Ongeza ufaulu wa somo la history kwenye shule/centre yako

swahili state

JF-Expert Member
Oct 14, 2014
261
146
Dhumuni kubwa la uzi huu ni kuuelezea umma kuwa Mimi ni miongoni mwa walimu bora mwenye mchango mkubwa kwa wanafunzi wasomao somo la history. Nimewasaidia wengi na matokeo yao yalikuwa makubwa sana mana nina fundisha kwa kutumia kanuni niliyoibuni iitwayo TQE( sitoweka wazi tafsiri yake kwa sasa).

Nimeweza kubadili matokeo katika shule na vituo nilivyowahi kuzunguka hapa nchini pia najiona kama dhahabu iliyofunikwa na tope zito mana nina uwezo mkubwa ila cha kusikitisha sina jina kubwa wala sifahamiki kama baadhi ya walimu wengine.

Nimewahi kuwafundisha wanafunzi kutoka katika shule kubwa na wakakiri uwezo wangu ni tofauti na walimu wao wa history kwenye mashule yao.

Kwa sasa ni mwalimu wa kujitegemea ambaye ninafundisha masomo ya ziada kwa watu wazima na wasio na muda wa kutosha wa kujiunga na vituo mbali mbali. Pia napatikana Dar-es-salaam japo ninakuwa na ratiba za kuzunguka kwenye vituo vya mikoani.

Maneno mengi hayajengi ghorofa ila kama unahitaji kupata mbinu(TQE) za kufaulisha kwenye shule yako au kituo chako, usisite kunitafuta na sitotanguliza maslahi mbele mana nitaomba unipatie wiki moja tu nifundishe vipindi kwenye madarasa mbali mbali bila malipo yoyote baada ya hapo tutapanga kila kitu kutokana na mwitikio wa wanafunzi.
Ukinihitaji unaweza ukani pm kisha tutawasiliana Zaidi na ntakuja kukuonesha vitendo si maneno tena.

Naamini wapo walimu wengi ambao wanambinu kubwa za kufundisha ila hawatambuliki wameishia kukaa majumbani bila ajira huku mashule yakiwa na walimu ambao wapo sawa au wamezidiwa mbinu kiasi Fulani na hao waliopo majumbani.

Ntawaaga kwa zawadi ya swali la o-level na advance ambayo nililetewa siku ya jana na wanafunzi wangu.

1. Why uneven scramble for the world in the 19th century?(O-level)

2. "States in pre-colonial Africa were imposed by super natural powers". Refute this fallacy by giving six facts.( A-level/history one).

Nikipata wasaa nitasolve maswali ya history ndani ya huu uzi, ukinihitaji utani PM, karibuni.
 
