Oneni madhara ya kutumia kichwa kuongoza badala ya sheria na miongozo

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
1.mkurugenzi wa wilaya ya ********* amewataka watumishi kufika kazini saa 12:30 alfajiri na kutoka saa 10 jioni tena ka vitisho , sasa sijui watumishi wafuate lipi sheria za utumishi au mawazo ya mkurugenzi, chanzo cha tatizo =??

2. Afisa elimu wilaya********* amewataka waalimu kutoka saa 12:00 jioni eti kisa wakitoka mapema wana zurura mitaani - huu ni udhalilishaji na ndio madhara ya kutumia kichwa na kuweka miongozo pembeni kwa kudhani walio iweka hawana akili kumbe walijua tukifuata akili ya mtu kuongoza badala ya kanuni zilizo pagwa kuna watawala wengine ni vichaa wa akili wanaweza kujisikia na kuwa ambia watumishi wote waende kazini uchi kisa tu amejisikia kufanya hivyo au amependa kumuona fulani akiwa uchi ana fananaje

. Jamani mlio pewa mamlaka fuateni sheria za utumishi wa umma zina sema nini na zina maana sana kuwepo msidhani nyie ndio mwajua kufikiri kuliko miongozo iliyopo hapa nyie mpo hapo kwa kuzingatia matakwa ya sheria

Nilicho kigundua ni baada ya baadhi ya viongozi kugundua kuwa mfumo wa serikali ya sasa ni wa kukiuka matakwa ya sheria hivyo viongozi wasio waadilifu na wenye akili ndogo wanatumia mwanya huo kukomoa watumish walio chini yao na kuwakandamiza kinyume na sheria

Ifike mahali TAMISEMI muwe mnawapa hawa watu semina za mara kwa mara kuhusiana na haki za watumishi na ikiwezekana kuwaadhibu pale watakapo kiuka miongozo kwa namna yeyote ile na kusababisha udhalilishaji kwa mtumishi

maana ni ukweli usio pingika kuwa watumishi huku chini wana nyanyasika sana na hawa watendaji wanao taka kujifanya wako juu ya sheria na kibaya zaid serikali kama imeachana kabisa na swala la kuwatetea watumishi, hakuna kauli za kufariji mrumishi wa umma kila siku ni vitisho ,makalipio sijui hii ni aina gani ya uongozi ,

Hakuna utendaji kazi bora kama hakuna ushirikishwa mzuri baina ya mtawala na mtawaliwa , kama kuna wanao amini eti vitisho na makalipio kila siku ndio uongozi bora basi nadiriki kusem WATUMISHI WA UMMA MNAONGOZWA NA WATU WENYE AKILI NDOGO NA WENYE UWEZO MDOGO KABISA TENA WA KIWANGO CHA CHINI KABISA KUFIKIRI hivyo ziteteeni nafsi zenu wenyewe maana hawa wenye akili ndogo watawaumiza sana maana hawana akili za uongozi bali ni manyapara.
 
Hapo ni kazi
bora huyo Mkurugenzi anaye himiza kazi
kuliko Lisu anaye ombea kuliangamiza Taifa
Kuna mada zingingine muwe mnawaacha wenye akili wachangie nyie vichaa msubiri zinazo endana na hali yenu, maswala ya lisu hapa yana tafuta nini? Nchi haita endelea kama hata katika mambo ya kitaalamu vichaa mnaingiza siasa
 
Kina mmoja nasikia ilipotoka List ya incomplete ya vyeti yeye akazuia mishahara.utumishi wakamkana.ila huyu sishangai coz anavutaga bangi
Hawa viongoz wa awamu hii wengi wao sijui wameokotwa jalala gani hawana sifa ya hata kuwa viongozi wa vijiwe vya gongo wana akili ndogo kiasi kwamba hata mtoto wa miaka 6 anayaona madhaifu yao
 
Hapo ni kazi
bora huyo Mkurugenzi anaye himiza kazi
kuliko Lisu anaye ombea kuliangamiza Taifa
Comrade
Lazima tukubaliane kutokubaliana mtazamo kuhusu masuala ya Taifa.

