Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Ongezeko la Ukimwi Morogoro na sababu zake
Manispaa ya Morogoro ni moja ya maeneo ambayo yameathiriwa na Ukimwi ambao kichocheo chake kikubwa ni mwingiliano wa kibiashara yakiwamo magari makubwa kama malori ambayo huegeshwa mjini humo likiwamo eneo maarufu la Itigi.
Eneo hili limekuwa maarufu kwa umalaya kwani nyakati za usiku malori mengi huegeshwa katika maeneo hayo na kuwa kishawishi kikubwa kwa baadhi ya watu wakiwamo vijana hasa wasichana ambao wamekuwa wakishiriki biashara ya ngono.
Kinadada kutoka kila kona ya Morogoro hufika Itigi kwa kufanya biashara hiyo ya uchangudoa.
Miongoni mwao wamo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vilivyoko Morogoro ambao hujihusisha na ngono. Vijana hao wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali wamekuwa wakifanya vitendo hivi bila kujali kuwa Ukimwi bado ni tishio.
Baadhi yao wanadai kuwa wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
Dk Getrude Lebby, mratibu wa Ukimwi Wilaya ya Morogoro Mjini anaeleza kuwa kinamama ndiyo wameambukizwa zaidi kuliko wanaume.
Dk Lebby anasema kuwa maambukizi ya Ukimwi wilayani humo yamekuwa yakisababishwa zaidi na:
Kwanza, vigodoro-harusi, ngoma za kunema wari ambazo zimekuwa zikichezwa hasa nyakati za usiku.
Pili, barabara kuu ya Iringa, Dodoma, Dar es Salaam ambayo huwezesha madereva wengi wa malori hasa ya mizigo kuegesha eneo la Msamvu.
Sababu nyingine ni wingi wa taasisi za elimu ya juu kama vile, Kigurunyembe, Mzumbe, Sokoine, Jordan na Chuo Kikuu cha Kiislamu ambazo wanafunzi wake wamekuwa wakishiriki ngono bila tahadhari.
Pia, Morogoro kuwa Kitovu cha biashara zikiwamo za mazao ya kilimo kama mchele kutoka Kilombero, Mahenge na Ifakara, viwanda vya sukari Mtibwa na Kilombero.
Viwanda mbalimbali mjini humo vinavyohitaji nguvukazi . Hivyo ni pamoja na vya tumbaku, nguo na ngozi.
Mtaalamu huyo anaeleza kitakwimu kuwa maambukizi ya VVU yamekuwa yakipanda na kushuka kila mwaka.
Amir Nondo Meya wa Morogoro anasema kuwa hana taarifa yeyote kuhusu mazingira hatarishi kama ya Itigi na Kaumba bali anachokijua kuwa maeneo hayo ni maarufu kwa kumbi za starehe. "Ninachokijua mimi ni kuwa maeneo hayo ni maarufu kwa starehe watu mbalimbali huenda maeneo hayo kwenda kuburudika na si vinginevyo"anasema Nondo.
Hata hivyo, ngono zinazofanyika Itigi ni kama mapenzi ya kuku ambayo hufanyika popote.
Uchunguzi unaonyesha kuwa chumba kimoja kidogo hutumiwa na watu zaidi ya sita kwa wakati mmoja na mmiliki wake kupata Sh1,000 kwa kila mtu anayehudumiwa.
Takwimu za maambukizi ya VVU Morogoro zinaonyesha kuwa jumla ya watu 12,482 waliopima VVU, wanaume 6,371 na wanawake 6,111, kati yao waliopatikana na maambukizi ni 668 wanaume 253 na wanawake ni 415.
Enedy Mwanakatwe, Mratibu na mshauri wa Ukimwi wilaya anasema kuwa ili kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua ni wajibu wa kila mtu kuchukua hatua kwa jamii pia elimu kuhusu Ukimwi itolewe kwa wanafunzi.
"Moja ya mikakati ni kuanzisha Klabu za afya/Ukimwi kwenye vyuo vikuu, vyuo vya kawaida na shule zetu ili tuweze kupunguza maambukizi kwani Ukimwi upo na unaua,"anasema.
Mwanahawa Hamis na Happiness John na ni miongoni mwa kinadada wanaojihusisha na biashara hiyo ya ngono ambao wanasema kuwa hufanya biashara hiyo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili.
"Maisha bwana kila mtu anajua anavyoishi kujikimu kimaisha, wapo wanaoiba mali za watu, majambazi, mafisadi na malaya kama sisi lakini hatufanyi hivyo kwa kupenda ni ugumu wa maisha ndiyo unaosababisha japokuwa wapo wanafanya hivyo kwa tamaa zao kama wanafunzi wa vyuo," alisema Mwanahawa.
Happiness anasema kuwa ukosefu wa ajira nchini ndiyo chanzo cha yote haya kwani kila mwaka wasomi kwa kila, idara wanaongezeka, lakini hakuna ajira.
Hisani ya Mwananchi Publication