Ongezeko la VAT kwa miamala ya kifedha, kwanini wabunge wa CCM mlipotosha?

Chillo97

JF-Expert Member
Jun 18, 2016
630
933
Wana bodi..

Baada ya baadhi ya benki kuweka tangazo la ongezeka la kodi VAT katika miamala ya kibeki leo tena nimeona tangazo la voda kupitia huduma yao ya m-pesa nao wakiwatangazia wateja wao ongezeko hili la VAT.

Wakati wabunge wakichangia bajeti kuu ya serikali walijikuta bila kuwa na uelewa wakisema eti ongezeko hili halitawaathiri wananchi bila kuomba ufafanuzi kutoka kwa waziri...wengi wao walisema hiyo VAT itakatwa kwa kiwango cha mwanzoni yaani
kama ulikuwa unatoa pesa kwa ATM au kwa Mpesa kile kiwango ndicho kitakacho katwa kodi hivyo mtoa huduma yaani kampuni ndio ilionekana itaathirika..

Tena wakijiamini walisema ongezeko hili ni kwa makampuni sasa najiuliza kama makato haya yalikuwa kwa viwngo vilevile na ingetozwa kampuni haya matangazo ya kuongezeka kwa VAT yanatoka wapi..??

Nyie wabunge wa CCM mliambiwa ili kato ni kwa makampuni si kwa wateja...??? Kama hamkuambiwa kwa nini hamkuomba ufafanuzi kuliko kupotosha jamii...??

Hata kabla hamjamaliza bunge Zitto alilisema hili lakini kama kawaida yenu mkaponda bila kutoa fact hadi kukamatwa na police... Sasa ni nani aliyekuwa anatetea wanannchi kati yenu na Zitto??

Ongezeko la VAT ambalo moja kwa moja linamuathiri mteja sasa naona mizunguko ya pesa ikipungua katika mabeki hata katika makampuni ya simu... Hii itakuwa athari kubwa kwa uchumi.

Mtu aliyekuwa anafanya miamala hata zaidi ya 10 sasa itapungua
kupunguza gharama za makato..

Nchi inaelekea wapi tukiwa na wanafiki kiasi hiki mnaoumbuka hata mwezi haujaisha..??
 
Kijana Chillo97, hebu acha ngonjela. Tanzania ya viwanda ni mchakato thabiti unaohitaji hatua kama hizi!
acha zako wewe weng wataumia kutokana na ongezeko LA kodi mzunguko was pesa utaathilika sana na wenye pesa uchwala tutazitunza tu ma home ila tambua wengi wanafanya kaz kwa presha na IQ zao ndogo wanataka sifa waonekane mapato yameongezeka kwa taifa kumbe wengi wanaumia mapato hayo c manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi no sawa kuuza viaz vi bichi na kwenda kununua vilivyochemshwa wengi wanakurupuka tutawaon mungu type uhai......
 
Wana bodi..
Baada ya baadhi ya benki kuweka tangazo la ongezeka la kodi
VAT katika miamara ya kibeki leo tena nimeona tangazo la voda
kupitia huduma yao ya m-pesa nao wakiwatangazia wateja wao
ongezeko hili la VAT.
Wakati wabunge wakichangia bajeti kuu ya serikali walijikuta bila
kuwa na uelewa wakisema eti ongezeko hili halitawaathiri
wananchi bila kuomba ufafanuzi kutoka kwa waziri...wengio wao
walisema hiyo VAT itakatwa kwa kiwango cha mwanzoni yaani
kama ulikuwa unatoa pesa kwa ATM au kwa Mpesa kile kiwango
ndicho kitakacho katwa kodi hivyo mtoa huduma yaani kampuni
ndio ilionekana itaathirika.. Tena wakijiamini walisema ongezeko
hili ni kwa makampuni sasa najiuliza kama makato haya yalikuwa
kwa viwngo vilevile na ingetozwa kampuni haya matangazo ya
kuongezeka kwa VAT yanatoka wapi..??
Nyie wabunge wa ccm mliambiwa ili kato ni kwa makampuni si kwa
wateja...??? Kama hamkuambiwa kwa nini hamkuomba ufafanuzi
kuliko kupotosha jamii...??
Hata kabla hamjamaliza bunge ZITTO alilisema hili lakini kama
kawaida yenu mkaponda bila kutoa fact hadi kukamatwa na
police... Sasa ni nani aliyekuwa anatetea wanannchi kati yenu na
zitto??
Ongezeko la VAT ambalo moja kwa moja linamuathiri mteja sasa
naona mizunguko ya pesa ikipungua katika mabeki hata katika
makampuni ya simu... Hii itakuwa athari kubwa kwa uchumi... Mtu
aliyekuwa anafanya miamara hata zaidi ya 10 sasa itapungua
kupunguza gharama za makato..
Nchi inaelekea wapi tukiwa na wanafiki kiasi hiki mnaoumbuka
hata mwezi haujaisha..??

