Ikaria
Member
- Jul 17, 2019
- 93
- 238
Huku dunia ikidhiamisha siku ya hamasishisho dhidi ya kujitia kitanzi leo, takwimu kutoka kwa Idara ya takwimu nchini (KNBS) pamoja na Idara ya polisi zimeonesha kuwa takriban watu 1,576 walijitia kitanzi katika kipindi cha miaka 4 iliyopita.
Shirika la kutetea haki za binadamu KNCHR limetoa rai kwa Serikali kuchukulia kwa uzito suala la afya ya akili, ikisadikiwa ndilo Sababu kubwa ya watu kujitia kitanzi. Aidha KNCHR imeitaka Serikali kuacha kuharamisha suala hili kwani kufanya hivyo kutasaidia wengi kuwa radhi kufunguka na kuomba usaidizi iwapo wanalo tatizo la afya ya akili.
Shirika la afya Duniani WHO linakadiria kuwa watu wapatao 703,000 hufariki kwa kujitia kitanzi kila mwaka. Aidha kitanzi kinashika nafasi ya nne katika orodha ya Sababu zinazopelekea watu kufa, kati ya umri wa miaka 15 hadi 29.
Visa vingi vya kujitia kitanzi Kenya haviripotiwi kutokana na unyanyapaa unaohusishwa na kitendo hicho. Kenya ni miongoni mwa mataifa 20 hapa Barani Afrika ambalo kujitia kitanzi ni kinyume cha Sheria.