Ona vituko vya katiba yako hii

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,863
5,694
Hivi karibuni tuu wakuu wa wilaya wameapishwa na mtukufu pale hemani na kugharimu mamilioni ya kodi zetu wana wa wadanganyika.

Pamoja na jamii kupiga kelele kuwa vyeo hivi ni mzigo kwa taifa havina tija yeyote, Leo nasikia tena eti Mkuu wa mkoa wa Dar naye anawaapisha tena wakuu wa wilaya wale wale walio apishwa na kuendelea kutafuna pesa zetu bila sababu ya msingi.

Wakati mtukufu anawaapisha wakuu wa wilaya mbona Mkuu wa Mkoa wa Dar alishuhudia pale na kama kulikuwa na haja hiyo kwanini hakuanza yeye kuwaapisha pale pale hemani?

Wakuu wa Wilaya wamesha apa kwa mamlaka iliyo wateau je wanakiapo cha tofauti na hicho walicho apa mwanzo ili Mkuu wa Mkoa awaapishe tena?

Hivi kwa nini wa CCM wanang'ang'ania hili katiba lenye mkanganyiko namna hii kwa faida gani?
 
Mbona huhoji kwa nini katiba ya CHADEMA haitambui nguvu ya mahakama katika kuleta haki kwa wanachama wake???? badala yake una lalamika kwa mambo yasio kuathiri!!!
 
mkuu nikusahihishe kidogo. pale ikulu hawakuwa wamekula kiapo bali walikuwa wanapewa mikakati ya kiutendaji na Rais. kwa kawaida wakuu wa mikoa ndio huapishwa na Rais halafu ma -DC wanaapishwa na wakuu wa mikoa husika.
 
Hivi karibuni tuu wakuu wa wilaya wameapishwa na mtukufu pale hemani na kugharimu mamilioni ya kodi zetu wana wa wadanganyika.

Pamoja na jamii kupiga kelele kuwa vyeo hivi ni mzigo kwa taifa havina tija yeyote, Leo nasikia tena eti Mkuu wa mkoa wa Dar naye anawaapisha tena wakuu wa wilaya wale wale walio apishwa na kuendelea kutafuna pesa zetu bila sababu ya msingi.

Wakati mtukufu anawaapisha wakuu wa wilaya mbona Mkuu wa Mkoa wa Dar alishuhudia pale na kama kulikuwa na haja hiyo kwanini hakuanza yeye kuwaapisha pale pale hemani?

Wakuu wa Wilaya wamesha apa kwa mamlaka iliyo wateau je wanakiapo cha tofauti na hicho walicho apa mwanzo ili Mkuu wa Mkoa awaapishe tena?

Hivi kwa nini wa CCM wanang'ang'ania hili katiba lenye mkanganyiko namna hii kwa faida gani?
Wakati mwingine jifunze kuuliza vitu ambavyo huvielewi kuliko kujiaibisha hadharani!
 
Back
Top Bottom