Mod usiunganishe na uzi mwingine
Hebu twambie kabla ya hapo mabank yalikuwa yanachukua asilimia ngapi? Na ilikuwa inakatwa VAT?
 
Muanzisha mada, huu mchezo hauhitaji hasira. Hivi kwa akili yako, mtu anayetoka mbaaali kuja Dodoma akakosa cha kuongea bungeni zaidi ya kuomba mnara ujengwe kukumbuka push up anaweza kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu VAT?

Kikubwa hapa ni kumuomba Mungu. Mihemko na kutojitambua ni shida pale mjengoni ndio maana swali badala ya kujibiwa na waziri, anapatikana mbunge wa CCM kujibu.
 
Eti wanajifanya wanakusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, kumbe ndo wamedhamiria kumkandamiza mtanzania. Hii serikali ni ya kisanii kama ilivyo kwa wabunge wa chama chao.
 
acha zako wewe weng wataumia kutokana na ongezeko LA kodi mzunguko was pesa utaathilika sana na wenye pesa uchwala tutazitunza tu ma home ila tambua wengi wanafanya kaz kwa presha na IQ zao ndogo wanataka sifa waonekane mapato yameongezeka kwa taifa kumbe wengi wanaumia mapato hayo c manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi no sawa kuuza viaz vi bichi na kwenda kununua vilivyochemshwa wengi wanakurupuka tutawaon mungu type uhai......
Huwe na IQ kubwa au ndogo na hata kama ukiwa Chizi Lipa kodi, Tanzania itajengwa kwa kulipa kodi na sio kuzungusha mikono
 
Mchakato wa kuwambia wananchi ili ongezeko haliwahusu huku ndio wanaathirika...au unasema mchakato upi??
Mkuu mimi upeo wangu wa kuelewa unaishia hapo ila ninachokumbuka tuliambiwa viwanda vinakuja nami nasubiri, kwa maana wanasema ukihoji basi unahojiwa so bora kukaa kimya.
Kikubwa hapa ni miluzi mingi ambapo hata mbwa wakubwa inaelekea watapotea safari hii!
 
kwa mbaaali naona uchumi wa Tanzania ukipanda kwa 7.5%kwa mwaka lakini watanzania wakipunguza milo mpaka mlo mmoja kwa cku na uko tunakokwenda kwenye vwanda tuisoma namba kwa sauti maana nw tunaisoma kimya kimya pale ambapo mama zetu na dada zetu watakapo kimbiwa na mabwana au wame zao coz mdingi kashindwa kuendesha family na pale thread za kutafuta wachumba zikiwa adimu hapa JF
 
Ili tuweze kusonga mbele, lazima kodi tulipe.Ss wengi tunakuwa masikini kwa sababu tunaogopa maumivu.Ni vigumu kufikia mafanikio bila kupitia maumivu.Kuna BANK ambazo gharama zao za huduma ziko chini na zingne gharama ziko juu lakini zote zina wateja.Kwa ni hao wateja wakubali kulipa gharama kubwa kungali na mbadala?Kama ulikuwa CRDB na gharma unaiona kubwa, nenda NMB, kutakuwa na unafuu.Vivyo hvyo kwe mitandao ya simu.
 
Hebu twambie kabla ya hapo mabank yalikuwa yanachukua asilimia ngapi? Na ilikuwa inakatwa VAT?
kwahiyo bank hazilipi kodi mwisho wa siku?unataka kunambia mteja wakawaida anakwenda ku purches pale bank!!tukiwaambia hamna maono mnakuwa wakali na wabishi sasa leo ni madouble taxation huyo masikini mnaemtetea ndio huyo kodi kumbe!! raisi wa masikini alikuwa anamaanisha jina lingine la masikini ni kodi
 
Hadi wananchi watakapoamka na kutambua wabunge wanaowapa kura kutoka CCM ni mizoga itakua too late!!!

