Ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nickname, Jul 20, 2011.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Nimepata habari za uhakika kutoka kwa Mkuu wangu wa kitengo cha rasilimali watu(Head of Human Resource-HHR) kuwa ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa serikali ni asilimia kumi na moja(11%) kwa kima cha chini na asilimia nane nukta sita(8.6%) kwa wengine wote.

  Kwa hiyo kama mtu alikuwa akipata mshahara wa Tsh 135,000 ataongezewa kwa 11% atapata Tsh 149,850 ikiwa ni ongezeko la Tsh 14,850 na yule aliyekuwa mathalani akipata mshahara wa Tsh 520,000 ataongezewa kwa 8.6% atapata Tsh 564,720 ikiwa ni ongezeko la Tsh 44,720.

  My Take:
  Habari ndiyo hiyo,naona serikali inafanya dhihaka,watu tumesubiri ongezeko la mishahara tukategemea tutapata angalau asilimia 30 lakini wameleta siasa.Kwa ongezeko hili maisha yetu yatazidi kuwa magumu ukizingatia kuwa bei ya mafuta ya dizeli na petroli haishuki ,mafuta ya taa yameongezwa bei na umeme ndio huo wa mgao uuwwiiiiiiii!!!!
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Asilimia hizo huwa ni general annual increment na siyo nyongeza, kwa hiyo mwaka huu mshahara haujaongezwa.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Factor in Inflation then jazia na mafuta ya taa = maisha bora kwa kila mtanzania.

  Hii budget ilipitaje? au ndio maana serikali kupitia Waziri mkuu ilisimamia 'posho' kwa wabunge? Wabunge wanapata 70,000 kila kikao achohudhuria!

  Ongezeko la Tsh 14,850 kwa mfanyakazi wa maisha ya 'mafuta ya taa - Increadible!
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kama haya ni ya kweli, mfanyakazi wa kima cha chini (ambaye possibly ana familia inayomtegemea) atapata arround tsh. 5,000/- kwa siku wakati mwanafunzi wa elimu ya juu (ambaye possibly mzazi wake ni wa category ya kima cha chini cha mshahara na bado anawategemea wazazi/walezi wake) atapata 7,500/- kwa siku!

  kwa kweli tanzania nchi ya ajabu sana!
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Hicho ndicho mnacho zalisha Mkuu, maana nyie watumishi wa Serikali ni sehemu ya ku-fail kwa Serikali mbona mnajisahau sana, nyie ndio source ya matatizo yote yaliopo hapa Tanzania;

  • Nyie ndio kila kona mnatuomba rushwa katika ofisi za Umma.
  • Nyie ndio Waganga mliopo Mahospitalini ambao unatuibia dawa wagonjwa.
  • Nyie ndio TAKUKURU ambao Rushwa imewashinda kushugulikia
  • Nyie ndio waalimu na wakurugenzi mnaotumiwa kusaidia wizi za Kura nyakati za uchaguzi.
  • Nyie ndio Polisi mnao uwa raia kila kukicha!
  • Nyie wezi wa TRA
  • etc etc etc...........................
  Myt:Nadhani mlipaswa kupunguziwa mishahara si kuongezewa kabisa.

  Tunahitaji maboresho ya maisha kwa wakulima na wafanyabiasha ndogondogo ndio sehemu ya kupunguza Umaskini wa Mtanzania.
   
 6. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Njia bora ya kudai haki ya wafanyakazi ni maandamano na migomo mpaka serikali ikubali,ukiongezea na matatizo ya kukosekana umeme mafuta bei juu n.k maandamano na migomo ni kama msumari wa moto kwa serikali LAZIMA isikie kilio cha wafanyakazi kwani naamini serikali yetu ni sikivu.
   
 7. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa sisi wenye nyumba ndogo nyingi we are finished!
   
 8. S

  Shauri JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  walimu wa shule za msingi je ,serikali haiwaoni jamani?mishahara ya kulenga kwa manati,mazingira magumu ya kufundishia, hakuna nyumba za walimu,
  yani ni usanii tu.:typing:
   
 9. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Generalization ni kitu kibaya sana.
  Wanaokula rushwa si hawa maskini wanaopokea 150,000 ni wazee ambao kwa sasa wapo dodoma.
  Hawa unaowaona ofisini, njaa kali ndio inayopelekea kuyafanya hayo.
  Jaribu kujiweka wewe kwenye mazingara hayo kabla ya kutoa huu upupu.
   
