Ongezeko la mishahara kwa 100% secta binafsi nini athari zake kiuchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ongezeko la mishahara kwa 100% secta binafsi nini athari zake kiuchumi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ndachuwa, Apr 21, 2010.

 1. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto Send to a friend Tuesday, 20 April 2010 22:30 0diggsdigg

  Patricia Kimelemeta na Voina Maganda
  [​IMG] Kapuya

  SERIKALI, ambayo inahaha kujaribu kuzuia mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kufanyika kuanzia Mei 5, imetangaza nyongeza ya asilimia 100 ya mishahara ya kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na kuahidi kutangaza mishahara ya watumishi wa umma kabla ya Mei mosi mwaka huu.
  Lakini Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limesema hatua hiyo haitabadili msimamo wake kwa sababu inahisi ni ya kisiasa hivyo hawatatangaza kusitisha mgomo wao hadi madai yao yote yatekapotekelezwa.
  Madai yaliyoifanya Tucta itangaze mgomo huo ni pamoja na nyongeza ya kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma hadi kufikia Sh315,000, kupanua wigo wa kodi ili kumpunguzia mfanyakazi mzigo wa kulipa kodi na makato kwa ajili ya mifuko ya hifadhi za jamii.
  Lakini jana, serikali iliamua kuweka kwanza kiporo madai hayo ya Tucta na kutangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa sekta binafsi.
  Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa ongezeko hilo la mishahara ya wafanyakazi wa sekta binafsi, liwanagusa wafanyakazi wote katika sekta hiyo.
  Kwa tamko hilo la serikali lililotolewa kwa mamlaka aliyonayo waziri mwenye dhamana kifungu namba 41 (1) cha sheria ya ajira namba 7 ya mwaka 2004, mishahara ya watumishi wote wa sekta binafsi iliyotangazwa Oktoba 8 mwaka 2007 na aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana John Chiligati, sasa italipwa mara mbili.
  Chiligati alitangaza viwango hivyo vya mishahara ambavyo vilianza kutumika Novemba mwaka 2007 baada ya mvutano mkali kati yake na Tucta.
  Viwango vya zamani vya kima cha chini kisekta pamoja na viwango vipya sasa vimetangazwa vitumike ni kutoka Sh65,000 hadi Sh130,000) kwa sekta ya kilimo, meli za mizigo na za abiria (Sh225,000 hadi Sh450,000), meli za uvuvi za ndani (Sh196,000 hadi Sh392000), makuli na wajenzi wa meli (Sh300,000 hadi Sh600,000).
  Wafanyakazi wa majumbani wapo katika makundi matatu; wanaofanya kazi kwa mabalozi (Sh90,000 hadi Sh180,000),wanaowafanyia maofisa wanaolipiwa huduma hiyo na waajiri wao (Sh 80,000 hadi Sh160,000) na wengine (Sh65,000 hadi 130,000).
  Wanaofanya kazi mahotelini (Sh150,000 hadi Sh300,000), hoteli za kitalii na hoteli za kati (Sh100,000 (200,000) na hoteli ndogondogo, baa, nyumba za wageni na migahawa (Sh80,000 hadi Sh160,000).
  Katika sekta ya madini, upande wa migodi mikubwa, wafanyakazi wanalipwa Sh350,000 na hivyo watatakiwa kulipwa Sh700,000, lakini waajiri wanaoshughulika na machimbo ya chumvi au chokaa waliwekwa kwenye kundi la viwanda vidogo kwa kuwa uwezo wao ni mdogo.
  Viwanda vidogo itakuwa kutoka Sh80,000 hadi 160,000, ulinzi binafsi, kampuni za kigeni (Sh105,000 hadi Sh210,000) na kampuni nyingine (S 80,000 hadi Sh160,000), sekta ya biashara na viwanda inayojumuisha mabenki, kima cha chini kilikuwa Sh150,000 na sasa kitatakiwa kiwe Sh300,000.
  Sekta ya afya imegawanywa katika makundi mawili yanayohusisha hospitali kubwa na maduka ambayo mshahara wake wa kima cha chini ni Sh120,000 na sasa itakuwa Sh240,000) na hospitali ndogo na zahanati (Sh80,000 hadi Sh160,000).
  Wafanyakazi wa huduma za anga mshahara wa kima cha chini ulikuwa Sh350,000 na sasa utakuwa Sh700,000, wasafirishaji wa mizigo (clearing and forwarding) ilikuwa Sh230,000 na sasa itakuwa Sh460,000), mawasiliano ya simu Sh 300,000 (600,000), usafiri wa nchi kavu (makondakta na madereva) sh 200,000 (400,000).
  Wafanyakazi katika vyombo vya habari wamegawanywa katika makundi mawili. Katika kundi linalohusisha vyombo vinavyojiendesha kibiashara, mshahara wa kima cha chini utabadilika kutoka Sh 250,000 hadi Sh500,000.
  Vyombo vingine ni vile visivyojiendesha kibishara kama vile vinavyorusha matangazo ya kidini, ambavyo kima cha chini kilikuwa ni Sh150,000 na sasa kitakuwa Sh300,000.
  Wakati serikali ikitangaza viwango hivyo vya kima chini cha mshahara mwaka 2007, iliweka wazi kwamba mwajiri haruhusiwi kulipa chini ya kiwango lakini anaweza kukiongeza kwa kadri anavyopenda ili kuboresha hali za wafanyakazi wao.
  Hata hivyo, viwango hivyo vilizua mtafaruku kwa waajiri wengi wakidai wakivitekeleza watafilisika kutokana na biashara kuwa ngumu na hasa ikizingatiwa wakati huo gharama za mafuta zilipaa na kukawa na wasiwasi pia ya dunia kukumbwa na uhaba wa chakula.
  Kwa kujua yaliyotokea kwenye sekta binafsi baada ya kutangaza viwango vipya mwaka 2007, Profesa Kapuya aliwataka waajiri wajitahidi kuvitekeleza kama vilivyotangazwa na serikali ili kuepusha migogoro sehemu za kazi.
  Aliigeukia Tucta akisema ilitoa mapendekezo saba ya kuitaka serikali kuyatekeleza kwa ajili ya kuondoa mgogoro huo na yoye yametekelezwa.
  Alisema tayari serikali imeridhia mapendekezo hayo na kilichobaki ni kuendelea na taratibu za mazungumzo hayo ili kuendeleza mchakato huo ikiwa ni pamoja na kutangaza siku ya kuanza kutumika kwa viwango vipya vya mishahara.
  Kapuya alisema serikali pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi walikaa kwenye kikao cha utatu kilichoitishwa na Baraza la Upatanishi (Lesco), ili kujadili hoja hizo saba.
  Kuhusu wafanyakazi wa serikali, alisema wataongezewa mishahara hiyo baada ya kutolewa notisi kwenye gazeti la serikali hivi karibuni ili waweze kutangaza ongezeko hilo kabla ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo hufanyika Mei Mosi.
  “Tumemaliza tofauti zetu, hivi sasa tuko kwenye mchakato wa mwisho wa kumaliza mgogoro huu. Kutokana na hali hiyo wafanyakazi wa sekta binafsi watalipwa ongezeko la asilimia mia moja, wakati serikali itatangaza rasmi kuongezwa kwa mishahara hiyo kabla ya sherehe za Mei mosi. Hivyo basi tunaamini kuwa wafanyakazi wataendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Profesa Kapuya.
  Kutokana na hali hiyo, alisema Aprili 27, mwaka huu watafanya kikao ambacho kitatoa majumuisho ya suala zima la mgogoro huo pamoja na hatua zilizofikiwa juu ya maamuzi yaliyobaki.
  Profesa Kapuya alisema ikiwa wafanyakazi wataaamua kuendelea na mgomo wakati muafaka wa matatizo yao umepatikana, utakuwa ni kukiuka sheria kwa sababu watakuwa wamevunja makubaliano waliyofikia kwa pamoja.
  Lakini hali haikuwa hivyo kwa upande wa Tucta. Naibu Katibu Mkuu Nicholaus Mgaya aliitisha mkutano na waandishi wa habari jana na kuwaeleza kuwa mgomo upo pale pale kama ulivyopangwa.
  Hata hivyo, Mgaya alisema makubalino yao na serikali ni kurudi kwenye meza ya majadiliano na sio kuzima mgomo.
  Mgaya alisema kutokana na hali hiyo wafanyakazi wataendelea kushikilia msimamo wa kugoma ikiwa serikali itashindwa kuyafanyia kazi malalamiko yao kabla ya sherehe za Mei mosi.
  “Tunachokitaka sisi ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanaongezwa mishahara yao,” alisema Mgaya.
  Aliongeza kutokana na hali hiyo wameitaka serikali iache siasa badala yake itatue matatizo hayo kwa kutumia busara na utalaamu.
  Alisema makubaliano hayo ni kurudi kwenye meza ya majadiliano wakati serikali inaendelea kurekebisha mishahara ya wafanyakazi.

