Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Castle

Senior Member
Jul 25, 2008
116
20
Habari za saa hizi wakuu,

Niende kwenye mada husika. Nina mwaka wa tano naumwa sana tumbo na maumivu yakiwa yanahama sehemu mbalimbali za tumbo wakati mwingine kifuani, kwenye, mbavu na hata kiuno na nyonga. Nimetumia madawa mbalimbali sipati nafuu.

Nimeshapima magonjwa kama yote. Nimejaza mafile ya makaratasi ya hospital. Natibu vidonda visivyopona. Sina raha nimepoteza ufanisi katika uchakalikaji wa kusaka kipato. Sina raha napata riziki si haba ila siifurahi. Sili ninachokitamani.

Nimeshafanya Endoscope 3 (mpira wenye kamera tumboni) zote zinaonyesha nina vidonda lakini nakunywa dawa siponi. Hii ya tatu nimefanya majibu yametoka baada ya week 3.Dokta kaniandika madozi mengine ila anipi ufafanuzi vizuri kama niko kwenye hali gani.

Niko stage gani? Ananiambia ni michubuko ya kawaida tu nitapona. kweli? mwaka wa tano mnanipa moyo tu? Aisee hata sielewi, nataka ukweli. Picha zinanishangaza nazidi pata wasiwasi zaidi. Na nimechoka kunywa dawa za hospital zinaniongezea maumivu hata sijui nifanyaje.

Tafadhali mtaalam yeyote ama aliyepitia changamoto kama zangu naomba msaada wako wa mali. Nishauri nifanyaje maana nilisikia mpaka mkojo wa asubuhi inaponya. Nilikunywa na sikupona.

Naambatanisha na majibu ya hospital pamoja na picha (OGD). Pia naomba kufahamu kwanini hii picha hapa chini ina vidude vyeusi ni alama ya vidonda kupona au ndio nazidi kulika.

Asanteni.

1597406324307.png

UFAFANUZI WA KITAALAMU KUHUSU TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ni nini?
Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana kama maji ya betri.

Vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao HELICOBACTER PYLORI, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non_steroids anti inflammatory drugs kama vile ASPIRIN /DICLOFENAC huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo.

1597406248426.png

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE)
Kuna aina nyingi za vidonda vya tumbo navyo ni
(a) vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni
b) vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo
(c) vidonda vinavyotokea katika koo /koromeo la Chakula

HATUA KUU ZA VIDONDA VYA TUMBO
ni vizuri kufaham kwamba huu ugonjwa una hatua nne ambazo ni muhimu

(1)HATUA YA KWANZA ~hatua ya kwanza ya huu ugonjwa ni ule uvimbe sugu unaotokea sehem ya ndan ya tumbo.

(2)HATUA YA PILI~hapa vijidonda hujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hvyo huongezeka na kua vikubwa katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia, tumbo kujaa gesi wakati wote, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu.

Hata hivyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu (CHRONIC DYSPEPSIA) yani kushindwa kufanya Kazi kwa mfumo wa mmeng'enyo wa Chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni huingia Kwenye mzunguko wa dam hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayar iko katika mfumo mzima wa damu.

(3) HATUA YA TATU ~hii ni hatua ambayo ni ya hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa yote midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumbon na kubadilisha rangi ya choo kuwa cyo ya kawaida, pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara, maumivu makali ya tumbo,hupata Homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.

(4)HATUA YA NNE ~katika hatua saratani ya utumbo inahusika kwani katika hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo.

VISABABISHI/ VIHATARISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO
visababishi vya ugonjwa huu vipo vingi sana hivyo yatupasa kuviepuka ili kujiepusha na huu ugonjwa.zifuatazo ni visababishi vya ugonjwa huu
i. Utumiaji wa madawa ya kuondoa maumivu kwa muda mrefu
ii.mawazo na huzuni kwa muda mrefu
iii.kutokuwa na muda maalum wa kula
iv.Utumiaji wa pombe uliopitiliza
v. Utumiaji wa madawa ya kulevya nk

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
~Dalili za vidonda vya tumbo ni nyingi ila sio wote wanaopata Dalili hizi Wana vidonda vya tumbo
i. maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (EPIGASTIC PAINS)
ii. kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi Hali hii huweza kuendana na kucheua na kujamba Mara kwa Mara
ii. kutapika damu
iii. mtu mwenye vidonda vya tumbo (gastric ULCERS) hupata maumivu makali pindi anapokula au amalizapo kula
iv. mtu mwenye vidonda vya tumbo katika utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali pindi anapokua na njaa.
v. kupoteza hamu ya kula
vi. kupata haja kubwa yenye rangi damu Tena chenye harufu mbaya
vii. kupungua uzito

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
~matibabu ya ugonjwa huu yanapatikana vizuri nchini mwetu ila tatzo ni tiba yenyew kutokua na wataalamu wa kutosha wa kutibu chanzo cha tatizo na kumaliza tatizo pasipo kuleta matatzo mengine kutokana na matibabu yenyewe kuhusisha mfumo wa dawa za kemikal ambazo zina madhara kwa mhusika na pia , hivyo tiba bora kwa vidonda vya tumbo ni mlo kamili na dawa zisizo na kemikal pia tunapaswa kuepuka baadhi ya vyakula na kuzingatia masharti.

MAMBO YA KUFANYA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
i. epuka kula vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau
ii. epuka kutumia pombe
iii. epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
iv. kula Chakula kidogo kwa muda maalum
v. kula vyakula vyenye fiber yan vyakula vyenye nyuzunyuzi ambavyo ni jamii ya mbogamboga na matunda
vi. epuka unywaji wa kahawa au kinywaji chochote chenye caffeine kiepuke

BAADHI YA USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
VIDONDA vya tumbo ni mojawapo ya ishara za mwili kuanza kuishiwa maji, ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha ndani ya tumbo.

Kwanini vidonda vya tumbo ni ishara ya mwili kuishiwa maji?

Asilimia 94 ya damu ni maji, ubongo wetu una zaidi ya asilimia 85 za maji, na tishu zetu laini zina asilimia 75 ya maji.Tunatumia maji kupumua nje, kila masaa 24 tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu nje.

Kwa sehemu kubwa miili yetu huishiwa maji kutokana na sisi kusubiri kiu ndipo tunywe maji. Ndiyo, haupaswi kusubiri kiu ndipo unywe maji, kiu ni ishara iliyochelewa ya mwili kuhitaji maji.

Akili ya kawaida inaniambia nikiwa na bustani ya mboga mboga au hata maua nitakuwa nikiimwagilia maji mapema asubuhi au jioni wakati jua tayari limezama na si mchana wakati wa jua kali, kadharika maji yakiisha ghafla kwenye injini ya gari ndani ya mwendo mrefu siwezi nikashuka tu kwenye gari na kuongeza maji kwenye injini!, ni lazima nisubiri injini ya gari ipowe ndipo niongeze maji mengine.

Tuendelee na vidonda vya tumbo …

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen. Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi kama juisi ya limau, juisi ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.

Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja katika kila watu wanne anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Dalili za vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni kuchoka choka sana bila sababu maalum, kuuma mgongo au kiuno, kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia, kizunguzungu, kukosa usingizi, usingizi wa mara kwa mara. Maumivu makali sehemu ya mwili, kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali. Dalili zingine ni kichefuchefu, kiungulia, tumbo kujaa gesi, tumbo kuwaka moto, maumivu makali sehemu kilipo kidonda, kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi.

Kutapika nyongo, kutapika damu au kuharisha, sehemu za mwili kupata ganzi n.k. Pia dalili zingine ni kukosa hamu ya kula, kula kupita kiasi, kusahahu sahau na hasira. Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?

Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na kama matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline. Vinaweza pia kuletwa na bakteria ajulikanaye kama H.Pyroli.

Vitu vifuatavyo vinahusika katika kuleta vidonda vya tumbo mwilini:

1. Asidi iliyozidi mwilini:

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.

Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.

Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili. Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, n.k.

2. Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha:

Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.

Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo kama matokeo ya mfadhaiko na hakuna chakula cha kufanyiwa kazi au kumeng’enywa humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !

Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.

Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili au mawazo yatokanayo na shida za maisha.

Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, watu waliopewa talaka na wale wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.

Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui. Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya mapigano au makabiliano na adui.

Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe tayari zaidi kwa mapigano, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni inayohusika na uzalishwaji wa nguvu mwilini huongezeka.

Kadiri mfadhaiko unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake zinavyokuwa ni fupi. Lakini pindi mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo mengi kila mara, athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.

Dalili za mtu mwenye mfadhaiko

Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko. Dalili hizo ni:

1. Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote,
2. kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi,
3. kupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa
4. Kupoteza hamu ya chakula
5. Kukosa usingizi
6. Wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia kwa ujumla
7. Kupoteza kumbukumbu au hali ya kusahausahau na kushindwa kuamua
8. Kughadhibishwa na vitu vidogo, yaani mtu kitu kidogo tu ameshachukia
9. Kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.

3. Sababu ya tatu inayosababisha vidonda vya tumbo ni Haraka haraka

Maisha ya kisasa yanataka haraka katika kazi nyingi tuzifanyazo kila siku, ni lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba katika shughuli zako za kila siku pia husababisha matumbo nayo kubanana.

Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: “Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, au nasikia kiungulia baada ya kula”. Haraka haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.

Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani. Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu.

Ili kuepuka kufanya kazi zako kwa hali ya uharakaharaka unashauriwa kupanga kabla ni kazi gani na gani utaenda kuzifanya siku inayofuatia kwa kuziandika kabisa katika karatasi au kitabu maalumu kiitwacho kiingereza diary au kumbukumbu za kila siku kwa Kiswahili na mhimu ni uwe na kiasi kwa kila jambo kwani si lazima umalize kazi zote leo.

4. Sababu ya nne ya kutokea vidonda vya tumbo ni ulaji wa Vyakula vya kusisimua

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile ketchup, chill sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni. Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo.

5. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi

Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni. Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

MAMBO YA MHIMU YA KUZINGATIA ILI UPONE VIDONDA VYA TUMBO:

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu. Pia unashauriwa kufanya yafuatayo katika kujitibu au kujikinga na vidonda vya tumbo:

Moja; Punguza haidrokloriki asidi:

Kama tulivyoona kule mwanzoni kuwa moja ya sababu ya kutokea kwa vidonda vya tumbo mwilini ni uzarishwaji wa haidrokloriki asidi ambayo huzalishwa tumboni dakika chache kabla hujaanza kula chakula ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. HAIDROKLORIKI ASIDI hii ni lazima ipunguzwe makali (must be neutralized) kabla hujameza chakula.

INAPUNGUZWAJE MAKALI? kwa kunywa maji kikombe kimoja au viwili nusu saa kabla ya kula chakula. Kwahiyo kama umepanga kuwa saa saba kamili mchana ndiyo utakula chakula cha mchana, basi saa sita na nusu unywe maji vikombe viwili. Kwa kufanya hivi kila mara kabla ya kula basi hakuna vidonda vya tumbo utakavyovipata kama matokeo ya hii haidrokloriki asidi.

Mbili; Pata usingizi wa kutosha:

Ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Haraka na pilikapilika za dunia yetu ya kisasa hazina mfano. Mvurugiko wa mawazo kutokana na mwenendo wa maisha uko kila mahali. Kutokana na mahitaji ya maisha, kuna idadi kubwa ya watu ambao neva zao hazitulii.

Kulala ni moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo, udhaifu na uchovu.

Kukesha usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na akili.

Madaktari wetu wanasema kuwa, kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili.

Sehemu ya kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na asilia. Hewa asilia ina athari nzuri katika mwili wa mwanadamu, miongoni mwa athari zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya kula.

Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri. Katika umri wa miaka miwili, mtu hushauriwa kulala masaa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne masaa 12 hadi 14 kwa siku, miaka sita hadi minane masaa 11 hadi 12 kwa siku, miaka minane hadi 11 masaa 10 hadi 11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 masaa 8 hadi 9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya sita na nane kwa siku.

Tatu; Dhibiti mfadhaiko:

Mbinu ya tatu katika kujikinga na kujitibu vidonda vya tumbo ni kujitahidi kwa kila namna kudhibiti mfadhaiko. Tambuwa kuwa kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kusababisha maradhi kama vidonda vya tumbo, maradhi ya moyo, n.k.

Mfadhaiko unaweza kuwa wa muda au wa kudumu. Matokeo yake yana madhara makubwa kama hautadhibitiwa. Ni vipi unaweza kudhibiti mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha? Unachotakiwa kufanya ili kujidhibiti na mfadhaiko wa namna hii ni kuridhika na maisha.

Kama utakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, ukaacha kuyakopa maisha ya jana na ukaacha kuhofu maisha ya kesho, ni hakika kabisa tumbo lako pia litatulia.

Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara wote duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.

Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo chanya katika mwili, pia wasiwasi na hofu ya maisha huweza kuleta magonjwa yanayoweza kuuwa kabisa sawa sawa kama inavyotokea pia kwa magonjwa yale yatokanayo na lishe dhaifu. Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.

Nne; Punguza au acha kabisa vinywaji na vyakula vifuatavyo:

Chai ya rangi, kahawa, pombe, soda, juisi za viwandani, sigara na tumbaku zote mpaka hapo utakapopona. Kama wewe ni mpenzi wa kunywa chai asubuhi au jioni basi sijasema usinywe chai, bali unachotakiwa kufanya ni kuchemsha maji yako ya chai na uiunge na ama tangawizi, mdalasini, au mchaimchai na uendelee na chai yako, kinachoepukwa hapa ni yale majani meusi ya chai ambayo ndani yake huwa na kaffeina na asidi nyingi na hivyo kuwa chanzo cha vidonda vya tumbo. Lakini pia tambuwa kuwa tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini, hivyo unapokunywa chai ya tangawizi faida nyingine unayopata zaidi ya kuondoa njaa au kushiba ni dawa iliyomo ndani yake, hivyo unashiba huku unajitibu, unaionaje hii siyo imetulia?.

DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU VIDONDA VYA TUMBO:

Chagua dawa 3 kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri haraka zaidi. Sasa usinywe zote wakati mmoja, moja tumia asubuhi, nyingine mchana na nyingine jioni. Kumbuka usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari.

1. UNGA WA MAJANI YA MLONGE

Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.

Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo.

2. KABEJI

Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.

*Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.

*Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.

*Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.

3. NDIZI

Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.

Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.

Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.

Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.

4. NAZI

Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.

Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.

Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.

5. UWATU

Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika kama utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.

Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.

Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.

Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.

Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa kama vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.

6. ASALI MBICHI

Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kama ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.

Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

7. KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu kinaweza kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini pia kudhiti bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye kama Helicobacter Pylori (H. pylori).

Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 1 kwa wiki 2 au 3

8. MKAA WA KIFUU CHA NAZI

Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya nazi. Chukua vifuu vya nazi vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.

9. MAFUTA YA HABBAT SODA

Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja kwa moja. Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu aina zote za vidonda vya tumbo!

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hadi siku 60 hasa habbat soda grade 1. Vidonda vya tumbo pia upate unga wa asili wa majani ya mlonge na mbegu za maboga kwa matokeo mazuri na ya uhakika, kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.

Umewahi kuwa na vidonda vya tumbo kabla na ukapona? tusaidie ni dawa gani ulitumia ili tusaidie na wengine wanaoendelea kuteseka bila sababu.
View attachment 501064
---
Kabeji
Kunywa juisi ya kabeji mbichi baada ya kuikatakata vipande kisha isage kwenye mashine ya kutengenezea juisi (Blender). Baada ya hapo pima kwenye kikombe kimoja cha chai na unywe mara nne kwa siku. Tiba hii inaweza kutibu tatizo la vidonda vya tumbo kwa muda wa siku kumi. Kumbuka kuzingatia masharti ya msingi yaliyoainishwa hapo juu.

Asali
Asali ina chembechembe za asili zenye kuua bacteria na virusi ambazo vina uwezo wa kuua helicobacter Pylory ambao ni wadudu wanaosabisha ugonjwa huu kitu kinachomaanisha kuwa ina uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo. Kingine ni kwamba asali huweza kulainisha umio, mfuko wa chakula na utumbo hivyo huweza kufunika vidonda vilivyopo tumboni. Kutokana na kufunika vidonda maumivu ya kuchoma pamoja na dalili nyingine za vidonda vya tumbo hupungua.
Asali pia huweza kusafisha uvimbe na kusafisha vidonda ambavyo hujitokeza kwenye njia ya chakula. Asali inayopaswa kutumika kwa kusudio hili inapaswa iwe mbichi na isiwe imeongezewa vitu vingine na dozi yake ni vijiko vya chakula viwili mpaka vitatu kwa siku.

Vitunguu Swaumu
Viungo hivi ni tiba nyingine inayofaa sana katika kutibu vidonda vya tumbo kutokana na kemikali zinazoua wadudu pamoja na virusi zilizomo ndani yake na hivyo huweza kupambana na kuua bacteria wanaosababisha vidonda vya tumbo.
Viungo hivi hufahamika kwa kusaidia katika kutibu vidonda vya tumbo hata pale vinapotumika vikiwa vimechanganywa na vyakula vingine kutokana na nguvu nyingi iliyomo ndani yake pamoja na chembechembe zenye kuamsha na kuboresha mwili zilizomo ndani yake ambazo huwezesha kuukinga mwili dhidi ya maambukizi kama vile vidonda vya tumbo.

Hivi ndivyo unavyopaswa kutumia vitunguu swaumu kwa ajili ya kutibu tatizo hili:
Kula punje tatu mpaka nne za kiungo hicho kwa siku zikiwa zimechanganywa na kijiko kimoja au viwili vya asali kwa siku.
---
Mkuu, pole sana kwa changamoto uliyonayo. Usikate tamaa utapona tu.
Kwa ushauri, naomba tuanzie hapa kwenye vyakula. Kama ikiwezekana;

1. Epuka kabisa vyakula vyenye asili ya asidi kama matunda uliyoyataja hapo juu (maembe, mananasi, machungwa, machenza, ndizi mbivu nk pia epuka ndimu, pilipili, nyanya na kachumbari yake nk ) tumia matango kwa wingi na matikiti kwani yana asili ya alkali ambayo husaidia kupunguza asidi tumboni.

2. Epuka kula vyakula kama pilau, Chipsi na viazi kwa ujumla, dagaa, nyama za kukaanga, vyakula vyenye mafuta mengi (tumia mafuta wastani kwenye chakula) nyama choma, mkate na bait zote zenye hamira, maandazi, maharage, nk.

3. Epuka kunywa vinywaji vyote vyenye gesi, mfano soda - hii weka mbali kabisa, pombe zote, juice zote zenye uchachu, maziwa mgando nk.

4. Pia epuka kula na kushiba sana, kula kidogo kidogo mara nyingi. Kakikisha muda wako wa kula unajulikana na hauchanganyi ratiba ya muda wa kula. Ukiamka asubuhi, kunywa maji ya uvuguvugu walao glasi moja ama kikombe cha robo lita (hii iwe ni sehemu ya maisha yako mapya kama huwa hufanyi hivyo)

5. Epuka baadhi ya vidonge vya maumivu kwani huchangia kuumiza tumbo, utauliza vizuri kuhusu hili kwa madaktari ama wazoefu wengine.

6. Epuka hizo hasira kwani nayo inaongeza madhara kwa sababu unapokasirika kuna hali hutokea tumboni inayotokana na nyongo kumwagika na kuendelea kuunguza utumbo.

7. Sehemu kubwa ya mlo wako viwe ni vyakula vya mchemsho, kama ni supu isiwe na mafuta mengi na usiweke ndimu, wanasema limao ni zuri kwa sababu ni alkali ila kwa hali ya sasa usitumie kwanza.

8. Usile chakula chochote kilichoungua, epuka vitu vya kukaangwa kaangwa.

9. Epuka vyakula vyote vyenye nyanya, hakikisha nyanya sio sehemu ya milo yako kwa kipindi hiki

Wakati unatafuta tiba angalia yafuatayo;

1. Tafuta asali mbichi - ukipata ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi. Utumie kijiko kimoja kikubwa kila asubuhi na jioni. Ukipata mayai ya kienyeji pase, changanya yai bichi na asali kidogo kisha koroga na hakikisha vimechanganyikana, kisha unywe huo mchanganyiko, inasaidia sana tumbo.

2. Tumia mbogamboga kwa wingi, tafuta brokoli, zukini na vinginevyo kama kabichi, jifunze kuandaa bila kukaanga kisha kula na chakula kingine. kama ni wali ama ugali tumia kidogo kwa kipindi hiki kwani navyo huumiza hilo tumbo.

3. Kunywa maji ya kutosha kila siku - angalia pia kuna baadhi ya maji ya kunywa PH scale yake sio nzuri, PH ianzie 7.0 na sio chini ya hapon kama ni maji ya kununua.

