Ongezeko la mauaji/Ubakaji na udhaifu wa vyombo vya uchunguzi, nini kifanyike?

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,540
9,472
Tunashuhudia ongezeko la mauaji kila kukicha sehemu mbali mbali za nchi yetu, huku Police na vyombo vya uchunguzi vikijaribu kupambana kwa kuwakamata wahusika na kuwafiksha mahakamani wale wanaobainika, ili sheria ichukue mkondo wake..
Bahati mbaya juhudi zinazofanywa na vyombo vyetu vya usalama, zinakwamishwa na ukosefu wa vifaa vya kuchunguzia, pamoja na weledi mdogo wanaofanya chunguzi hizi.. Kwa ajili ya kusaidia mawazo katika kupambana na tatizo hili kubwa, ninapenda kutoa mawazo yangu, kama mchango wangu kwenye kadhia hii inayopoteza maisha ya watanzania wasio na hatia..

1. Forensic Science ni sayansi yoyote ambayo inatumiwa kwa ajili ya sheria, na kwa hiyo huwa inatoka ushahidi wa kisayansi mahakamani, kwenye uchunguzi wa jinai (pamoja na mauaji).. Forensic Science inabeba uchunguzi unaoanzia eneo la tukio, kuanzia na kulifunga eneo la tukio, (ili kuzuia ushahidi wowote ambao uko eneo la tukio kuingiliwa au bahati mbaya au kwa makusudi).. Hapa mara baada ya kutokea tukio na kufungwa wanakuja wataalamu wa forensic na watachukua finger prints hapo, watachukua damu kama ipo kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha DNA, watachukua na sample za sperms kama tukio ni kubakwa, wataangalia shoe prints, wataangalia risasi (kama ilitumika) ili kugundua aina ya bunduki iliyotumika, wataangalia position ya victim ili kujaribu kugundua alikuwa katika state gani, kama alikuwa anamjua mtenda wa tukio au la..

Haya ndo yanaweza kutengeneza kesi iliokamilika dhidi ya mtuhumiwa kama akija kupatikana na kufikishwa mahakamani.. hata akikataa na hakuna shahidi alieona tukio lakini forensic science inathibitisha pasipo shaka tukio kutendwa na huyo mtuhumiwa.

Najua mtasema haya mambo yanapatikana Ulaya na Marekani, lakini tusisahau Tanzania tuna mashine ya DNA na mashine za fingerprints (ambazo wapiga dili wamechangamkia) kwa hiyo tunaweza kabisa..

2. Facial sketch experts ambao wana uwezo kupitia macho ya mashahidi waliobahatika kuwaona watuhumiwa, kuchora na kuweza kupata sura za watuhumiwa na hivyo kurahisisha kazi ya kuwatambua watuhumiwa hao toka kwa wananchi pindi picha zitakapotolewa public..

3. Watendaji wenye weledi katika kazi za kiuchunguzi, ambao miongoni mwao wanatakiwa watendaji wenye ufahamu kuanzia kwenye crime scene, wataalam kwenye fingerprints na DNA, wataalam wa kuhoji watuhumiwa na ambao wana uwezo wa kutengeneza profile za mtuhumiwa kwa kuangalia aina ya uhalifu uliotendeka..

4. Serikali kufunga camera za cctv maeneo mengi ya jiji, na vile vile kuwahamasisha wananchi kufunga cctv camera kwenye maduka na supermarkets huku wakihakikisha hizo cctv camera zielekezwe mpaka nje ya duka na kwenye parking za magari.. Hii itasaidia pale nyendo za washukiwa wakiwa wanafuatiliwa kwa ajili ya kupata ushahidi zaidi..

Haya yote niliyoyaandika hapa yanawezekana kufanyika ndani ya nchi yetu, kama serikali ikiamua kuwekeza kwenye kitengo cha uchunguzi wa makosa ya kijinai.. Mtindo wa kuwakamata watuhumiwa na kuwatesa imepitwa na wakati.. Mahakamani wanataka concrete evidence na sio statement toka police kwamba mtuhumiwa alikiri kufanya tukio..