 10. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kasomee uchumi kabla hujaanza kuandika usiyoyajua!au hujui wafanyakazi ,wakulima na wafanyabiashara wanategemeana?mfano meneja wa benki atahitaji kununua ndizi,nguo,chumvi,nyanya kwa wajasiriamali.Kuhusu rushwa anayetoa na anayepokea rushwa wote hawafai,sababu kama unajua sheria ya nini utoe rushwa?unatakiwa umchukulie hatua mwizi kama huyo na siyo kumchekea.Suala la wafanyakazi kuiba kura nalo litazame kwa pande mbili kwa sababu mwaka jana mpaka maaskari walipiga kura CDM kwa sababu wamechoshwa na serikali dhalimu!kilichotokea ni wizi wa mchana uliofanywa na akina Lewis Makame,Kiravu na wenzao wachache!si unajua kila sehemu wajinga lazima wawepo haya ndiyo yaliyotuangusha na si wafanyakazi wote!Mimi ni mfanyakazi wa serikali lakini naichukia serikali mbovu siku zote!rushwa,kupiga mabomu waandamanaji,kusema uongo kama kina Ngeleja,kukingia kifua wanaofilisi taifa letu,kuwaita wanafiki wanaotaka posho zifutwe kama Sitta(mnafiki mkubwa-na jumba lake la mmbunge kule Urambo,kuendelea kulipiwa mil 12 kwa mwezi eti kisa ni spika mstaafu!angekua na huruma angeelekeza hizo pesa angalau kununua vitanda maohospitalini,vitabu,pamoja na kuajiri walimu shule za kata huko kwake!badala yake domo la hili zee linatafuna tu pesa za wananchi! ),Bi Kiroboto kuzima hoja za kweli za upinzani,rais kujifanya Vasco da Gama wakati matatizo lukuki kayaacha nchini mwake!haya ni baadhi tu ya mambo yanayonichukiza sana!
   
 11. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa mkuu!Nadhani muda wa kukaa kimya na kunung'unikia pembeni unapaswa kukoma sasa.Rai yangu kwa wafanyakazi wote nchini tuamke sasa na tudai maslahi bora kwa vitendo...TUANZISHE MGOMO NCHI NZIMA USIO NA KIKOMO MPAKA WATAKAPOTUELEWA,vinginevyo tutaendelea kuumia!
   
 12. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Huu ni wakati wa kuitaka TUCTA kwamba ongezeko hilo la 11% ndio zao la mazungumzo yao na serikali au la!Huu ni upuuzi,tena matusi makubwa kwa mfanyakazi wa nchi hii.
   
 13. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Tafuta mfanyabiashara mama.
   
 14. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Rushwa ni rushwa tu iwe kubwa au ndogo, mtu aliyekulia katika mazingira na hali kama hiyo ndio baadae wanapanda vyeo wanakuwa wakurugenzi na PS wanakuwa kama Jairo, samaki mkunje angali mbichi.
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Weka CV yako ya Uchumi hapa tuichambue; By the way huo uchumi wako mbona hatuuoni kila kukicha uchumi wa Taifa unadorora, Nyie mliorundika vyeti bila kuelimika ndio chanzo cha kushindwa kwa uchumi wa Taifa hili! Mmejaa maofini na vyeti lukuki lakini vichwani hamna kitu eti wachumi mbona hatuoni kitu mmebaki kupiga kelele kama kasuku na kukalili aya za vitabu huku taifa linaangamia, mi naona kama hakuna aliyesomea Uchumi Tanzania, maana Kikwete alisoma uchumi UDSM anafanya nini na hiyo Degree si kama wewe tu!
   
 16. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe binafsi unaweza kuishi kwa 150,000 hapa mjini ukiwa na familia?
  Nakushauri uangalie chanzo na sio tatizo lenyewe.
   
 17. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hayo ni mawazo mgando mkuu, wape wafanyakazi wako mshahara wa kumtosheleza then tafuta wala rushwa kwa dhati. huwezi kumkamata mtu unaemuita mfanyakazi wa serikali kwa rushwa wakati unajua fika hawezi kusurvive kwa mshahara wake meaning ili aishi lazima ale rushwa, you will remain beating around the bush. Tuache nadharia za kishabiki bali tusimamie haki ambayo ndo msingi wa binadamu
   
 18. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Arafat acha hasira mkuu; Ingawaje hii unayosema ni kweli siyo wote wenye tabia ulizotaja mkuu ila ninachojua Serikalini watu wengi ni wale wanaowasindikiza wenzao kuwa na maisha bora na wao watabaki tu kusikilizia vijiko na umma vikigongana wakati wenzao wakishiba.
  Wasipoamua kufanya changes watabakia kusubiri mishahara iongezwe kila mwaka huku miaka ikisonga mbele bila kuona malengo yao yakitimia. nawaonea huruma ila Mungu atawapigania.
   
 19. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Miss Judith, ndo unagundua leo. Unajua miaka ya around 2006, niliwahi kwenda nchi fulani huko ulaya, nilikuwa na waethiopia kadhaa. Jamaa walipofika huko hawakurudi. Nikawashangaa sana. Sasa hivi nafikiria kwamba nikipata nafasi ya kwenda huko, naweza pia nisirudi. Tanzania hivi sasa inaboa kupita maelezo. Yaani mgao wa umeme tu unatosha kuyafanya maisha yawe magumu, inflation ipo around 11% na bado kamshahara ndo haka. Tanzania isishangae kupoteza wataalamu wake walio wengi.
   
 20. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mihasira yote juu ya mgao wa giza tunaopewa na juu ya usanii unaoendelea huko dodoma, umenifanya nicheke, kitu ambacho siyo kawaida ktk jukwaa hili!! Asante mkuu! (ila mlioguswa msinipige mawe!)
   
Loading...