boniuso
JF-Expert Member
- Mar 13, 2013
- 680
- 852
KINACHO KUVUNJA MOYO SIO UBAYA WA TABIA ZA WATU BALI MATARAJIO YAKO KWAO
Kama usielewa asili ya tabia za binadamu utapata wakati mgumu sana kuwaelewa na kuishi nao
Alisema Marcus Aurelius miaka takribani 2000 iliyopita "Unayo nguvu ya kudhibiti akili yako tu sio watu au matukio kutoka nje yako"
Kwa sababu watu wengi hawajui hilo ndio sababu ya mateso yao ya kihisia kila siku
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna binadamu aliyekamilika na huwezi kuwa mkamilifu hivyo unatakiwa kuishi na watu vile walivyo sio vile unataka wewe
Binadamu huongozwa na hisia kwa kila maamuzi anayofanya hivyo akiwa na hisia za furaha atakusifia sana na akiwa na hasira atakulaumu sana hivyo sio matendo yako yenye kuamua kauli zao bali hisia zao kwa wakati huo
Chochote ambacho utasema au kufanya watu hawakipokei kwa uwiano sawa kwa sababu kila mtu anapitia maumivu tofauti na hisia tofauti
Mtu akiwa na hasira akili huwa inazima (brain shutdown) hivyo chochote utasema kwa ukali hakuelewi hivyo ukiendelea kumfokea ndio utafanya awe jeuri sana kuliko mwanzo
Kwa kawaida akili huwa inafanya kazi mtu akiwa na utulivu wa akili na sio kwenye stress
Hivyo unapokuwa na hasira huwezi kumuelewa mtu kwa chochote atasema na unaeongea nae akiwa na hasira hawezi kukuelewa hivyo inakuwa sawa na ubishi wa viziwi
Mtu aliyepita maumivu makali sana kama kubakwa,kuteswa, kubaguliwa, kupata ajali ikafanya apate ulemavu wa kudumu,kufanyiwa unajisi labda kubakwa na baba yake mzazi au ndugu wa karibu,mtu mwenye kupitia mahusiano yasiyodumu, mtu mwenye kupitia kipindi kigumu sana kiifedha, endapo utasimulia hadithi ya kuhuzunisha utaona analia sana au kuhuzunika sana unaweza kudhani hadithi yako ndio inafanya atoe machozi kumbe anakumbuka maumivu alipitia zamani au maumivu anayopitia kwa wakati huo
Ndio sababu mnaweza kwenda. Sehemu labda kwenye vituo vya watoto yatima kisha ukaona mwenzio anatokwa machozi kwa kuwaona yatima huku mwingine haonekani kuhuzunika kwa chochote
Kumbe mwenzio analia kwa uchungu kwa sababu alipitia maumivu utotoni hivyo ameona mtu ambaye anapitia maumivu kama yake
Watu wakiwa wamechanganyikiwa huwa hawaelewi chochote hivyo hata ukiwapa ushauri hawaoni uzuri wa ushauri bali wanaona giza kwa sababu ya maumivu wanayopitia
Kinachotokea katika maisha yako sio tatizo ila tafsiri unayoweka ndio inaweza kuwa tatizo au suluhu ya matatizo.
Maisha huleta 10% ya furaha yetu au huzuni yetu kisha kile watu huwa wanafikiria ndio huamua 90% ya furaha au huzuni
Mnaweza kutukanwa mkiwa kwenye kikao watu wengi tu lakini kuna baadhi watakuja juu sana kumshambulia alietukana na wengine utaona wapo kimya
Mfano kwenye whatsap group mtu anaweza kutuma link au video ambayo haiendani na maudhui ya group lakini kuna member wengi wa group baadhi watamtukana alietuma link na wengine watakaa kimya na wengine wanaweza kumjibu kwa ustaarabu tu
Tatizo sio kile kimetokea bali tasfiri yako unayoweka ndio huamua hisia zako wakati huo
Ukiamua kuangalia mabaya kwa watu utakuta mabaya mengi sana na utawachukia watu na ukitazama mazuri yao utawapenda
Ukiona mtu anakupenda anakuwa ametazama mazuri yako na endapo atatazama mabaya yako atakuwa adui yako
Na ukiona mtu anakuchukia anakuwa ametazama mabaya yako na endapo akitazama mazuri yako atakupenda
Hakuna binadamu mwenye mazuri tu au mabaya tu
Kwa vyovyote utafanya kuna mtu atapenda na kuna mtu atachukia kwa sababu kila mmoja huamua kuchagua upande wa kutazama kwa kila tukio
Ukitazama ubaya utapata hasira na ukitazama uzuri utakuwa na furaha ila watu wengi zaidi ya 80% ya watu duniani hutazama mabaya kwa kila jambo na kwa kila mtu ndio sababu maadui zako ni wengi kuliko marafiki wa kweli
Humpendi kila mtu hivyo huwezi kupendwa na kila mtu
Ili umchukie mtu tazama mabaya yake kwenye tabia na kasoro zake za maumbile lazima utamchukia
Ili ujichukie tazama kasoro zako za maumbile na matatizo yako unayopitia kwa sasa au makusa yako ya zamani
Ukianza kumsema mtu kwa mabaya yake lazima utamchukia na unaemchukia akipata pesa kukuzidi au cheo kikubwa au kuwa maarufu wewe ndio utateseka sio yeye
Utateseka kwa sababu utakuwa unapata hasira kwa mafanikio yake
Watu wanakuvunja moyo sio kwa sababu ya ubaya wa tabia zao bali matarajio yako kwao
Ondoa matarajio kwa watu kisha kubali chochote watafanya kisha angalia wapi unaweza kubadilisha na ikiwa huwezi kubadilisha acha tatizo kama lilivyo
Kama utaondoa matarajio utakuwa umejipa jukumu la kuwa problem solver na ukiwa na matarajio unakuwa unajizuia kufikiria njia mbadala endapo matarajio yako hayatatimia
Ondoa matarajio kisha wekeza nguvu kwa kile kipo ndani ya uwezo wako
Kusubiri .mtu mwengine abadilike tabia ili wewe uwe na furaha huko ni kuchanganyikiwa
Utazidi kupata hasira kama unataka mtu awe vile unataka wewe badala ya kumuacha awe vile alivyo kisha jifunze kuishi naye vile alivyo
Mvua ikinyesha na wewe umeanika nguo huwa unazitoa kwenye mvua ili hali ikiwa nzuri uanike upya kwanini ukipata matatizo hukubali kubadilika kuendana na mabadiliko?
Ukipata hasira kwa sababu mvua inanyesha ni kujitesa bure kwanza hasira haiwezi kukusaidia chochote wala haiwezi kuzuia mvua kunyesha
Ukipata matatizo kisha ukapata hasira ni wewe unateseka sio matatizo yako na vilevile hasira zako haziondoi tatizo unalopitia
Tabasamu kwa sababu haumiliki matatizo yote ya ulimwengu
Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke, Dar es salaam