Ongezeko la Ajira kwa watoto, Serikali kupitia ustawi wa jamii imejisahau?

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
7,248
2,000
Achia mbali ongezeko la watoto wa mtaani katika miji yote mikubwa.,
Tatizo lingine linaloonekana kwa sasa ni wingi wa ajira kwa watoto wenye umri kati ya miaka 9-13. Tena katika mfumo tofauti tofauti kama ifuatavyo.

Kwa maeneo ya mjini watoto wenye umri tajwa hapo juu siku hizi ndo hutumika kuwaongoza omba omba barabarani, masokoni, Madukani nk. Hufanya Kazi hiyo kutwa nzima wakizunguka mjini mzima hadi giza linapoingia,na baada ya kazi hupewa fungu lao.

Kuuza mifuko, Wazazi na matajiri huwapa watoto mifuko kwenda kuuza masokoni na minadani na baadae jioni hupeleka hesabu kwa wawaliowatuma.

Ubebaji wa mizigo, Katika masoko mengi kuna idadi kubwa ya watoto ambao hutumika kuwabebea mizigo wateja wanaokuja kununua mahitaji mbalimbali sokoni.,hubeba vifurushi hivyo hadi kwenye vituo vya daladala au kwenye magari yao kwa ujira wa Tsh. 500-1000.

Watoto wengine wenye umri tajwa hapo juu wamekuwa wakipewa bidhaa mbalimbali za biashara kama vile miwa.,kahawa na vitu vingine vidogo vidogo watembeze mitaani.

Wafanyakazi wa majumbani , watoto wa umri huo wamekuwa wakisafirishwa kwenda mikoa mbalimbali kwaajili ya kazi za ndani, na wengine wakienda kutumika kwa ajili ya kwenda kufuga mifugo.

Watoto wenye umri tajwa hapo wanatakiwa wawe shuleni tena chini ya uangalizi wa wazazi
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
8,714
2,000
Bora hata hao madogo Wanaingiza hela,Kaka na dada zao wanamaliza Universities na hakuna ajira na hawaingizi hata mia kwa siku.Madogo chapeni kazi.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
54,722
2,000
Hivi viongozi na watendaji wa vijiji na mtaa wanajua idadi ya watoto katika maeneo yao.

Wanaoishi maisha magumu
Wasioenda shule
Wenye ulemavu na magonjwa sugu.
Uhakika wa matibabu yao.
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
8,714
2,000
Hivi viongozi na watendaji wa vijiji na mtaa wanajua idadi ya watoto katika maeneo yao.

Wanaoishi maisha magumu
Wasioenda shule
Wenye ulemavu na magonjwa sugu.
Uhakika wa matibabu yao.
Waliambiwa wazae kadiri wawezavyo elimu Ni bure.
 

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
7,248
2,000
Hivi viongozi na watendaji wa vijiji na mtaa wanajua idadi ya watoto katika maeneo yao.

Wanaoishi maisha magumu
Wasioenda shule
Wenye ulemavu na magonjwa sugu.
Uhakika wa matibabu yao.
Ningekuwa na uwezo ningeanzisha hata NG'O, haswa kwa hao wenye ulemavu na magonjwa sugu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom