johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,874
Ongezeko la mshahara ni lazima lianzie au likamilishwe na mchakato wa kibunge. Bajeti ya mishahara ni lazima ipitishwe na bunge baada ya kuangalia mahitaji ya wafanyakazi na mwenendo wa Uchumi.
Mara kadhaa huko nyuma ni wabunge wawili tu ambao walikuwa wakipigania haki za wafanyakazi ambao ni JJ Mnyika wa Chadema na Jaffo wa CCM. Lakini katika bunge la sasa simuoni mbunge yoyote wa CCM akishughulika na Wafanyakazi.
Wabunge wa CCM wengi ni wafanyabiashara na wale hohehahe wachache wanaotegemea mshahara ndio wale wenye uwezo mdogo wa kupambanua mambo.
Mbunge anayeondoka na mshahara na marupurupu ya zaidi ya sh 12 milioni kwa mwezi saa ngapi atamkumbuka mtumishi wa kima cha chini ikiwa madereva wao kila siku wanalia kudhulumiwa mishahara yao.
Mishahara itapanda pale tu watanzania watakapotambua namna ya kuchagua wabunge sahihi na si vinginevyo. Mei mosi siyo siku ya kupandisha mishahara bali Wafanyakazi kusherehekea mafanikio yao na kutiana moyo japo wafanyakazi wa Tanzania hutumia sherehe hizi kuwapongeza wanasiasa mfano leo kila kiongozi wa Tucta ilikuwa ni lazima ampongeze Jenister Mhagama.
Maendeleo hayana vyama!