Mwenye la ziada anaweza kuongezea hapa, kwa manufaa ya Taifa letu..

Naomba kuwasilisha..
 
Tatizo udhaifu wa usimamizi wa jeshi letu la polisi hasa idara ya upelelezi. Kama mtu mwenye tatizo ndio polisi wanakugeuza ndio mpelelezi wao huku wakikuchomoa hela za kuwalipa "informer" hapo una wapelelezi au wapiga ramli?

Kesi nyingi sana zimelundikana polisi hazipelelezwi, mtu akiuwawa kama ndugu hawatafuatilia faili linafungwa bila hata upelelezi kukamilika. Kuna mauaji ya miaka ya tisini hayajapelelezwa mafaili yanakula vumbi ma CID wanashinda Bar wanakunywa bia tu
 
Tatizo udhaifu wa usimamizi wa jeshi letu la polisi hasa idara ya upelelezi. Kama mtu mwenye tatizo ndio polisi wanakugeuza ndio mpelelezi wao huku wakikuchomoa hela za kuwalipa "informer" hapo una wapelelezi au wapiga ramli?

Kesi nyingi sana zimelundikana polisi hazipelelezwi, mtu akiuwawa kama ndugu hawatafuatilia faili linafungwa bila hata upelelezi kukamilika. Kuna mauaji ya miaka ya tisini hayajapelelezwa mafaili yanakula vumbi ma CID wanashinda Bar wanakunywa bia tu

Mkuu hayo yote unayosema ni ya ukweli.. Nadhani tunahitaji overhaul kwenye jeshi na ianzie juu.. Kwa maoni yangu vijana wapewe nafasi kwenye uongozi wa juu maana hawa wako creative na wana uthubutu.. Unajua wanaweza kuangalia kinachofanywa kwenye nchi nyingine na wakajiapiza wanaweza kufanya hapa, wakati hawa viongozi wa sasa ukiwauliza kuhusu wenzetu walivyoendelea wanakujibu hao walianza zamani na pia ni nchi tajiri.. Hayo majibu ambayo unayapata toka kwa viongozi wa jeshi la Police..
Unaona ugumu hapo..
 
Sasa kama polisi wenyewe ndiyo hao wanaoshirikiana na watuhumiwa tutegemee nini mkuu

Hilo ndilo tatizo jingine.. Na sadly wananchi wengi wamevunjika moyo kutokana na ukweli huo Mkuu..
 
Kuna matukio ambayo yanawahusu polisi ama familia zao yakitokea wanayafanyia kazi ndani ya muda mfupi na upelelezi uliotukuka,lakini haya ya kina sie duuuuuuuu inachukua miaka nenda rudi upelelezi haujakamilika.

Hapo ndo huwa napata shida kigodo iweje ya kwao upelelezi unakamilika haraka na ya kina sie upelelezi unadinda?
 
Ningekuwa mshauri wa raisi mambo ya usalama ningemwambia avunje utaratibu wa uendeshwaji wa jeshi la polisi.. Kuna baadhi ya wakuu humo ndani wanaendekeza rushwa na kesi inaisha simple endapo wafiwa hawatasimamia.. Kiukweli jeshi la polisi na vitengo vyake vyote vijitathimini kila mara kama alivosema Rais.. Wanatia aibu na raia sisi tunapenda kuwa na imani nao kuna matukio ya mauaji vijijini yanapotezewa kabisa.. Ila wewe umetoa ushaur mzuri kipindi polisi na wananchi wanapiga vita rushwa basi muhimu technology zaidi ikaanza kutumika wataalam waongezeke jeshi la polisi kesi mtuhumiwa Anakamatwa GUILTY na full evidence
 
Kuna matukio ambayo yanawahusu polisi ama familia zao yakitokea wanayafanyia kazi ndani ya muda mfupi na upelelezi uliotukuka,lakini haya ya kina sie duuuuuuuu inachukua miaka nenda rudi upelelezi haujakamilika.