Serikali inapitisha Sera na sheria nyingi za hovyo zinazoumiza wananchi wao ni ndiooo.... Wabunge wa CCM hawana uelewa kabisa juu ya mambo mengi ktk nchi!!!

Wanatia kinyaa mno!!
 
Tutakoma......wabunge wa Ccm ni janga,hata kodi ya gari imepanda kutoka 150,000/ mpaka 250,000/

Hii imejificha kwa kuwa yanamilikiwa na wachache
 
kwahiyo bank hazilipi kodi mwisho wa siku?unataka kunambia mteja wakawaida anakwenda ku purches pale bank!!tukiwaambia hamna maono mnakuwa wakali na wabishi sasa leo ni madouble taxation huyo masikini mnaemtetea ndio huyo kodi kumbe!! raisi wa masikini alikuwa anamaanisha jina lingine la masikini ni kodi
Usiongee jambo usilo lifahamu! Ukitoa pesa au ukiulizia salio au ukimtumia pesa mtu makampuni yalikuwa yana kukata bila wao kulipa VAT kwenye hizo huduma! Sasa serikali imechukua hatua ya kuweka VAT!

Sasa naomba uniambie kabla ya hapo mabank kwenye huduma walikuwa wanatoza asilimia ngapi na ilikuwa haikatwi kodi maana wameongeza hadi 18 kutokana na kuwekewa VAT kwenye huduma!
 
Inasikitisha na kuleta mkanganyiko katika jamii. Nachelea kusema kwamba nchi hii inahitaji ushauri wakisomi wakizalendo na unoatoa haki kwa wananchi. Hapana wananchi hawatendewi haki na uongozi wa awamu hii.

Ni mshauri gani anaishauri serikali kusitisha utoaji ajira za serikali kwenye nchi masikini kama hii ambayo ajira za serikali ndio moyo wa ajira na uchumi? Mwenzetu huyu alisoma vitabu gani?

Ni msahauri gani anaishauri serikali kubuni aina mbalimbali za kodi zisizowiana na gawio la ongezeko la uzalishaji? Sekta ya huduma binafsi katika nchi masikini ni dhahifu mno na inastahili jitihada za serikali kuikuza! kadhalika sekta binafsi, ni changa mno kwetu. Kwa hali hii kodi stahiki ni kodi zinazotokana na ongezeko la uzalishaji au mwendelezo wa uzalishaji. Sasa leo hii mfanyabiashara mdogo anayelipa wafanyakazi wake kwa m-pesa au anayeweka kiasi chake bank na kukitumia kwa matumizi ya kila siku anabuniwa kodi; kwa uzalishaji gani anaoufanya?

Sasa ajabu wapo wanaotutaka tusilalamikie uwingi wa kodi. Wanasahau kwamba malalamiko yetu ni matokeo ya lundikano la sera zinazoumiza. Sio kodi tu bali kodi hizi zinapoleta madhara katika sekta ya utalii, uwekezaji, microeconomic activities, telecommunications, banking industry, transportation, etc madhara yake ni makubwa kuliko kiasi cha ela kinachokusanywa na serikali kutoka kwenye kodi hizi.

Ni Tanzanian tu, narudia Tanzania tu, ndiko uongozi wa nchi unapimwa kwa ukali wake katika kukusanya kodi. Kadhalika ni wachumi wa Tanzania wa awamu hii ndio wanaodhani nchi inaendelea kwa ukali na utitili wa kodi. Nchi zilizoendelea hazikeshi mezani kubuni aina mbalimbali za kodi, sio kwasababu wananchi wake watiifu katika kulipa bali viongozi wa nchi hizo wanajuwa madhara ya kodi katika uchumi. Kodi kama chumvi kwenye mchuzi, ukiweka sana huwezi kula na ukila kiasi hiko hiko miaka nenda rudi bila kupunguza jiandae kwenda hospitali kwa high blood pressure!

Aisha uongozi huu unakosa washauri wa kiuchuni au washauri wake bado hawana ukomavu katika fani mzima ya economic development na development economics. Uchumi wa taifa tulioujenga miaka kadhaa leo unaangamia at a supersonic speed!
 
Back
Top Bottom