4. Ndizi bukoba za kupika ukipata ndio ndizi za kula na si nyinginezo.

Kwenye tiba, tafuta tiba ya hao H.Pilori, vipimo vinaonesha wako wengi. Sijui wewe uko wapi maana kama uko Dar nenda pale Burhani, muone dokta Sidika asubuhi mpaka saa saba, aliwahi nipa dawa ya hao bacteria ikanisaidia.

Kwa sasa naomba tuanzie hapo. nikipata ndondo nyingine nitajitahidi kukuvunjia. ila pole sana Ambition plus.
---
Nitakujibu na ukifata ushauri huu utapona kabisa within 2 moths.
Kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako unaweza kuwa na leaky gut na hii imepelekea SIBO (Small intestine bacterial overgrowth).

Leaky gut kwa maelezo rahisi ni kwamba chekecheke la utumbo wako ambamo ufyonzaji wa viini lishe hufanyika limelegea na hivo kuruusu vitu visivyotakiwa kupenya vipenye, incluiding harmful bacteria.
Changamoto ikiwa ya muda mrefu hupelekea imbalance ya microbiome tumboni.
Microbiome kwa luga rahisi ni kwamba tumboni kuna bacteria wazuri na wabaya, bakteria wazuri ni kinga na pia wanaahusika katika digestion, imbalance yetu tunaongelea ni kwamba bakteria wabaya kuwa wengi kuliko bakteria wazuri.

Sasa unapotaka kusolve swala la leaky gut inabidi uwe strict sana kwenye swala la lishe:

1.ONDOA vyakula vyote ambayo vinaharibu gut(mfumo wa chakula), vitu hivi ni kama vyakula vilivyosindikwa+vinywaji, vyakula vya ngano,antibiotics, vionjo mbalimbali vya kiwandani, mafuta yaliyosafishwa ie margarine.

2. RUDISHA vyakula vya kuimarisha mfumo wa chakula.Vyakula hivi ni kama ifuatavyo:
  • Supu ya mifupa ( bone broth) kama unaweza kuotengeneza ama ukapata mahali wanaipika.
  • Maziwa mtindi ya asili. Achana na yale ya kwenye pakiti. Maziwa mtindi tunasema yana probiotics ( probiotics ni viumbe wadogo ambao wana uwezo wa kutibu mfumo wako wa chakula). Maziwa yanapoferment yanatengeneza live becteria ambao ni wazuri kwa gut yako.
  • Mboga za majani, zipikwe kidogo sana . Ama ukiweza tengeneza juisi ya mbogamboga hii itaharakisha mchakato wa kupona. Juisi ya mboga inapromote good bacteria growth.
  • Bidhaa za nazi. Mfano mafuta ya kupikia ya nazi ( haya yatumie kama kiungo chako). Mafuta ya nazi tunasema yana aina ya fat ambazo tunaita ni medium chain fatty acid ambazo ni rahisi kuchakatwa (digested) ukilinganisha na mafuta mengine, ukikosa mafuta ya nazi basi pikia mafuta ya olive.
  • Vyakula vyenye mafuta mazuri kama: parachichi,mbegu za maboga , mayai nk. Vitasaidia kuharakisha uponaji wa gut yako.

Anza kufatilia then utanipa majibu.

NB: mimi siyo daktari kwahiyo kuna mahali naweza kuwa nimekosea, wale vipanga mnaruusiwa kunisahihisha.
---
a
REVITAL HEALTH CARE
ULCER TREATMENT

Get raw pawpaw and wash it. It must be raw, not ripe
Do not peel it and do not remove the seeds.

After washing the outside neatly, slice it without peeling it into small small pieces. The cutting should be small like sugar cubes.

Put all the small pieces of the raw pawpaw into any clean container.

Fill the container with water to stop at the same point the sliced pawpaw stopped.
Leave the pawpaw in the water for four days. For example if u soak it on a Monday, count Tuesday, Wednesday, Thursday and Friday will be the fourth day.

On the Fourth day, the water will be looking white in colour. Seive it and throw away the pawpaw and the water becomes your cure for ulcer.

DOSAGE: drink half a glass of the pawpaw water every morning, afternoon and evening. You will no longer feel those ulcer pains because it will heal the wounds inside that are causing the pain.

This morning, afternoon and evening drinking of the pawpaw water can continue for weeks and months depending on how severe the ulcer is. It is not relief. It is a cure.

Additional note: an ulcer is an internal wound usually in the stomach or intestines.

Common causes of ulcer are infection with the bacterium Helicobacter pylori (H. pylori) and long-term use of aspirin and certain other painkillers, such as ibuprofen (Advil, Motrin, others) and naproxen sodium (Aleve, Anaprox, others). Stress and spicy foods do not cause peptic ulcers. However, they can make your symptoms worse.

Pls avoid taking strong pain killers without prescription. If you take time to read the side effects you will see that the drugs for pain relief cause ulcer or wounds in the body.

This treatment mentioned is not a reason not to go to hospital, because not all internal pains are ulcers.
Let someone know and help someone get cured today.
---
Vidonda vya tumbo vilinisumbua sana toka mwaka nikiwa na miaka 14 kiasi kwamba nilikata tamaa kabisa ya kupona na nilitumia dawa nyingi sana lakini wapi kuna dawa madukani zinaitwa omeplazone kama sikosei nazo zilikua zinatuliza tu mpaka mwaka 2014 ndio nilipata dawa kutoka kwa mama mdogo rafiki yangu anaitwa Rama.

Yenyewe niyakienyeji kama magome ya mti yanatwangwa zen unga wake unachanganya kwenye uji wowote ule alinipa kidogo sana nilitumia siku tatu ilisha nikawa nakunywa maji ila nikawa bado situmii maharage,pilipili,soda nikawa nahofia kuchokoza tumbo mpka mwaka 2015 January ndio niligundua nimepona kabisa nakumbuka.

Siku Ile nilikula maharage tumbo alikuniuma asubuh yake nikala tena ikawa safi tu mpka nimeenda kusoma advance sikuwahi kuumwa tena mpka leo ilishabaki story, mwaka jana nilifanya uchunguzi na kufanikiwa kuipata na kujua kwamba inapatika kigoma uko na nimewapatia watu wa kalibu waliokua wanasumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa malipo kidogo kwa bahati nzuri nao wamepona kama upo mbeya naweza kukusaidia maana ninayo imebaki kidogo.
---
Mkuu, pole sana kwa changamoto uliyonayo. Usikate tamaa utapona tu.
Kwa ushauri, naomba tuanzie hapa kwenye vyakula. Kama ikiwezekana;

1. Epuka kabisa vyakula vyenye asili ya asidi kama matunda uliyoyataja hapo juu (maembe, mananasi, machungwa, machenza, ndizi mbivu nk pia epuka ndimu, pilipili, nyanya na kachumbari yake nk ) tumia matango kwa wingi na matikiti kwani yana asili ya alkali ambayo husaidia kupunguza asidi tumboni.