Why uneven scramble for the world in the 19th century?
Kwanza kabisa kabla mwanafunzi hajafanya swali inampasa kutambua swali hilo limetoka topic gani,topic hiyo ina vipengele gani, swali ni la kipengele gani,kipengele hiko kinamata asome nini, mwisho kujua swali kwa ujumla linataka nini.
Swali letu hapo juu ukimpa advance atalielewa kwa uelewa mpana kutokana na topic inayotoa ilo swali kwa upande wa advance(Imperialism and territorial division of the world),kipengele kinachotoa ilo swali(To discuss the reasons for colonial rivalry in Africa,the Middle East and the Far East) kutokana na hayo advance atatanua mawazo yake.
Ila kwa ndugu zangu wa o-level akiliona anaweza kuwaza mbali lakini mwongozo unamtaka awaze Zaidi kuhusu Africa na kisha maeneo mengine. Kwa kifupi swali linataka uoneshe kwanini scramble haikuwa sawa mana kuna baadhi ya maeneo(Nigeria, East Africa,South Africa,North Africa)yaligombewa sana na kuna baadhi ya maeneo(Somaliland) yaligombewa kidogo au hayakugombewa kabisa. Hapa utaeleza mambo yaliyowavutia kwenye yale maeneo ambayo yalipata kugombewa sana.
Tukienda kwenye swali.
INTRODUCTION
Hapa lazima mwanafunzi azingatie vipengele muhimu vinavyo hitajika na ambavyo vitavyomfanya msahihishaji avutiwe na uandishi ila kabla hajaanza kushughulika na vipengele hivyo ni lazima atambue neno la msingi linalobeba swali(key word) kisha atalitumia katika vipengele vyote vya kwenye introduction. Baadhi ya vipengele hivyo ni kama, Definition, hapa mwanafunzi atadefine neno la msingi ambapo kwenye swali letu neno la msingi ni scramble hivyo basi atatoa maana ya scramble,mfano scramble was the colonial rivalry between the capitalist nations.
Kipengele kingine ni period, hapa mwanafunzi ataeleza muda wa tukio halisi, mfano scramble for took place during the second half of the 19th century.
Kipengele kingine ni,Place, hapa mwanafunzi ataeleza eneo la utendekaji wa tukio,mfano, European powers scramble for external world especially African countries.
Kipengele kingine utaonesha,participants, hapa mwanafunzi ataonesha wahusika wakuu na wadogo wa hilo tukio,mfano, scramble for involve capitalist nations like Britain,France,Germany,Portugal,Holland,Belgium and Italy.
Na kuna kitu cha mwisho ambacho pia ni muhimu kwenye introduction(sitokiweka wazi) ila ukimaliza introduction kabla ya kuanza main body kuna connecting point inayounganisha intro na main body. Nawaelekeza wanafunzi wangu mbinu nzuri za kuiandika.
MAIN BODY
Hapa kuna kanuni yake ambayo ukiifahamu utaona urahisi wa main body ila usipoifahamu utapata shida. Ila lazima ukumbuke kuwa unapaswa kuandika point sahihi,kuielezea point sahihi uliyoiandika na kuitolea mfano ili uitetee.
Mfano, swali letu points zake ni kama, High population(nimeandika point sahihi),European power compete for the areas with large number of people because high population ensure availability of market and cheap labour(nimeelezea point sahihi). For instance, Nigeria experienced intensive scrambe due to its population pressure(nimetoa mfano wa points sahii). Points nyingine ni kama(sitozielezea), availability of the water bodies,favourable climate condition, agriculture potential,mineral potential and strategic areas.
CONCLUSION
Hapa walimu wengi wanasema hakuna kanuni ya uandishi wa conclusion ila kwangu kanuni ninayo na niliipata kwa kushirikiana na team ya wanafunzi wenzangu tulipokuwa chuo kikuu. Nitafute nikupe kama unapata mkanganyiko. Ila kikubwa wengi hupendelea kuanza na maneno kama generally, therefore, in summary na mengineyo ila ntakwambia utumie neon lipi.
Nawasilisha.
 
Nashukuru kwa wote mnaoni pm, pia nawakaribisha wote, mtaniwia radhi kwa wale ninaochelewa kuwajibu mana wanaonitafuta ni wengi na ninapenda nimjibu kila mtu kwa kirefu.
 
Tukidamka nitakuja na concerns zangu kadhaa.. please, i am kindly requesting you to be open minded ili tuutanue huu mjadala..
 
Umeelezea tu sababu za upande wa Africa lakini pia kwa upande wa nchi za Ulaya unaweza ukapata baadhi ya sababu zao kujibu hilo swali....
Mfano nchi kama Britain na France kutokana na uwezo wao na mahitaji yao waligombania maeneo mengi kuliko akina Portugal na Spain...
 
Mleta mada hilo swali ni pana sana zaidi ya ulivyolidadavua..sema unatakiwa uwe wazi kuwa unatafuta ajira...
 