Hapo ndo huwa napata shida kigodo iweje ya kwao upelelezi unakamilika haraka na ya kina sie upelelezi unadinda?

Hata hayo unayodhani wanayafanyia kazi ndani ya muda mchache na kuwakamata watuhumiwa, ukija kufuatilia mahakamani unaweza kusikia watuhumiwa wameachiwa kutokana na kutokuwapo na ushahidi wa kutosha.. Kinachofanyika ni Police kupeleka jalada lenye confession toka kwa mtuhumiwa/watuhumiwa.. Na wanapokuwa mahakamani watuhumiwa huwa wanayaruka maelezo waliyoyatoa Police, kwa kusema kwamba hawakuyatoa kwa hiari yao.. Sasa hapo Police inabidi watafute ushahidi mwingine ambao hawana..
 
Elimu elim Ilmu
Angalau kwa kuangalia TV discovery investigation
Itawapa uweledi wa kufanya kazi zao barabara.
 
Haikuhitaji kuwa na ufahamu mkubwa kujua kuwa tuliowakabidhi dhamana ya kulinda usalama ni kwamba wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo au wamezidiwa nguvu na wahatarishi wa usalama wetu na mali zetu....ikiwa ni hivyo basi hao wahusika tuliowakabidhi kazi hiyo hawana budi kuachia ngazi mara moja kwani hakuna haja ya kuendelea na kazi umeishindwa....itakuwa ni aibu kwa taifa letu ikiwa kodi zetu bado zitaendelea kukatwa mishahara ya hawa jamaa......
 
Ndiyo Mkuu hapa Suala kubwa ni Elimu ili kuendana na Mahitaji husika ya huu wa Science na Technology iliyopo kwa sasa.
Sema Watakuja hapa majamaa/ wakubwa / wahusika kwenye idara yenyewe huenda wakatema cheche , kutoa Mapovu au kuzalisha Uzi ndani Uzi .
Design kama mnakosoa utendaji kazi wa Jeshi la police Kitu sio Kizuri.
Obviously liko poa sema machache yanalikumba ;- Facilities and Elites to copy with the Particular time.
 
KikulachoChako umezungumza vizuri.. Swali huna imani na huyu kiongozi wa awamu ya tano, kuweza kutekeleza mabadiliko makubwa kwenye Jeshi la Polisi..?
 
Hao waliokwisha kamatwa na kupatikana na hatia mbele ya mahakama kesi zao ulipeleleza wewe? muwe waungwana basi hata kidogo polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu, hata hayo wanayoyafanikisha wanastahili pongezi.
 
hivi hizi DNA zinazopimwa kwenye matukio wanaenda kuzilinganisha wapi?

Hakuna DNA ambazo zinachukuliwa sehemu za matukio hapa kwetu.. DNA inatumika kwa wanaume ambao wana mashaka kama wamebambikiwa watoto, but not for crime sakes..
 
DNA unaichukuaje kwenye tukio, au munamaanisha damu na majimaji mengine yatokayo katika mwili wa binadamu.
 
Hao waliokwisha kamatwa na kupatikana na hatia mbele ya mahakama kesi zao ulipeleleza wewe? muwe waungwana basi hata kidogo polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu, hata hayo wanayoyafanikisha wanastahili pongezi.

Ungekuwa unafuatilia haya mambo ya kesi za jinai, ungeelewa pointi yangu.. Unafuatilia kesi ambazo zipo kwenye mahakama za rufaa..? Fuatilia huko ndo utagundua ninachosema.. Wahalifu wanashinda rufaa kwa sababu Majaji wa mahakama kuu na rufani kuona ukiukwaji mkubwa kisheria kwenye hukumu.. Huwezi kumtia hatiani mtuhumiwa kwa maelezo yaliyochukuliwa na Polisi kituoni bila ya kuwapo hata kwa mwanasheria wa mtuhumiwa..
 
Back
Top Bottom