2. Epuka kula vyakula kama pilau, Chipsi na viazi kwa ujumla, dagaa, nyama za kukaanga, vyakula vyenye mafuta mengi (tumia mafuta wastani kwenye chakula) nyama choma, mkate na bait zote zenye hamira, maandazi, maharage, nk.

3. Epuka kunywa vinywaji vyote vyenye gesi, mfano soda - hii weka mbali kabisa, pombe zote, juice zote zenye uchachu, maziwa mgando nk.

4. Pia epuka kula na kushiba sana, kula kidogo kidogo mara nyingi. Kakikisha muda wako wa kula unajulikana na hauchanganyi ratiba ya muda wa kula. Ukiamka asubuhi, kunywa maji ya uvuguvugu walao glasi moja ama kikombe cha robo lita (hii iwe ni sehemu ya maisha yako mapya kama huwa hufanyi hivyo)

5. Epuka baadhi ya vidonge vya maumivu kwani huchangia kuumiza tumbo, utauliza vizuri kuhusu hili kwa madaktari ama wazoefu wengine.

6. Epuka hizo hasira kwani nayo inaongeza madhara kwa sababu unapokasirika kuna hali hutokea tumboni inayotokana na nyongo kumwagika na kuendelea kuunguza utumbo.

7. Sehemu kubwa ya mlo wako viwe ni vyakula vya mchemsho, kama ni supu isiwe na mafuta mengi na usiweke ndimu, wanasema limao ni zuri kwa sababu ni alkali ila kwa hali ya sasa usitumie kwanza.

8. Usile chakula chochote kilichoungua, epuka vitu vya kukaangwa kaangwa.

9. Epuka vyakula vyote vyenye nyanya, hakikisha nyanya sio sehemu ya milo yako kwa kipindi hiki

Wakati unatafuta tiba angalia yafuatayo;

1. Tafuta asali mbichi - ukipata ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi. Utumie kijiko kimoja kikubwa kila asubuhi na jioni. Ukipata mayai ya kienyeji pase, changanya yai bichi na asali kidogo kisha koroga na hakikisha vimechanganyikana, kisha unywe huo mchanganyiko, inasaidia sana tumbo.

2. Tumia mbogamboga kwa wingi, tafuta brokoli, zukini na vinginevyo kama kabichi, jifunze kuandaa bila kukaanga kisha kula na chakula kingine. kama ni wali ama ugali tumia kidogo kwa kipindi hiki kwani navyo huumiza hilo tumbo.

3. Kunywa maji ya kutosha kila siku - angalia pia kuna baadhi ya maji ya kunywa PH scale yake sio nzuri, PH ianzie 7.0 na sio chini ya hapon kama ni maji ya kununua.

4. Ndizi bukoba za kupika ukipata ndio ndizi za kula na si nyinginezo.

Kwenye tiba, tafuta tiba ya hao H.Pilori, vipimo vinaonesha wako wengi. Sijui wewe uko wapi maana kama uko Dar nenda pale Burhani, muone dokta Sidika asubuhi mpaka saa saba, aliwahi nipa dawa ya hao bacteria ikanisaidia.

Kwa sasa naomba tuanzie hapo. nikipata ndondo nyingine nitajitahidi kukuvunjia. ila pole sana Ambition plus.
---
i. Matango
Tengeneza juisi ya matango na kunywa kila kwenye mlo wako.
ii. Karela na mtindi
Majani ya karela 15 g
Mtindi glasi 1
Pondaponda majani ya karela, changanya na mtindi.
Matumizi:
Glasi 1 kila siku kwa muda wa mwezi 1.
iii. Bilinganya.
Katakata bilinganya vipande vidogo vidogo, chemsha na tia chumvi kidogo.
Matumizi:
Kula mara 2 kila siku kwa muda wa mwezi 1.
iv. Kabichi.
Kabichi ½ kilo
Maji ½ lita
Katakata kabichi vipande vidogovidogo, tia maji na chemsha hadi maji yawe ¼ lita tu.
Matumizi:
Kunywa maji yote baada ya kupoa, mara 2 kila siku kwa mwezi 1.
v. Ndizi.
Ndizi 2 za kupika na maziwa glasi 1 mara 4 kama chakula pekee kwa muda wa siku 14.

KUMBUKA:
Kabichi lina kemikali inayosaidia kuondoa vidonda vya tumbo
​ Asali na mdalasini inatibu maumivu ya tumbo pia hutibu vidonda vya tumbo kwenye shina la vidonda
---
VIDONDA vya tumbo ni mojawapo ya ishara za mwili kuanza kuishiwa maji, ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha ndani ya tumbo.

Kwanini vidonda vya tumbo ni ishara ya mwili kuishiwa maji?

Asilimia 94 ya damu ni maji, ubongo wetu una zaidi ya asilimia 85 za maji, na tishu zetu laini zina asilimia 75 ya maji.Tunatumia maji kupumua nje, kila masaa 24 tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu nje.

Kwa sehemu kubwa miili yetu huishiwa maji kutokana na sisi kusubiri kiu ndipo tunywe maji. Ndiyo, haupaswi kusubiri kiu ndipo unywe maji, kiu ni ishara iliyochelewa ya mwili kuhitaji maji.

Akili ya kawaida inaniambia nikiwa na bustani ya mboga mboga au hata maua nitakuwa nikiimwagilia maji mapema asubuhi au jioni wakati jua tayari limezama na si mchana wakati wa jua kali, kadharika maji yakiisha ghafla kwenye injini ya gari ndani ya mwendo mrefu siwezi nikashuka tu kwenye gari na kuongeza maji kwenye injini!, ni lazima nisubiri injini ya gari ipowe ndipo niongeze maji mengine.

Tuendelee na vidonda vya tumbo …

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen. Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi kama juisi ya limau, juisi ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.

Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja katika kila watu wanne anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Dalili za vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni kuchoka choka sana bila sababu maalum, kuuma mgongo au kiuno, kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia, kizunguzungu, kukosa usingizi, usingizi wa mara kwa mara. Maumivu makali sehemu ya mwili, kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali. Dalili zingine ni kichefuchefu, kiungulia, tumbo kujaa gesi, tumbo kuwaka moto, maumivu makali sehemu kilipo kidonda, kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi.

Kutapika nyongo, kutapika damu au kuharisha, sehemu za mwili kupata ganzi n.k. Pia dalili zingine ni kukosa hamu ya kula, kula kupita kiasi, kusahahu sahau na hasira. Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?

Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na kama matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline. Vinaweza pia kuletwa na bakteria ajulikanaye kama H.Pyroli.

Vitu vifuatavyo vinahusika katika kuleta vidonda vya tumbo mwilini:

1. Asidi iliyozidi mwilini:

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.

Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.

Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili. Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa, baadhi ya dawa tunazotumia kujitibu maradhi mbalimbali mwilini, n.k.

2. Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha:

Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.

Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo kama matokeo ya mfadhaiko na hakuna chakula cha kufanyiwa kazi au kumeng’enywa humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia sehemu kubwa ya nguvu ya mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !

Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.

Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili au mawazo yatokanayo na shida za maisha.

Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, watu waliopewa talaka na wale wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.

Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui. Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya mapigano au makabiliano na adui.

Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe tayari zaidi kwa mapigano, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni inayohusika na uzalishwaji wa nguvu mwilini huongezeka.

Kadiri mfadhaiko unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake zinavyokuwa ni fupi. Lakini pindi mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo mengi kila mara, athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.

Dalili za mtu mwenye mfadhaiko

Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko. Dalili hizo ni:

1. Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote,
2. kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi,
3. kupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa
4. Kupoteza hamu ya chakula
5. Kukosa usingizi
6. Wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia kwa ujumla
7. Kupoteza kumbukumbu au hali ya kusahausahau na kushindwa kuamua
8. Kughadhibishwa na vitu vidogo, yaani mtu kitu kidogo tu ameshachukia
9. Kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.

3. Sababu ya tatu inayosababisha vidonda vya tumbo ni Haraka haraka

Maisha ya kisasa yanataka haraka katika kazi nyingi tuzifanyazo kila siku, ni lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba katika shughuli zako za kila siku pia husababisha matumbo nayo kubanana.

Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: “Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, au nasikia kiungulia baada ya kula”. Haraka haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.

Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani. Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu.

Ili kuepuka kufanya kazi zako kwa hali ya uharakaharaka unashauriwa kupanga kabla ni kazi gani na gani utaenda kuzifanya siku inayofuatia kwa kuziandika kabisa katika karatasi au kitabu maalumu kiitwacho kiingereza diary au kumbukumbu za kila siku kwa Kiswahili na mhimu ni uwe na kiasi kwa kila jambo kwani si lazima umalize kazi zote leo.

4. Sababu ya nne ya kutokea vidonda vya tumbo ni ulaji wa Vyakula vya kusisimua

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile ketchup, chill sauce, achali, pilipili na vingine vingi vya jamii hii huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni. Sababu ni kuwa, visisimuaji hivi huzichoma pia kuta za tumbo.

5. Vinywaji na vyakula vyenye kaffeina na asidi nyingi

Vinywaji vyenye kaffeina na asidi nyingi kama vile chai ya rangi, kahawa, soya sauce, mayonnaise, jibini, Vyakula jamii ya Mkate, samaki wa kwenye makopo, pombe, soda na juisi za viwandani pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni. Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

MAMBO YA MHIMU YA KUZINGATIA ILI UPONE VIDONDA VYA TUMBO:

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu. Pia unashauriwa kufanya yafuatayo katika kujitibu au kujikinga na vidonda vya tumbo:

Moja; Punguza haidrokloriki asidi:

Kama tulivyoona kule mwanzoni kuwa moja ya sababu ya kutokea kwa vidonda vya tumbo mwilini ni uzarishwaji wa haidrokloriki asidi ambayo huzalishwa tumboni dakika chache kabla hujaanza kula chakula ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. HAIDROKLORIKI ASIDI hii ni lazima ipunguzwe makali (must be neutralized) kabla hujameza chakula.

INAPUNGUZWAJE MAKALI? kwa kunywa maji kikombe kimoja au viwili nusu saa kabla ya kula chakula. Kwahiyo kama umepanga kuwa saa saba kamili mchana ndiyo utakula chakula cha mchana, basi saa sita na nusu unywe maji vikombe viwili. Kwa kufanya hivi kila mara kabla ya kula basi hakuna vidonda vya tumbo utakavyovipata kama matokeo ya hii haidrokloriki asidi.

Mbili; Pata usingizi wa kutosha:

Ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Haraka na pilikapilika za dunia yetu ya kisasa hazina mfano. Mvurugiko wa mawazo kutokana na mwenendo wa maisha uko kila mahali. Kutokana na mahitaji ya maisha, kuna idadi kubwa ya watu ambao neva zao hazitulii.

Kulala ni moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo, udhaifu na uchovu.

Kukesha usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na akili.

Madaktari wetu wanasema kuwa, kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili.

Sehemu ya kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na asilia. Hewa asilia ina athari nzuri katika mwili wa mwanadamu, miongoni mwa athari zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya kula.

Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri. Katika umri wa miaka miwili, mtu hushauriwa kulala masaa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne masaa 12 hadi 14 kwa siku, miaka sita hadi minane masaa 11 hadi 12 kwa siku, miaka minane hadi 11 masaa 10 hadi 11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 masaa 8 hadi 9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya sita na nane kwa siku.

Tatu; Dhibiti mfadhaiko:

Mbinu ya tatu katika kujikinga na kujitibu vidonda vya tumbo ni kujitahidi kwa kila namna kudhibiti mfadhaiko. Tambuwa kuwa kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kusababisha maradhi kama vidonda vya tumbo, maradhi ya moyo, n.k.

Mfadhaiko unaweza kuwa wa muda au wa kudumu. Matokeo yake yana madhara makubwa kama hautadhibitiwa. Ni vipi unaweza kudhibiti mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha? Unachotakiwa kufanya ili kujidhibiti na mfadhaiko wa namna hii ni kuridhika na maisha.

Kama utakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, ukaacha kuyakopa maisha ya jana na ukaacha kuhofu maisha ya kesho, ni hakika kabisa tumbo lako pia litatulia.

Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara wote duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.

Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo chanya katika mwili, pia wasiwasi na hofu ya maisha huweza kuleta magonjwa yanayoweza kuuwa kabisa sawa sawa kama inavyotokea pia kwa magonjwa yale yatokanayo na lishe dhaifu. Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.

Nne; Punguza au acha kabisa vinywaji na vyakula vifuatavyo:

Chai ya rangi, kahawa, pombe, soda, juisi za viwandani, sigara na tumbaku zote mpaka hapo utakapopona. Kama wewe ni mpenzi wa kunywa chai asubuhi au jioni basi sijasema usinywe chai, bali unachotakiwa kufanya ni kuchemsha maji yako ya chai na uiunge na ama tangawizi, mdalasini, au mchaimchai na uendelee na chai yako, kinachoepukwa hapa ni yale majani meusi ya chai ambayo ndani yake huwa na kaffeina na asidi nyingi na hivyo kuwa chanzo cha vidonda vya tumbo. Lakini pia tambuwa kuwa tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini, hivyo unapokunywa chai ya tangawizi faida nyingine unayopata zaidi ya kuondoa njaa au kushiba ni dawa iliyomo ndani yake, hivyo unashiba huku unajitibu, unaionaje hii siyo imetulia?.

DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU VIDONDA VYA TUMBO:

Chagua dawa 3 kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri haraka zaidi. Sasa usinywe zote wakati mmoja, moja tumia asubuhi, nyingine mchana na nyingine jioni. Kumbuka usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari.

1. UNGA WA MAJANI YA MLONGE

Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.

Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo.

2. KABEJI

Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.

*Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.

*Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.

*Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.

3. NDIZI

Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.

Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.

Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.

Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.

4. NAZI

Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.

Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.

Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.

5. UWATU

Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika kama utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.

Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.

Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.

Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.

Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa kama vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.

6. ASALI MBICHI

Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kama ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.

Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

7. KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu kinaweza kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini pia kudhiti bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye kama Helicobacter Pylori (H. pylori).

Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 1 kwa wiki 2 au 3

8. MKAA WA KIFUU CHA NAZI

Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya nazi. Chukua vifuu vya nazi vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.

9. MAFUTA YA HABBAT SODA

Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja kwa moja. Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu aina zote za vidonda vya tumbo!

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hadi siku 60 hasa habbat soda grade 1. Vidonda vya tumbo pia upate unga wa asili wa majani ya mlonge na mbegu za maboga kwa matokeo mazuri na ya uhakika, kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.

Umewahi kuwa na vidonda vya tumbo kabla na ukapona? tusaidie ni dawa gani ulitumia ili tusaidie na wengine wanaoendelea kuteseka bila sababu.
View attachment 501064
---
Wana jf Leo naomba ni share na nyie tiba ambayo binafsi nliifata na kujiponya vidonda vya tumbo

Kwanza baada ya hali kuanza kuwa mbaya kukosa hamu ya kula na wakati huo na njaa kali au kula na ukimaliza hapo hapo tumbo la kuharisha linakupata, kiukweli vinatesa kwa wale wenye tatizo hili nadhani lugha ninayoongea mnaielewa vizuri.

Leo naomba niwaeleze wahanga wenzangu (kama mpo) jinsi me nlivopona.
  1. Nimetumia tiba asili kujitibia hadi kupona nlianza kwa kutumia kabeji kwa kuisaga kiasi fulan na kutoa juice yake nikatumia juice hiyo kwa mfululizo wa wiki mbili hali ilibadilika sana na nikaanza kurudi hali yangu ya zamani
  2. Pili baada ya kumaliza dozi nilielezwa nianze kutumia asali ya mdalasini ambayo kiukweli pia imensaidia sana na namshukuru Mungu nimepona kabisa na naamini havitarudi.
Kama na wewe unashida hii nakusihi wahi matibabu yake ni kama hayo ne rahisi pia ni nafuu

Asante

Pia unashauriwa kusoma:
1. Ushauri kuhusu dalili hatarishi za vidonda vya tumbo - JamiiForums

2. naomba kujua dawa asili ya Vidonda vya tumbo - JamiiForums

3. Yajue haya majani ni Dawa ya vidonda vya tumbo - JamiiForums

4. Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

5. Angalizo: Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo hufanana na dalili za magonjwa ya moyo - JamiiForums

6. Vyakula Vinavyoliwa na Mgonjwa wa Vidonda Vya Tumbo
 
Mwambie apunguze mawazo na awe ana kunywa mazima.

Ajitahidi kukimbia vyakula vyenye tindikali?? (Acid) kama Limau, ndimu, binzari, maharage, pombe kali au pombe kwa ujumla nk ...

Kwa nyie nduguze mjitahidi kuwa naye kwa karibu na kumkeep busy ili asiwe na muda wa kukaa na kufikiri saana.
 
Vidonda vya tumbo havisababishwi na kile unachokula bali kile kinachokula wewe hivyo tafadhali msaidieni kufaham ni nini kinamla? anawaza nini na kwakua ni mda mrefu sasa atumie maziwa wengine wanasisitiza ya mbuzi na kupunguza vitu vya acid kwakua tayari kuna michubuko.

Asante.
 
Katika matibabu yake alishapewa antibiotics yoyote au ni antihistamines tu?mara nyingi normal flora helicobacter pylori ndiyo chanzo kikubwa cha vidonda vya tumbo.

Sasa, kimatibabu pamoja na hizo H2antihistamines lazima uwadhibiti hawa jamaa pia kwa antibiotics.

Sikonge kakushauri vizuri,vidonda vya tumbo kama hypertension matibabu yake yanaambatana na lifestyle change. Kama anavuta sigara aache. Aepuke vyakula vyenye mafuta mengi,spices na vyenye acid. Asitumie any non steroidal antiinflammatory drug kama aspirin, ibuprofen nk.

Dawa pekee hazitoshi bila kubadili style yake ya maisha kwani vidonda vitakuwa haviponi au vitajirudia. Jaribu kuzingatia matibabu na ushauri wa daktari wako kabla hujaenda kwa waganga wa kienyeji
 
Katika matibabu yake alishapewa antibiotics yoyote au ni antihistamines tu?mara nyingi normal flora helicobacter pylori ndiyo chanzo kikubwa cha vidonda vya tumbo...
HELIGO KIT in antibiotics ndani yake!

Ushauri!

Aende kwa vipimo zaidi, inawezekana sio vidonda vya tumbo ambavyo tunavihisi/fahamu (hivyo vya H. pylori, NSAIDs, ama vya mawazo); yaweza kuwa ugonjwa mwingine kama Crohn's disease, matatizo ya kifuko cha nyongo, na syndrome yenye my favourite name- Zollinger-Ellison syndrome!
 
hahaha mazee umenikumbusha mbali sana na Zollinger-Ellison syndrome, lakini hata h2 antihistamines like cimetidine zingeiondoa kama ingekuwepo.

Anyway ushauri wako mzuri lakini mimi bado nasisitiza kuhusu kupata matibabu bora na kufuata ushauri wa daktari wake kama ugonjwa wake utabaki kuwa vidonda vya tumbo.
 
Dawa ya vidonda vya tumbo Mfahamishe huyo jamaa anayeumwa na Vidonda vya Tumbo atumie Dawa ya Hii ya Kienyeji Akiamka Asubuhi kabla ya kula kitu akojowe mkojo wake mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja awe anakunywa mkojo wake kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha Aende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa Mwambie ajaribu kutumia hiyo Dawa itamsaidia Sana.

Tahadhari:
Kabla ya kunywa huo Mkojo wake aende kupima Hospitali huo mkojo wake je unayo maradhi ya Zinaa au hauna? Ahakikishe Mkojo hauna Maradhi yoyote yale ndio anaweza kuutumia kwa kunywa .
 
Ndio Akinge (Urine) wake awe anakunywa kila Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa wiki moja aende kupima hivyo Vidonda vyake vya Tumbo vitakuwa Vimekwisha kauka na Matatizo yake yatakuwa yamekwisha nasema kweli simtanii hiyo dawa imewasaidia wengi.Kabla ya kunyw a:Mkojo wake akaupime hospitali je mkojo wake hauna maradhi yoyote yale? ndipo anaweza kutumia kwa kunywa.
 
Ndio Akinge (Urine) wake awe anakunywa kila Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa wiki moja aende kupima hivyo Vidonda vyake vya Tumbo vitakuwa Vimekwisha kauka na Matatizo yake yatakuwa yamekwisha nasema kweli simtanii hiyo dawa imewasaidia wengi.
Tena akiuvundika huo mkojo ndio bora zaidi, hata mie nimeona watu wamepona kwa dawa hiyo.
 
Hizi dawa zingine jamani zahitaji moyo,ninachojiuliza huyu aliyegundua dawa hii alikuwa anatafuta nini mpaka akafanikisha ugunduzi huu,any way kama pretty na mzizimkavu wako serious though I can't see it in their words,mgonjwa akashauriwe atumie dawa husika.DAWA HII NI ZAIDI YA DAWA YA KIENYEJI.
 
Dawa ya vidonda vya tumbo Mfahamishe huyo jamaa anayeumwa na Vidonda vya Tumbo atumie Dawa ya Hii ya Kienyeji Akiamka Asubuhi kabla ya kula kitu akojowe mkojo wake mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja awe anakunywa mkojo wake kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha Aende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa Mwambie ajaribu kutumia hiyo Dawa itamsaidia Sana.

Mzee wewe ni msabato masalia nini?!
 
Dawa ya vidonda vya tumbo ni mchanganyiko wa asali mbichi na juice ya alovera katika ratio ya 1:1. Tumia vijiko vya chakula viwili asubuhi, viwili mchana na viwili usiku kwa muda wa mwezi mmoja itakusaidia! Pia mwambie apunguze mawazo na ajitahidi kula ili tumbo lake liwe na digestable food material kwa muda mrefu!

How it works:
Kwanza, layer nene ya mchanganyiko huu hufunika kabisa vidonda vya tumbo na kuzuia uwezekano wa intestinal acids (e.g week hydrochloric acid, HCL) kuendelea kuishambulia ile ngozi laini iliyoathilika (vidonda).

Pili, wakati alovera juice (chemical) inatibu vidonda vya tumbo, asali inafanya kazi ya ku-hold still hiyo alovera chemical ili iendelee kukaa palepale kwenye kidonda(Asali inatumika kama binding material). So the mixture will persistently coat the infected area, hence it completely removes any further possibility of the intestinal acids and any other corrosive chemicals to reach that area.
 
Last edited:
Hizi dawa zingine jamani zahitaji moyo,ninachojiuliza huyu aliyegundua dawa hii alikuwa anatafuta nini mpaka akafanikisha ugunduzi huu,any way kama pretty na mzizimkavu wako serious though I can't see it in their words,mgonjwa akashauriwe atumie dawa husika.DAWA HII NI ZAIDI YA DAWA YA KIENYEJI.
Hizi ndio tiba mbadala wandugu na siyo utani!
Mkojo wako lakini, siyo wa mtu mwingine na unatibu magonjwa mengi sana.
 
wakuu habari za leo, nina ndugu yangu anasumbuliwa sana na vidonda vya tumbo tangu mwaka 1993 alipo pima na kugundulika kuwa ana matatizo hayo.
ombi langu kwenu kama kuna mtu nafafahamu dawa ya vidonda vya tumbo hata kama ya kienyeje naomba msaada wenu wa wapi inapatikana na kiasi gani. alisha tumia dawa za aina mbalimbali mpaka ile dozi kubwa ya HELIGO KIT, lakini bado.
naomba msaada wenu
Thanks

Castle,

Kwanza mpe pole sana. Mimi siyo Daktari ila ninajua dawa ya kienyeji ambayo niliwahi kuelekezwa kwa ajili ya my wife wangu, na alipoitumia akapona kabisa na ninatamani siku moja nimpate Daktari aliyebobea katika ugonjwa huu anielezee kwa undani.

Dawa yenyewe ni hivi, chukua kokwa la parachichi, likatekate vipande vidogovidogo kisha anika juani mpaka likauke. Baadae saga ili kupata unga laini. Chukua yai la kuku wa kienyeji, pasua utoe kile kiini chenye rangi ya njano, changanya na ule unga ambao umeandaa awali, koroga ili kupata mchanganyiko mzuri.

Kisha mpe mgonjwa wako anywe kijiko kimoja mara tatu, baada ya siku tatu atakuwa amepona.

Baada ya hapo akitaka kujua kama amepona au la, anaweza kufanya test ya kawaida kabisa kwa kula maharage, au chakula chenye pili*2 au akaenda kupima hospitali kabisa.

Ukifanikiwa ni PM.
 
Ndugu Che Kalizozele hiyo Dawa niliyosema Ya kutibu Mgonjwa Wa Vidonda Vya Tumbo nimeipata katika vitabu vya zamani sana vya Uganga wa Kienyeji vya Mwaka 1200 na Huo Utaalamu wa Kutumia Mkojo Kwenye Hospitali hawajuwi hata Ma Proffeser hawaoni ndani usione kuwa natani hiyo ni kweli na wengi waliojaribu wamepona.

Hakuna Dawa Ya kutibu Vidonda vya Tumbo yaani kwa lugha ya kigeni ni (Ulser) hakuna Hospitali ipo ya kutuliza tu sio kutibu Kunguru Mweupe kuna Maradhi ambayo hayawezi kutibika Hospitalini lakini kwa Wataalamu wa Kienyeji wanaweza kutibu kama Ugonjwa wa Pumu ugonjwa wa kisukari, Ugonjwa wa Kifafa, Ugonjwa wa Wendawazimu Kupooza na Ugonjwa wa Saratani (Cancer) na Ugonjwa Hepatitis B Virus.

Mpaka sasa hakuna Dawa za kutibu hayo maradhi ila zipo za kutuliza sio kuyamaliza Maradhi kinachotakiwa kwa Mgonjwa ni kujaribu kutumia Dawa ili kuona kama itaweza kumsaidia sio kupinga jamani Wenzangu tunajaribu kuelimishana sina kushindana asanteni sana.
 
mafuta ya Mamba sio Dawa ya kutibu Maradhi ya Vidonda vya Tumbo Jaribu kutumia Urine (Mkojo) wako mwenyewe kila siku ukinge Asubuhi Glasi moja unywe kabla ya kula kitu kwa muda wa siku 10 kisha uende kupima utakuta vidonda vyote vya Tumbo vimekauka na hiyo wamejaribu watu wengi imewasaidia ukiweza fanya hukuweza Achana nao itawasaidia wengine wenye huo ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo asante sana.
 
Inawezekana ikawa kweli,maana mimi nakumbuka ilikuwa 1994,nilikuwa nasumbuliwa na jino halafu nilikuwa ugenini nikuwa hapo Livingstone Zambia,sikuwa nafedha ya kutosha kung"oa jino nikashauliwa na mtu, lakini mimi hakuwa kunywa,niliambiwa asubuhi mapema kabla ya kula chochote nichukue glasi moja la mkojo wangu wa kwanza baada ya kuamka nisukutue kwenye meno na niteme kwa siku 3,nikafanya hivyo,leo ni mwaka 2009 sijawahi kuumwa jino mpaka leo,inawezekana Mzizi mkavu ni mkweli kabisa,kwani si ni mkojo wako kwani kunashida gani.
 
Lusajo Kyejo Waeleze wewe ndio labda watamini wanafikiri mimi ninawadanganya kuwa Mkojo wako mwenyewe unatibu Maradhi ya Vidonda vya Tumbo? wanafikiri ninasema maneno ya uongo jaribu kuwaeleza wewe labda wataelewa vizuri asante sana ndugu Lusajo Kyejo
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom