Ona hapa aina mbili mpya za wizi wa pikipiki ulioshamiri mijini

Fya-fyafya

Member
May 2, 2019
43
125
Hapa Nchini kumekuwepo na wimbi kubwa la wizi wa pikipiki hasa pikipiki aina ya Boxer.

Tena baada ya uzuka kwa ugonjwa wa Kirona, ndo hali imekuwa mbaya. Watu (bodaboda) wengi wamekuwa wakilizwa mara kwa mara.

Kwa nini pikipiki aina za boxer ndo zimekuwa zikishambuliwa sana kuibiwa? Wengi wanasema kinachotafutwa pale ni injini yake tu. Inasemekana inatumika sana kama mita ya kuvutia na kumwagilizia maji kwenye visima au kilimo cha umwagiliaji. Ila kama ni kuuza kwa ajiri ya spea, wezi hao huziuza kwa bei ya kutupwa sana.

Siku hizi ukiwa na pikipiki mpyunaifanyia kazi basi inabidi uwe mwangalifu sana tena sana. Hasa uwe selective wa abiria wako.

Baada ya utangulizi huo sasa niende kwa maada husika :" Ona hapa aina mbili mpya za wizi wa pikipiki uloshamiri mijini" na hizo mbinu za wizi ni

1) Mhogo feki kwenye mguu.

Hapa inakuwa hivi. Jamaa anachukua mabox ama vitambaa na kujiviringishia pamba juu kwenye unyayo na vidole hadi usawa wa goti mithili ya mtu aliyevunjika mguu na kuwekewa mhogo.

Kisha anachukua gongo na kuzuga nalo mara nyingi wanategeshea maeneo ya hospitali. Anajifanya kama vile ameruhusiwa (discharge) kwenda nyumbani. Anaweza akawa na kijibegi mkononi au mgongoni.

Basi ana chunguza bodaboda mwenye pikipiki boxer mpya na kumwita ampeleke mahali hasa hasa nyumbani. Basi kwa shida sana atapanda piki piki kisha anaondoka.

Trick ya wizi
Mkiwa njiani, tadondosha kwa makusudi lile ngongo kisha kukuomba msimame. Basi kwa vyovyote vile kwa huruma bodaboda atasimamisha pikipiki na kwenda kwa mguu harakaharaka kumchukulia lile gongo. Hapo hapo ndo penye mistake. (One mistake one goal) Bodaboda akiwa anaenda kuchukuwa hongo ndipo Mwizi huyo hudandia Pikipiki na kuondoka nayo Nduki. Watoto wa mjini wanasema anamwachia manyoya huku akijisemea kwa dharau :" Pumbavu Shenzi!"

2) Makazi feki kwenye nyumba ya heri.

Hii nayo inakuwa hivi:
Tofauti na ya kwanza ambapo anakuwa mtu mmoja, hapa hawa mabwana (wezi) wanakuwa kidogo a team. Wanaweza kuwasiliana watatu ama wanne.

Mchezo unakuwa hivi.
Hawa jamaa wanatafuta nyumba yenye geti iliyoko sehemu tulivu sana. Na wanakuwa wanakuwa kuwa wakazi wa nyumba hiyo si wengi na wako bize na mambo yao ( watu wa serikali au wafanyabishara) na once wametoka hawarudi mapema na endapo wamerudi hawatoki tena mpaka kesho.

Basi, hawa mabwana wanajipanga hivi. Wawili ama watatu wanabaki wamejificha maeneo ya getini la hiyo nyumba kisha mmoja wao anaenda kijiwe chochote cha pikipiki na kusellecki (kuchagua) bodaboda mwenye pikipiki boxer mpya na kumwambia ampeleke nyumbani.

Basi bodaboda walivyo na haraka atakubali na kubagain naye bei na kumpakia na kwenda naye kama abiria. Wakiwa njiani, huyu bwana anakuwa anawasiliana na wenzake wale kuwa wanakuja nao wajiseti kisawasawa.

Kama tujuwavyo bodaboda huongozwa na abiria basi jamaa atampekeka mbaka getini kwenye ile nyumba ambayo wenzie wameshajipanga. Basi jamaa (wizi) atashuka na kumpa bodaboda hela kubwa inayohitaji Change let's say 10000 au 5000.

Basi huyu bodaboda akiwa kwenye harakati za kujisachi chenji mfukoni ndipo wale wezi wengine hujitokeza na kumkaba ama kumpiga sehemu mbaya mwilini (wao wanazijua) ambapo ukipigwa mara moja unalegea hata sauti haitoki. Basi wao hujisemea kwa zarau'' Bumbavu" na kuchukuwa pikipiki na kupakizana mshikaki na kuishia nayo.

Aina hii ya wizi hutokea muda wowote . Hasubuhi, mchana na hata jioni.

My take. Chonde chonde, madereva bodaboda kuweni makini sana. Yamkini wewe unaesoma post hii si bodaboda ila una ndugu au jamaa ambaye ni boda boda au kabisa wewe mwenyewe unamiliki Pikipiki na umemwajiri kijana anakuletea hesabu jioni, basi ni mwafaka wa kumpa semina ya wizi huu wa piki piki.
 
Hiyo njia ya pili ilishawahi kutumika nyumbani kwangu. Ilifanyika mchana tukiwa hatupo nyumbani (Yaani mimi na Mr. Wangu) walikuwepo watoto tu nyumbani
 
Hiyo njia ya pili ilishawahi kutumika nyumbani kwangu. Ilifanyika mchana tukiwa hatupo nyumbani (Yaani mimi na Mr. Wangu) walikuwepo watoto tu nyumbani
Waliingia ndani ya geti kabisa au walikuwa nje kwenye fensi?
 
Toka niibiwe simu aina ya tecno p3 mwaka 2012 na Malaya wa buguruni sidhani kama nitaibiwa kwa vimaneno tu.

Sina huruma na wezi.
 
Kuna jamaa wawili kutoka Dar walienda kuiba piki piki huko Bagamoyo na wakafanikiwa....kufika njiani Piki piki ikazima wakahisi ni mafuta...wakaingia chaka kidogo mmoja akaenda kutafuta mafuta...kumbe ile piki piki imefungwa kifaa cha Kui track popote iendapo na mwenyewe huweza kuizima muda wowote.

Basi baada ya muda yule mwizi akashangaa kundi la bodaboda likienda direct alipojificha....walichukua piki piki wakamuua kwani alikua amejificha juu ya mti...aliyeenda kununua mafuta alinusurika.

Fundisho:Kuna kampuni zinafunga vifaa hivi,kwa Piki piki haizidi 200k na chombo kinakua salama....kama unampa bodaboda Mkataba unaijumlisha kwenye mkataba kwani ukilipa umelipa...tujifunze kujiweka salama jamani...Sijazitaja kampuni makusudi ila zinajulikana sana tu.
 
Asante kiongozi taarifa tutawapa wahusika mana hata bodaboda tunazopanda pia unaweza kumweleza ili akotoe somo kijiweni kwake inaweza kusaidia!
 
Nilikuta damu nyingi, na watoto waliniambia walisikia fujo na mtu akikoroma nje ya geti wakajifungia ndani kimya hadi kulipotulia.

Majirani waliokuja kushuhudia waliniambia hapo kwangu leo kuna mtu kaibiwa pikipiki, mwizi alimwambia dereva bodaboda ya kuwa eti anafanya kazi hapo kwangu, hivyo anahitaji usafiri, na mwizi alinunua hadi mfuko wa cement kwa ajili ya kazi hiyo kwangu wakati sio kweli. Wala sikuwa na ujenzi wowote pale kwangu muda huo. Naambiwa kuna wezi wengine walijificha porini, ndio walishirikiana kumuumiza dereva bodaboda.
 
Kuna jamaa yangu boda boda zake kazitrack,popote ilipo anaiona na akitaka kuizima muda wowote anaizima,hii kidogo inaweza kusaidia
 

Attachments

  • Screenshot_20201009-091804_SinoTrack Pro.jpg
    Screenshot_20201009-091804_SinoTrack Pro.jpg
    121 KB · Views: 24
Back
Top Bottom