Ona mbinu za kuingiza madawa ya kulevya Bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ona mbinu za kuingiza madawa ya kulevya Bongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jun 29, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mwakilishi wa Matemwe, Abdi Mosi Kombo (CCM), amedai kuwa madawa ya kulevya yanaingizwa nchini na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao hufanikisha zoezi hilo kupitia Viwanja vya ndege na kupokewa na Polisi baada ya kupigiwa saluti.

  Kabla ya kauli hiyo, Mwakilishi wa Mwajuni, Mbarouk Wadi Mussa (CCM) alisema, “Hili suala naona hatujalifanyia kazi kikamilifu, kwa sababu wanaofanya biashara hiyo wapo na wanajulikana na wengine wamo humu humu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.”

  Kwa kauli hizo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman, aliwataka wajumbe hao kuthibitisha kauli zao kwa kuwa baadhi zinatoa shutuma nzito kwa Serikali na taasisi nyingine za kisheria, “Hizi ni kauli nzito sana na zinatakiwa kuthibitishwa na mjumbe ... kauli hizi zinadhalilisha wawakilishi na baadhi ya taasisi kama Jeshi la Polisi na wananchi kwa kusikia watadhani kwamba kumbe dawa za kulevya zinaletwa na viongozi,” alisema Othman.

  Mwanasheria Mkuu alimtaka Kombo kuthibitisha madai yake au kuomba radhi, ambapo Mwakilishi huyo aliomba radhi na kusema ni makosa ya kibinadamu tu. Othman aliwakumbusha wajumbe kuheshimu kanuni zinazoendesha Baraza la Wawakilishi, ikiwamo kutoa kauli kwa kuthibitisha na si kwa dhana tu.

  - HabariLeo
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,228
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Nilijua ni lazima alazimishwe kufuta kauli kwani kwa kauli hii maana yake kauli ya mh rais wa Tz itakuwa imefutwa. Kiuwajubikaji nilidhani kama serikali inania ya dhati ya kupambana na janga hili basi ingefanyia kazi kauli hii na kumtisha na kumzima mdomo muwakilishi.
   
 3. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi, kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, Kitengo cha Madawa ya kulevya si kiko chini ya Maalim Seif Sharrif Hamad! Sawa sawa!
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Serikali haina uwezo huo wa kuzui madwa ya kulevya ,kwani ndio inawanufaisha baadhi ya vigogo
   
Loading...