Hata Nyerere watu walimpinga mawazo yake na kuna aliyoyachukua ya wapingaji.

Nchi yetu sote Wakulima na Wafanyakazi
.... Kiongozi yeyote hata angekuwa nani a kienda kinyume na akatenda isivyo halali Lazima apingwe kwa kuambiwa inavyopasa.
Kwani yeye amekuwa Mungu?

Tuacheni kuwatisha Watanzania wenzetu....mbona sisi tupo katika Mfumo toka awamu zilizopita na hatuwatendei yasiyopaswa Wananchi wenzetu, nyie ni akina nani ?

Miaka inakimbia sana bora kuishi kwa kumuogopa Atupae Uzima kuliko Mwanadamu anayekufa Leo au kesho

Chief Economist
 
Hapo ni kazi
bora huyo Mkurugenzi anaye himiza kazi
kuliko Lisu anaye ombea kuliangamiza Taifa
"Tunachohitaji sio wingi wa watu bali watu wenye moyo na maendeleo." From Kijiji Chetu.

So, issue sio kukesha ofisini tena nje ya saa rasmi za kazi bali issue ni ufanisi!!

Watu walio results oriented hawajali unaingia ofisini saa ngapi na unatoka saa ngapi... what they want ni RESULTS! Hata kama unafanya kazi 24/7 lakini delivery ni poor then you're shit as hell compared na yule anayefanya kazi 3 hours/day na ku-deliver maximum results!

Kwahiyo anachotakiwa kuhimiza DED sio watu kufanya kazi nje ya saa rasmi za kazi bali to fully utilize working hours!!!
 
Mbona ukiambiwa ukweli unavimba kama puto? Ni kweli mada zingine muzipishe tuu kwani ni kiwango cha juu ambacho hamjafikia
Yaani hawa vichaa sijui nao waliokotwa jalala gani maana wao kila kitu wanaweka siasa mi nimeeleza matatizo wanayo yapata watumishi kutoka kwa viongozi wapumbavu wanao waoongoza yeye ananiletea habari za kina lisu sijui karogwa huyu ,
 
"Tunachohitaji sio wingi wa watu bali watu wenye moyo na maendeleo." From Kijiji Chetu.

So, issue sio kukesha ofisini tena nje ya saa rasmi za kazi bali issue ni ufanisi!!

Watu walio results oriented hawajali unaingia ofisini saa ngapi na unatoka saa ngapi... what they want ni RESULTS! Hata kama unafanya kazi 24/7 lakini delivery ni poor then you're shit as hell compared na yule anayefanya kazi 3 hours/day na ku-deliver maximum results!

Kwahiyo anachotakiwa kuhimiza DED sio watu kufanya kazi nje ya saa rasmi za kazi bali to fully utilize working hours!!!
Nashikuru kwa kumuelimisha huyo kichaa maana ninapo mwambia mada zingine wawaache wenye akili timamu wachangie na vichaa wasubirie mada zao anadhani natania ,
 
Hujitambui
ungeipeleka Kwa dadako mkajadili wenyewe
Mawazo ya kimakinikia na ya faru john. Wewe unajiyambua kwa lipi hasa? Mbona unajiona kuwa unajua kumbe mweupe sana? Wewe una dafa mwenye kujitambua zaidi ya wale waliozaa wakiwa darasa la nne? Punguza uhayawani wako humu jf na ukijibu hoja kuwa na staha na adabu.
 
Me mambo hayo ndo yalinikimbiza serikalini. Kazi nilikuwa naipenda lakin Umwinyi na Comands zisizo na msingi ndo zilinikimbiza
 
yuko sahihi watumishi wengi wakitoka mapema wanaenda kwenye ulevi na uzinzi wengine wanakuwa idle bora watoke hata saa 2 usiku waende nyumbani
 
Back
Top Bottom