Ona Mkakakati wa Serikali yetu kudhibiti bei ya Chakula | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ona Mkakakati wa Serikali yetu kudhibiti bei ya Chakula

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Jan 13, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  SERIKALI imekutana na wasagishaji wa unga wa mahindi kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kupanga mkakati endelevu wa kudhibiti upandaji wa bei za mazao_Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Charles Walwa alisema jana alipokuwa akizungumza na wasagishaji hao.


  Alisema, lengo la kukutana nao ni mwendelezo wa mwaka jana ambapo wamekutana tena kutathmini nchi nzima ili kuhakikisha unga unauzwa kwa bei nafuu, isiyozidi sh 650 ikiwa watakubaliana. Alikiri kuwa hivi sasa bei za vyakula ziko juu, lakini kwa kuwa unga wa mahindi ndio chakula kikuu, bei yake ikidhibitiwa itasaidia kushuka kwa mazao mengine. Alisema katika mkutano huo wamekubaliana kuunda timu ya watu wachache kwa ajili ya kuchambua gharama wanazotumia ili kuhakikisha kuwa mlaji anafikiwa kwa bei nafuu kabla ya uhaba wa chakula unaokuwepo Februari hadi Aprili.


  Naye Godfrey Mlangu, akiwawasilisha wasagishaji wenzake aliulalamikia utaratibu uliotumika mwaka jana wa kuuza mahindi ya serikali, haukumnufaisha mlaji kwa kuwa gharama bado ilikuwa ni kubwa.

  Source: Tanzania Daima
  Maoni yangu.

  Hivi kwa mikakati ya kibabaishaji kama hii tutatoka kweli???Mimi sio mchumi ila sidhani kama kwa kukutana na kujadili na madalali wa mjini ndio unaweza kushusha bei ya chakula nchini. Hii ni sawa na kutibu dalili madala ya ugonjwa au kumwagia mti matawi badala ya mizizi. Mfumuko wa bei za bidhaa una sababu nyingi sana kuna inflation, production costs kupanda, high demand than supply etc???Kwa serikali kujadiliana na madalali/wasagishaji wa mjini kuna maana mbili tu kubwa: -

  1. Serikali inaona kuwa hawa madalali/wasagishaji ni walanguzi hivyo inashauriana nao ili wapunguze ulanguzi japo kidogo

  Dawa ya hili sio kujadiliana na walanguzi enzi za Sokoine watu ambao walikuwa wanalangua bidhaa kazi ya Polisi ilikuwa ni kukamata na kuwaweka ndani. Sina uhakika kama sheria aliyotumia Sokoine imeshafutwa. Ni jambo la ajabu kujadiliana na waalifu.

  2.Serikali inawaomba madalali/wasagishaji wapate hasara kwa faida ya walaji

  Kama madalali hawa sio walanguzi, maana yake bei wanayouzia nafaka kwa sasa inatokana na jinsi wao wanavyonunua mahindi toka kwa mkulima, wanaongeza gharama za usafirishaji na gharama nyingine pamoja na reasonable profit. Kama hivi ndivyo serikali kujadiliana nao ili bei ishuke ni kupoteza muda mana hakuna mfanyabiashara atakayekubali kupata hasara iwapo atakubaliana na serikali kupunguza faida kidogo anayoipata, kwani gharama nyingine zipo pale pale tena mbaya zaidi gharama za mafuta na umeme zinapanda kila siku. Je wakipunguza Serikali itawapa ruzuku???

  Kwa kweli kwa mikakati ya hivi jamani hatutoki, Serikali ikiri kushindwa kazi. WanaJF ishaurin serikali yenu nini kifanyike kupunguza kupanda kwa gharama za bidhaa nchini, mimi nadhani Serikali sasa ina tapatapa haijui nini cha kufanya, imeishiwa ubunifu na kukosa maarifa!!!
   
 2. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hayo ndiyo Maisha Bora kwa kila Mtanzania! Tliahidiwa hivyo tukatoa kura sasa tunaliwa.
   
 3. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Narudia kwa mara ya ishirini na tatu!, mpaka tutakapodhibiti matumizi yetu ya mafuta, inflation itakuwa inaongezeka tu.
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni siasa kuingilia sekta zote hata zile za kitaalamu. Hapo hahitaji kupiga siasa badala yake watu warejee kwenye references ili kupata solution za nguvu! Lakini kwa vile vilaza wameshika hizo nafasi, ni bora liende tu.
   
 5. h

  hmzuyu Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NFRA wana point muhimu hapa,
  Kama wananunua mahindi kati ya 300 na 330 kwa kilo vijijini,kwa kuamua kuwauzia wasagaji kwa Tshs 400/kg(mfano) kutafanya bei ya unga ishuke sana na sana.
  Kwa mantiki hiyo kutafanya wannachi wengi wawe na option kati ya kula ugali na vyakula vingine,litakalotokea ni kwamba vayakula vingine vitakuwa luxury needs na ugali utakuwa first choice.mpaka hapo bei ya mchele na baadhi ya nafaka itashuka automatick coz demand itakuwa ndogo kuliko suply.simply they are creating less demand in the remaining foods.
   
 6. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  NFRA hawana point yyte ya muhimu. We are facing with the problem of supply(mismatching of demand with supply). Uzalishaji wa nafaka umekufa(siyo umeshuka), umeme hakuna/umepanda, transportation costs ziko juu, then utarajie unga uuzwe 650-sahau. Ukweli ni kwamba serikali imeshindwa everywhere kusimamia uchumi kwa ujumla,so general govt reforms and restructuring z needed, otherwise all we gonna be die softly!
   
 7. h

  hmzuyu Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NFRA wana point muhimu hapa,
  Kama wananunua mahindi kati ya 300 na 330 kwa kilo vijijini,kwa kuamua kuwauzia wasagaji kwa Tshs 400/kg(mfano) kutafanya bei ya unga ishuke sana na sana.
  Kwa mantiki hiyo kutafanya wannachi wengi wawe na option kati ya kula ugali na vyakula vingine,litakalotokea ni kwamba vayakula vingine vitakuwa luxury needs na ugali utakuwa first choice.mpaka hapo bei ya mchele na baadhi ya nafaka itashuka automatick coz demand itakuwa ndogo kuliko suply.simply they are creating less demand in the remaining foods.
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  dawa ya kupanda kwa bei ni kuongeza wingi wa bidhaa sokoni, basi
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,906
  Likes Received: 5,367
  Trophy Points: 280
  inflation=a lot of money chasing few commodities,...
  solution=increase productivity not stupid slogans(kilimo cha kufa na kupona,kilimo kwanza,mabadiliko ya kijani(ccm)
   
 10. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Siamin unachokiongea na nina imani hata wewe huamini unachokisema. Anyway lets say Serikali itafanikiwa kwa mkakati huu wa kibabaishaji kushusha bei, je vipi kuhusu bei ya nafaka na vyakula vingine???Je nazo kwa serikali ni sahihi kuwa juu kiasi hicho???
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280

  :A S embarassed:Umeme nao umepanda bei, huyo msagaji atapunguzaje gharama? labda waparaze badala ya kusaga
   
Loading...