Ongezeko la Vifo na fursa ya ajira kwa wauzaji wa Majeneza

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,014
1,498
Habari wakuu...

Dunia na maajabu yake sifa zote anastahili M/mungu (kwa waaminio) hakika katika kila zito kuna wepesi,katika dhiki kuna faraja,kwenye majuto kuna mafunzo, huu ndio mwendo wa dunia kwa kila chenye uhai kilichomo ndani yake, ni kung'ata na kupuzia.

Jambo moja linaweza kuwa zuri kwa yule anaenufaika kwalo na hiloilo linakuwa baya kwa yule linalomharimu. Nimewakumbuka Wachimba makaburi,wachongaji na wauza Majeneza wanaangaliwaje kipindi hiki kwa neema iliyowashukia!?

Niseme (Neema)kwasababu vifo ni fursa kwao, ila kwa wafiwa ni huzuni kubwa!! Naisubiri kwa hamu siku ambayo Wachimba Makaburi na wauza Majeneza wataombwa kutoa maoni kulingana na kazi yao juu ya Vifo vya watu wengi vinavyoendelea kutokea ulimwenguni kote.
 
Kwa mbaali naona kama vile kuna watu wanaowaonea wivu wachongaji na wauzaji wa Majeneza kwa jinsi biashara yao inavyowanufaisha kipindi hiki!?
 
Kiukweli hii biashara inalipa sana, hapa ninapoishi kuna jamaa wanajiita majanga majani wanazidi kutajirika kupitia biashara ya majeneza
 
Kwa mbaali naona kama vile kuna watu wanaowaonea wivu wachongaji na wauzaji wa Majeneza kwa jinsi biashara yao inavyowanufaisha kipindi hiki!?
 
Back
Top Bottom