Ongezeko la vilabu vya pombe kama miradi makambi ya Jeshi

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,533
8,619
Hivi karibuni baada ya taasisi mbali mbali kutakiwa kubuni miradi ya Kujikimu , kumekua na Ongezeko kubwa Sana na Bar katika maeneo ya Jeshi

Mfano ukianzia Hapo Mwenge hadi Lugalo kuna Bar zinazopokea Raia zaidi ya Sita
Hiyo ni mbali ya Ranks , Officer and Brigade Mesa ambazo ni moja ya stahiki za askari kujiliwaza

Hapo nimeangalia sehemu hiyo kama case Lakini karibu Kila kambi imefungua mradi wa Bar

Hili sio jambo zuri hata kidogo Kwani linashusha Hadhi ya jeshi kama ni Bar basi ziishie zile za Suma Lakini sio makambini

Lakini pia Core activity ya jeshi sio kufanya biashara ndio maana hata miradi inayofanywa na Majeshi ni ile inayoendana na uwezo wao wa Teknelojia au Vifaa ambavyo uraiani hakuna Mfano Viwanda , Ujenzi

Napenda kushauri CDF na watendaji wake watizame ongezeko la hii miradi tunatambua haja ya kuwe na miradi ya kusupplement budget za Vikosi Lakini sio lazima kuwe na miradi isiyoendana na majukumu yao

Naamini SUMA wanaweza kubuni miradi mikubwa kabisa ya kimkakati ituondolee na aibu ya hizi biashara za Bar na ikazalisha pesa za kutosha kugharamia mambo madogo madogo hata makubwa pale budget kuu inapochelewa
 
Acha tunye mkuu wanajeshi sisi walevi sana

Hakuna tatizo kunywa pombe kwenye Mess zao ni haki yao kabisa kwenye majeshi yote duniani ambako kunakua na ration ya Bia au bia za punguzo last bei .

Tatizo liko kwenye kufungua Bar kama biashara za Vikosi, hiyo haijapata kutpkea

Polisi wenyewe waliofanya Hivi kipindi fulani wakaanza kupata matatizo
 
Sasa ndugu yangu hujui uchumi unaendeshwa na viwanda vya bia.....waha tutengeneza tu taifa la walevi maana hadi sasa sisi ni nchi ya tatu duniani kwa kutokua na furaha
 
Back
Top Bottom