Tetesi: Ongezeko la Tsh 40/lita kwenye mafuta na maoni ya wapinzani.

pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,216
2,000
Wakuu

Nakumbuka wakati waziri wa Fedha, Dr Mpango anasoma bajeti, kipengele kilichoshangiliwa sana kuliko vyote ni habari ya kufutwa kwa kodi ya motorvehicle

Wabunge hasa wa CCM walishangilia sana bila kuangalia kwamba hiyo kodi imewekwa kwenye mafuta na kwamba pengine ikawa na madhara makubwa sana.

Walishangilia zaidi baada ya serikali kutamka kuwa inafuta madeni yote yatokanayo na kodi hiyo sumbufu.

Wapinzani wao walipinga wazi wazi, huku wakisema serikali imekosea

Kwa kuwa kodi hii ilikuwa ni kero kwa watu wengi, wakiwemo watu walio wahi kuuza vyombo vyao vya moto pasipo kubadilisha umiliki ,watu ambao vyombo vyao vya moto vimechakaa na havitumiki tena, wote hao walitakiwa kulipa TRA malimbikizo ya kodi hiyo ambayo kwa wengi wao yalionekana kuwa ni mzigo mkubwa, na kuna baadhi mali zao zilishaanza kukamatwa na TRA

Je:Wapinzan kwenye bajeti yao ya kivuli wametoa msimamo gani juu ya hili?

Nataman wawe wameunga mkono kufutwa ,ila wawe wamepinga kuwekwa kwenye mafuta ,na wawe wametoa suluhisho makini zaidi ,la kitaalamu zaidi,ambalo litatoa suluhisho bora zaidi.

Ila kama wameishia tu kulalamika bila kutoa wazo Mbadala lolote then nathubutu kusema haina maana ya kuwa na bajeti kivuli wala kuwa na hao wapinzani labda kama tunataka tuwe na watu ambao katiba inawatambua kuwa ni wapingaji wa kila kitu.

Na kama wamekaa kimnya ,yaani hawajasema chochote juu ya hili ,basi watakuwa ni wapuuzi kwa sababu watakuwa wamepuuzia kero ya wananchi juu ya kodi iliyo kuwa sumbufu, lakin pia watakuwa wamejionesha namna ambavyo wao ni mabingwa wa kulalamika lalamika tu bila kutoa ufumbuzi mbadala wa kero za wananchi,kwa sababu wamepiga kelele sana juu ya kuwekwa kwenye mafuta, hivyo tunategemea waioneshe serikali mahali sahihi pa kuiweka.

Mwenye update ya kile walichosema naomba anijuze tafadhali.
 
UKWELI NI HUU

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
262
500
Gari langu dogo lenye cc1500 natumia lita 5 za mafuta kila siku kwenda na kutoka kazini na visafari vya hapa na pale mjini.

Ina maana kwa siku nalipia sh.40x5 = 200

Kwa siku 30 za mwezi nalipia sh.200 x 30 = 6000 (elfu sita)

Kwa mwaka mzima nalipia sh.200 x 365 = 73,000/= (elfu sabini na tatu)

Hapo awali kodi ya gari langu hili dogo kwa mwaka ilikuwa 150,000/=

Kwa gari langu hili la cc1500 kama itanibidi kutumia mafuta lita 10 kila siku ili kodi hii irudi kwenye 150,000/= kama zamani basi itamaanisha kuongeza mizunguko yangu kwa mara mbili zaidi, kuongeza mara mbili zaidi kama haitakuwa kwa malengo ya kibiashara basi nitakuwa na tatizo mimi binafsi.

Point yangu ni kwamba kodi hii ya sh.40 imemlenga sana mtumiaji wa gari kibiashara. Kodi hii ni imepanda kwa mfanyabiashara na kupungua kwa mtumiaji gari binafsi. Ni mara nyingi pia tumelalamika kuwa wafanyabiashara wanakatwa kodi ndogo ukilinganisha na wafanyakazi, nadhani kwa hapa ni sehemu ambapo mfanyabiashara analipa kodi kuliko mfanyakazi.

Hata hivyo, kodi ya mfanyabiashara inalipwa na mlaji.....
 
pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,216
2,000
Gari langu dogo lenye cc1500 natumia lita 5 za mafuta kila siku kwenda na kutoka kazini na visafari vya hapa na pale mjini.

Ina maana kwa siku nalipia sh.40x5 = 200

Kwa siku 30 za mwezi nalipia sh.200 x 30 = 6000 (elfu sita)

Kwa mwaka mzima nalipia sh.200 x 365 = 73,000/= (elfu sabini na tatu)

Hapo awali kodi ya gari langu hili dogo kwa mwaka ilikuwa 150,000/=

Kwa gari langu hili la cc1500 kama itanibidi kutumia mafuta lita 10 kila siku ili kodi hii irudi kwenye 150,000/= kama zamani basi itamaanisha kuongeza mizunguko yangu kwa mara mbili zaidi, kuongeza mara mbili zaidi kama haitakuwa kwa malengo ya kibiashara basi nitakuwa na tatizo mimi binafsi.

Point yangu ni kwamba kodi hii ya sh.40 imemlenga sana mtumiaji wa gari kibiashara. Ni mara nyingi pia tumelalamika kuwa wafanyabiashara wanakatwa kodi ndogo ukilinganisha na wafanyakazi, nadhani kwa hapa ni sehemu ambapo mfanyabiashara analipa kodi kuliko mfanyakazi.

Hata hivyo, kodi ya mfanyabiashara inalipwa na mlaji.....
Sasa ndo hapo nina hamu ya kujua ,wapinzan wametoa pendekezo gan juu ya kodi hii, pendekezo waliloliwasilisha bungeni

Isije ikawa wameishia kulalamika huku mitandaoni
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom