Ongezeko la mifugo kutoka nje ya nchi ni chanzo cha mapigano ya wakulima na wafugaji?


jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
26,920
Likes
17,663
Points
280
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
26,920 17,663 280
Rais wa JMT amesimama wima dhidi ya mifugo iliyovuka mpaka!

Kwa miaka nenda rudi Tanzania imeshuhudia mapugano na mabushano makali sana kati ya wakulima na wafugaji wanaoingiza mifugo mashambani.

Mauaji na mapigano mengi sana yametokea nchini na sababu ya msigano huu ni kitendawili.

Waziri mkuu mstaafu ambaye sasa ni mwanachadema ndugu Sumaye atakumbukwa kwa kushindwa kuzuia mauaji makubwa ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Kilosa.

Sekta ya mazingira nchini ina kumbukumbu kubwa sana za uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanywa na mifugo katika bonde la mto Ruaha mkuu.

Uhamishaji wa mifugo na wafugaji kutoka katika maeneo mbalimbali nchini ili kukabili uharibifu wa mazingira na mapigano kati ya jamii sio jambo geni nchini.

Vyimbo vya habari vimewasilisha matukio mengi sana kuhusuana na majanga ya mifugo na ufugaji hasa hasa mifugo ya ng'ombe

Yapo mambo mengi ambayo ninaweza kuyaelezea na kujaza kurasa nyingi kuhusiana na masakata ya ya ufugaji na mifugo nchini Tanzania.

Hoja yangu ni kwamba.. hadi leo hatujajua kiini cha tatizo la mifugo mingi kutapakaa nchini bila moangilio na inayoleta taharuki kila uchao.

Je ni kweli Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo kuliko ardhi ya malisho?
Au

Je Tanzania ina idadi ya kawaida kabisa ya mifugo kulinganisha na ardhi ya malisho lakini tatizo ni usimamizi?

Au

Je Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo ya kigeni inayoletwa kusaka malisho na hivyo kuzidisha migogoro katika jamii yetu?
 

Forum statistics

Threads 1,236,491
Members 475,174
Posts 29,259,708