Why uneven scramble for the world in the 19th century?
Kwanza kabisa kabla mwanafunzi hajafanya swali inampasa kutambua swali hilo limetoka topic gani,topic hiyo ina vipengele gani, swali ni la kipengele gani,kipengele hiko kinamata asome nini, mwisho kujua swali kwa ujumla linataka nini.
Swali letu hapo juu ukimpa advance atalielewa kwa uelewa mpana kutokana na topic inayotoa ilo swali kwa upande wa advance(Imperialism and territorial division of the world),kipengele kinachotoa ilo swali(To discuss the reasons for colonial rivalry in Africa,the Middle East and the Far East) kutokana na hayo advance atatanua mawazo yake.
Ila kwa ndugu zangu wa o-level akiliona anaweza kuwaza mbali lakini mwongozo unamtaka awaze Zaidi kuhusu Africa na kisha maeneo mengine. Kwa kifupi swali linataka uoneshe kwanini scramble haikuwa sawa mana kuna baadhi ya maeneo(Nigeria, East Africa,South Africa,North Africa)yaligombewa sana na kuna baadhi ya maeneo(Somaliland) yaligombewa kidogo au hayakugombewa kabisa. Hapa utaeleza mambo yaliyowavutia kwenye yale maeneo ambayo yalipata kugombewa sana.
Tukienda kwenye swali.
INTRODUCTION
Hapa lazima mwanafunzi azingatie vipengele muhimu vinavyo hitajika na ambavyo vitavyomfanya msahihishaji avutiwe na uandishi ila kabla hajaanza kushughulika na vipengele hivyo ni lazima atambue neno la msingi linalobeba swali(key word) kisha atalitumia katika vipengele vyote vya kwenye introduction. Baadhi ya vipengele hivyo ni kama, Definition, hapa mwanafunzi atadefine neno la msingi ambapo kwenye swali letu neno la msingi ni scramble hivyo basi atatoa maana ya scramble,mfano scramble was the colonial rivalry between the capitalist nations.
Kipengele kingine ni period, hapa mwanafunzi ataeleza muda wa tukio halisi, mfano scramble for took place during the second half of the 19th century.
Kipengele kingine ni,Place, hapa mwanafunzi ataeleza eneo la utendekaji wa tukio,mfano, European powers scramble for external world especially African countries.
Kipengele kingine utaonesha,participants, hapa mwanafunzi ataonesha wahusika wakuu na wadogo wa hilo tukio,mfano, scramble for involve capitalist nations like Britain,France,Germany,Portugal,Holland,Belgium and Italy.
Na kuna kitu cha mwisho ambacho pia ni muhimu kwenye introduction(sitokiweka wazi) ila ukimaliza introduction kabla ya kuanza main body kuna connecting point inayounganisha intro na main body. Nawaelekeza wanafunzi wangu mbinu nzuri za kuiandika.
MAIN BODY
Hapa kuna kanuni yake ambayo ukiifahamu utaona urahisi wa main body ila usipoifahamu utapata shida. Ila lazima ukumbuke kuwa unapaswa kuandika point sahihi,kuielezea point sahihi uliyoiandika na kuitolea mfano ili uitetee.
Mfano, swali letu points zake ni kama, High population(nimeandika point sahihi),European power compete for the areas with large number of people because high population ensure availability of market and cheap labour(nimeelezea point sahihi). For instance, Nigeria experienced intensive scrambe due to its population pressure(nimetoa mfano wa points sahii). Points nyingine ni kama(sitozielezea), availability of the water bodies,favourable climate condition, agriculture potential,mineral potential and strategic areas.
CONCLUSION
Hapa walimu wengi wanasema hakuna kanuni ya uandishi wa conclusion ila kwangu kanuni ninayo na niliipata kwa kushirikiana na team ya wanafunzi wenzangu tulipokuwa chuo kikuu. Nitafute nikupe kama unapata mkanganyiko. Ila kikubwa wengi hupendelea kuanza na maneno kama generally, therefore, in summary na mengineyo ila ntakwambia utumie neon lipi.
Nawasilisha.
unatafuta jina
Waweza pata ila una uelewa wa kawaida
 
unatafuta jina
Waweza pata ila una uelewa wa kawaida
Wanaharakati kama Nelson Mandela na Robert Mangaliso Sobukwe kwa mara ya kwanza walionekana wanatafuta majina ila wao waliweka wazi kuwa dhumuni lao ni kupambana na serikali ya makabulu kutokana na sera ya kibaguzi iliyoanzishwa mnamo mwaka 1948 na ilijulikana kama apartheid policy.
Wanaharakati hawa walienda mbali Zaidi mfano, mwezi wa kumi na mbili mwaka 1959 wanachama wa ANC walifanya kikao ambacho kiliazimia kuipinga sheria iliyopitishwa na makaburu ambayo iliwataka Africans wasifike kwenye maeneo waishiyo makaburu. Pia wanachama wa Pan Africanist Congress (PAC) chini ya Robert Sobukwe nao waliazimia kufanya maandamano ya amani kupinga sheria hiyo ya makaburu. Robert Sobukwe aliacha kazi yake ya uhadhiri katika chuo kikuu cha Witwatersrand na kuamua kufanya harakati za kupinga sera za kibaguzi ila bado wazungu waliendelea kuamini kuwa anatafuta jina.
Mnamo tarehe 21/3/1960 wanachama wa PAC wanaokadiriwa walikuwa 5,000 waliandamana na kwenda kwenye kituo cha polisi, hamad! Polisi waliuwa wafuasi wa PAC kama 69 na kujerui kama 180 kisha wakamtafuta mwanaharakati ambaye mwanzo walifikiri anatafuta jina na pia walifikiri ana uwezo wa kawaida kumbe walijidanganya, mwisho waliamua kumfunga miaka mitatu mana waligundua mtu huyo hakuwa akitafuta umaarufu bali alikuwa anatafuta ukombozi na pia hakuwa na uwezo wa kawaida bali alikuwa na uwezo mkubwa mithili ya wanafalsafa kama John Locke, Baron Montesquieu,Jean Jacques Rousseau na Karl Marx yule mwandishi maarufu wa vitabu vya The Das Capita na The manifesto of communist party.
NAWASILISHA.
 
Mleta mada hilo swali ni pana sana zaidi ya ulivyolidadavua..sema unatakiwa uwe wazi kuwa unatafuta ajira...
Unaweza ukawa unaelekea kwenye ukweli kiasi fulani mana kuna connection kubwa kati ya ajira na kuwasaidia watu, ndio mana daktari yupo pale kusaidia watu ila pia udaktari ni ajira, mwanajeshi analinda mipaka ya nchi ila pia ni ajira.
Mfano, mwaka 1625 huko England alifariki mfalme aliyejulikana kama King James 1, hivyo basi ilibidi arithiwe na mwanaye ambaye aliitwa Charles 1.
Charles 1 aliiongoza England vibaya na aliliamuru bunge liwe linampatia pesa ambazo alizitumia kwa matumizi yake binafsi hali iliyopelekea kutokea kwa ugomvi mkubwa kati yake na bunge.
Mnamo mwaka 1629, Charles 1 alilivunja bunge na aliongoza kwa miaka 11 bila kuwa na bunge, Mwaka 1640 mfalme alilirudisha bunge ila kipindi hiko alikuwa amegombana na watu wa Scotland mana aliwaamuru wafuate misingi ya kianglican na waachane na mafundisho ya kikatoliki.
Mfalme alilitaka bunge limpe pesa nyingi iliaweze kuinvest kwenye vita ila bunge liligoma na akalivunja pia akatishia kuuwa wabunge hapo alitokea raia wa kawaida aliyejulikana kama Oliver Cromwell ambaye aliamua kuongoza mapambano ya kumng'oa King Charles 1, ikumbukwe Oliver Cromwell hakuwa akitafuta ajira bali aliamua kujitolea ili awasaidie watu.
Mapambano kati ya King Charles 1 na wanaompinga chini ya Oliver Cromwell yalianza mwaka 1642 hadi mwaka 1649 na mfalme alipigwa vibaya kama kipigo cha mbwa aliyekula mboga ya mchana.
Baada ya kipingo mfalme aliuliwa na Oliver Cromwell aliteuliwa kuwa kiongozi hapo akapata ajira.
MY TAKE
Ukijitolea kwa jiri ya watu na ukaonesha uwezo ajira itakuja mana ajira na kujitolea ni pande mbili za sarafu kama fani na maudhui.
 
Back
Top Bottom