Ona jinsi Israel ilivyoichafua na kuibana mbavu Palestina

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,122
10,829
Kwa wale wenye umri kama wa kwangu enzi hizo watakuwa na uzoefu wa majina ya miji ya kipalestina ambayo kwa sasa yote imezingirwa na makazi ya mayahudi wanaohamishwa kutoka mataifa mengine duniani kuja kuwabana wapalestina katika lengo la kuwamaliza.

Hayo maeneo yenye bluu iliyokoza ndiyo makazi ya kiyahudi. Unaweza ukashangaa kwanini yote yasiwe eneo moja na karibu na mpaka upande wa magharibi. Haya maeneo yanakuwa yamechaguliwa maalum na kuwekwa kwenye ramani. Yanakuwa ni yale yenye rutuba au vyanzo vya maji safi au miinuko kwa matumizi ya kijeshi. Kinachofuatia huwa ni muda tu kulingana na bajeti ya nchi.

Zamu ya eneo fulani ikifika wakazi wa eneo hilo hupewa notisi ya kuhama kwa visingizio mbali mbali. Kwa udhaifu walionao na kwa kujua nguvu ya Israel wapalestina wengi huvunja majumba yao na kukushanya baadhi ya vitu vyao na kutia kwenye masanduku.Wale wanaoduwaa hawajachukua uamuzi, siku ikifika mabuldoza hufika na kuvunja bila kuhoji. Baada ya muda mfupi unakuta maghorofa ya wakaazi wa kiyahudi yakiwa yamebadili sura ya eneo lote.

Wapalestina waliokosa makaazi hawajui pa kwenda pia hupewa jina la wakaazi na sio raia na huwa wanapigwa danadana huku na huko mpaka wengi hufa na wachache wanaoamua kuhama hurahisishiwa njia za kutoka nje ili wakawe wakimbizi.

Mbali na makazi ya kiyahudi vijiji vilivyobaki vya wapalestina huzingirwa na kutenganishwa kwa kuta ndefu na seng'enge kiasi kwamba wapalestina waliokuwa majirani inaweza kuwachukua siku nzima mtu kumfikia mwenzake kutokana na kulazimika kuvuka vizuizi vingi vya kijeshi.

Mbinu hizi ni za muda mrefu na zinapata kasi kila mwaka.Mwaka 1948 mpaka 1967 ilikuwa ni kitu kingine na kutoka 1967 mpaka ilipomegwa Gaza ni kitu kingine. Na kuanzia hapo mpaka muda huu ni mbinu hiyo ya kuwazunguka wapalestina ndani kwa ndani.

Mafanikio ya Israel katika kuwadhoofisha maadui zao zinaonekana zimezivutia nchi nyingi zenye raia waislamu kama vile China na India.

1601284286690.png
 
Wapalestina warudishe maeneo ya watu waende kwao maana hayo ni maeneo ya islael tangu enzi za ibrahimu,maana kihistoria hapo walikuwepo wahiti,waamori,wahivi na baadae wafilisti.je wapalestina ni akina nani miongoni mwa hao?
Wafilist walikutwa na Abraham pale gaza,,mkumbuke mfalme wa waflist,Abimael alietembea na sara mke wa Abraham,mpaka abraham akampiga faini ya mifugo kibao,

Wafilisti ndo hao wapalestina wa gaza,

Wapalestina wa west bank ni tofauti na gaza lakini
 
Lete ushahidi kihistoria tuone,nionavyo nikuwa wapalestina ni waarabu wavamizi kutoka uarabuni.
 
Unaamini Israelites doesn't belong there?
 
Lete ushahidi kihistoria tuone,nionavyo nikuwa wapalestina ni waarabu wavamizi kutoka uarabuni.
Wewe inaonekana ni kilaza kweli kweli wa Jiografia na hupendi hata kuchungulia ramani na hujishughulishi na historia hata ya miaka ya karibuni.

Israel haikuwepo kabla,iliundwa 1948 na ikawekwa katikati ya mataifa ya kiarabu. Hivi sasa imezungukwa kila upande na hao unaowaita waarabu. Kwa kauli yako hii naona kama unadhani Israel imepakana na Burundi.
 
Ongezea kwa kuanisha mipaka ya Israel ilikuwa imeishia wapi
Wafilist walikutwa na Abraham pale gaza,,mkumbuke mfalme wa waflist,Abimael alietembea na sara mke wa Abraham,mpaka abraham akampiga faini ya mifugo kibao,
Wafilisti ndo hao wapalestina wa gaza,
Wapalestina wa west bank ni tofauti na gaza lakini
 
Wewe inaonekana ni kilaza kweli kweli wa Jiografia na hupendi hata kuchungulia ramani na hujishughulishi na historia hata ya miaka ya karibuni.
Israel haikuwepo kabla,iliundwa 1948 na ikawekwa katikati ya mataifa ya kiarabu.Hivi sasa imezungukwa kila upande na hao unaowaita waarabu.Kwa kauli yako hii naona kama unadhani Israel imepakana na Burundi.
Mkuu punguza jazba,Israel ilikuwepo hapo kabla ya 1948,sema waliondoka muda mfupi
Wewe inaonekana ni kilaza kweli kweli wa Jiografia na hupendi hata kuchungulia ramani na hujishughulishi na historia hata ya miaka ya karibuni.
Israel haikuwepo kabla,iliundwa 1948 na ikawekwa katikati ya mataifa ya kiarabu.Hivi sasa imezungukwa kila upande na hao unaowaita waarabu.Kwa kauli yako hii naona kama unadhani Israel imepakana na Burundi.
Mkuu punguza jazba,hebu tusianzie mbali tuanze tu tr.1/1/1,Yesu alizaliwa bethrehemu,alisali yerusalemu hapo ni mwaka 30,mpaka hapo unadhani wapalestina walitangulia? Na kwa nyingeza tu hata msikiti wa Al aksa umejengwa juu ya mahali palipokuwa na hekalu la mfalme sulemani ambaye ni muislael.wapalestina warudi kwao.
 
Wewe inaonekana ni kilaza kweli kweli wa Jiografia na hupendi hata kuchungulia ramani na hujishughulishi na historia hata ya miaka ya karibuni.
Israel haikuwepo kabla,iliundwa 1948 na ikawekwa katikati ya mataifa ya kiarabu.Hivi sasa imezungukwa kila upande na hao unaowaita waarabu.Kwa kauli yako hii naona kama unadhani Israel imepakana na Burundi.
Kaz wanayofanya israel ni nzursana. Kitu wanachoudh ni kule kuchelewa kuwamaliza hao wapalestine.
 
Back
Top Bottom