiniwa wa shule?

3: Biashar: Pia naamini imeonekana kamani biahsra ambayo haina stress kwani kwa mwaka unajua idadai ya wanafunzi unaopata na taasisi imeingiza kiasi gani na imetumia gharama kiasi gani. Hakuna haja ya kuwa na mkaguzi kwani hesabu zake ni za kuvukia barabara tu na wala hazihitaji welesi wa ukokotozi wa hesabu za biashara.

4: Kijiwe cha wanafunzi: Milijaribu kuongea na baadhi ya wanafunzi na kugundiua kuwa , pia mara nyengine hizi taasisi hutumika kama kijiwe cha wanafunzi kukutana na kubasilishana mawazo bilaya kujali muda na wakati wanaopoteza katika wakati huo.

Kama kuna sababu nyengine naomba tuziainishe hapa ili tujue tunawasaidia vipi vijana wetu katika kuokoa muda na kuwaepusha na vishwawishi ambavyo vinaweza kuwakumba wakiwa katika harakati ya kurudia masomo yao

Niwatakie Pasaka njema Wakristo wote ulimwenguni
 
Omgezeko la wahitimu mtaani hivyo kujipatia ajira kwa kufungua vituo wakishirikiana na baadhi ya walimu wa Shule zilizosajiliwa kwa mfumo wa kawaida.
 
Back
Top Bottom