Ongezeko la ada ya uwanja wa ndege

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,537
32,145
Wadau!
Jana nilikuwa safarini kuelekea Afrika kusini nilikata tiketi toka tarehe 3 na SOUTH AFRICA AIRWAYS sasa jana nafika uwanjani naambiwa niongeze dola 10 kwa kuwa ADA YA UWANJA WA NDEGE imepanda toka 30 USD to 40 USD toka tarehe 01/07/2012 nikawauliza mbona mimi nimekata tiketi tarehe 3/7(baada ya tarehe 1/7/2012) wanasema wao hawajui hilo wanachotaka ni ni hela kama sina hawaniruhusu ku-check-in hivyo niahirishe safari. Najiuliza hivi kwa nini watu/abiria wasiarifiwe mapema mabadiliko yoyote yanayotokea kabla kodi husika kutozwa? hivi wageni wanatuonaje waTZ kwa hili? wasi wasi wangu ni kuwa huu ni mradi wa mtu binafsi pale AIRPORT! maana ukidai risiti hupewi unaambiwa risiti zimeisha? So wadau mnaotaka kusafiri kwa ndege ndani/nje ya nchi jiandaeni na kadhaa ya kudaiwa pesa zaidi ukifika uwanja wowote wa Ndege ndani ya Tanzania be it JNIA,KIA, Mwanza, TBR,KGM,MTWR,ZNZ etc.
 
Pole Joshua! Leo mchana yamenikuta na mimi nilikuwa naenda Mwanza nikaambiwa niongeze 10,000/= kama AIRPORT SERVICE CHARGES nikadai risiti nikazungushwaaaa mpaka karibu ndege iniache nikaambiwa nikirudi nitaikuta duuuh! Ndo TZ yetu hiyo kaka
 
andreakalima wewe si mkweli!
Kiasi cha Airport service charge kilichoongezeka kwa Local trips ni Tshs 5000 tu, na kwa hiyo kama ni kuongeza utakuwa umedaiwa extra 5K tu na si 10K!.
Kwa safari za nje ya nchi ni sahihi kabisa, ongezeko ni 10K.
Kwa mtazamo wangu ongezeko hili limekuja wakati muafaka maana bei hizo mlizozizowea zimedumu kwa zaidi ya miaka 10 ndiyo maana mnaziona kama mna hati miliki nazo.
Badilikeni bana!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu PakaJimmy!
mimi sipingi kuongezeka! nashauri ni bora mtu apewe taarifa mapema/ijumuishwe kwenye nauli na si kumshtukiza mtu. Zaidi nimefanya ka-utafiti kwa nchi kadhaa TZ ina vijigharama mshenzi vingi sana inayofanya kupanda ndege kuwe ni anasa na kitu cha kufikirika sana. halafu mapovu yanawatoka kuwa Kenya,Rwanda na South Africa wanawachakachua kwenye utalii nawaambieni vitu vidogo kama hivi ndio vinafanya TZ kutokuwa Major Tourist Destination achilia mbali kukosa huduma nzuri kwa wageni (taxi, hoteli,),wizi, ktojitangaza etc
 
Sasa hivi pale Airport wale jamaa wa IMMIGRATION nao wameongeza ka "kodi" mshenzi eti kaka tunaomba "CHAI" inatia hasira kwa kweli
 
duh sasa hii ni kero mbona kienyeji hivi na kama haziingii mikononi mwa watu why hamna risiti. ahsante kwa taarifa kiongozi wiki hii nina safari ya ndani ngoja nijiandae
 
Back
Top Bottom