  HEMBU TUJADILI KAMA VILE WEWE NI MWAJIRI MATHALANI UNA INTERNET CAFE NA UMEAJIRI WADADA 3 KWA MSHAHARA WA SH 70,000 KWA MWEZI SASA UTALAZIMIKA KUMLIPA KILA MMOJA SH 140,000
   
 2. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Bwana Vincent! Heshima....

  Hapa hamna cha kujadili, kwa sababu hizi ni bla bla za kisiasa tu. Professor Juma Kapuya kesha wekwa mfukoni na mafisadi wa siasa, sasa amepofuka anaropoka ovyo tu. Mpaka mtu unajiuliza kama amesoma kweli au naye ndo hao wanunuzi wa degree. Haingii akilini serikari kutangaza vima hivyo badala ya chama cha waajiri ambao ndio wana uwezo wa kudhibiti hao wenzao watakao kiuka. Hivi unadhani mwajiri gani atakubali kuongeza cost zake za mishahara ( ambazo ni DIRECT labour obviously) by 100% bila kuathiri bisahara zake? Hii ni upuuzi mtupu, na TUCTA wakikubali hili ni bora wafutwe kama Jumuiya maana watakuwa nao ni wasanii tu.
  Multip[lier effect ya hii kitu ni kubwa: Business may lose profit margin, hiyo nayo ita leta redunduncies, halafu un employement and then, political unrest.
  Nadhani serikari imefika mahali wamekuwa vipofu kama yule mfalme wa Babeli aliyekufuru kwa kulewa madaraka.
  Slowly but surely, I begin to like Mkapa over Kikwete!
   
Loading...