on xxl,Diamond afunguka kuhusu mganga na show zake kuishiwa watu

heaven on desert

JF-Expert Member
Jan 25, 2013
1,025
393
KAMA KAWAIDA YANGU..NANDELEA KUSEMA MAZURI KUHUSU PLATMUMZ MPKA HATERS WAKAE

Leo Diamond Platnumz kupitia
kipindi cha XXL cha Clouds FM,
ameamua kufunguka kwa undani
kuhusiana na shutuma
zinazoelekezwa kwake kuanzia
kudaiwa kutumia waganga wa
kienjeji kuosha nyota yake na
scandal zingine. Kuhusiana na
mganga anayedai kuwa atamshusha
Diamond baada ya kumtelekeza
Diamond amesema:
Mganga wa ukweli hawezi akaenda
kulalamika kwenye media eti ‘ mteja
wangu kanikimbia nini na nini’
mganga anaenda kulalamika katika
killing! Kama ni mteja wako kweli
utaenda kuripoti kwa mzee wako
aliyekupa ndumba kwamba yule
ashuke, akishuka mwenyewe
atarudi atakwambia ‘broo
nimeshuka tuyamalize,’ lakini mtu
anaenda kwenye redio eti namba
yangu ya simu napatikana hii eti
napatikana kwenye Facebook
(anacheka) ……….mara ya kwanza
nilivyosikia nilicheka sana nikasema
da!!!! Mwenyezi Mungu kanipa
nyota kubwa sana mpaka baadhi ya
waganga wanataka ku hit kupitia
nyota ya Diamond hiki ni kitu cha
kuchekesha! Halafu kikanishangaz.
Kuna siku nilienda katika tv station
moja nilipofika nikaona jina lake
nikasema mimi nataka niwekwe
naye meza moja tukae nizungumze
nisikie anasemaje lakini mwisho
wasiku akakataa ananikimbia
anasema ‘mimi sitaki kulumbanan
nae nini na nini’ sasa ukitazama
unaona tu.
Unajua kuna kitu kimoja ambacho
kipo Tanzania mtu anapoanza
kufanya vizuri kutengeneza ramani
nzuri watu baada ya kumsaidia
kumsapoti kutoka juu aende mbali
zaidi wanataka kumgandamiza
kumshusha na hili ndilo tatizo
tunalipata hata kwenye mipira
tunakosa wachezaji wakucheza nje
na nini, kwasababu watu kama
akina Ngassa wakiwa wanajitahidi
badala ya kuwasapoti mwisho wa
siku mtu akitaka kusajiliwa na timu
fulani kucheza oo!! mara watu
wanaanza kuzusha kapewa chakula
hajamaliza kapewa kuku mzima
hajamaliza wewe unatakiwa
umsapoti.
Kuhusu kama aliwashahi
kumuona mganga huyo
Sijawai kumuona nilimuona kwenye
gazeti na kwenye gazeti niliona
picha yake inakuwa vipi , kilicho
nistaajabisha ikanibidi mimi lazima
nitafute source imekuwaje?
nikatoka unajua kila kitu lazima
nimlalamikie mama yangu,mama
akaenda kumtafuta papaa
akamwambia kwasababu alikuwa
anasema alikuwa ananitumia toka
zamani basi hii link imetoka huko.
Papaa akaulizwa akasema ‘kuna
watu mwanzo tulikuwa tunafanya
nao kazi hadi tukavunja mkataba
mimi na Papaa hadi nikamlipa pesa
papaa wale watu walikasirika
kwanini papaa umevunja mkataba
na Diamond, wakati Diamond
anazidi kufanya vizuri tungekuwa
tunavuna mapesa ,kwahiyo wale
watu ndio wanaunda fitina hivyo
wanamtishia papaa. Huwezi kuamini
hawa watu walikuja kuniibia tuzo
moja ama kwamba waende
wakaizindike wenyewe wanavyodai
ili wakaichimbie kwenye shimo lile
shimo ndilo linalopandisha msanii,
kwahiyo atashuka, cha ajabu
nikapata tuzo nyingine.
Kuhusu Q-Chief
Kiukweli naomba niongee ukweli
maana kuna vitu vina fichwa fichwa
mimi nawaheshimU sana wasanii
waliotangulia sababu najua hata
nikifanya nini siwezi kuwafikia, wao
alioanza kaanza tu. Lakini
nasononeshwa na mimi eti
kujitangaza kwangu namkubali Q
chief yeye mwenzangu anasema
mimi natembelea nyota yake,
kampigia simu dada yangu Halima
anamtukana hadi meseji zipo eti
Diamond anasifia nyota yangu, sijui
nini na nini! Come on mimi naanza
kutoka maskini ya Mungu na Nenda
Kamwambie Q chief kishapotea,
mimi mapenzi yangu tu namkubali
kwanini nisingesema labda..
brother Dully wajua kaka yangu
kabisa siwezi kusema ndugu lakini
ananisaidia katika vitu vingi
ningekuwa mnafiki ningesema labda
namkubali sana Dully ndio msanii
wangu namna moja namkubali.
Lakini nasema hhaa namkubali Q
Chief.
Lakini yeye kumheshimu kwangu
mimi anasema eti mimi namroga.
Kuna siku unajua alinikuta kwa
Manecky akaniambia “ mdogo
wangu mwanzo mimi nilikuwa
nafikiri unaniroga mimi nilikuwa
nikienda kila kwa mganga
ananiambia haunirogi, dah nilikuwa
nakumind kinoma”. Kila nikienda
namkuta Khalid sasa yeye kasema
mwanzoni TID alikuwa anamroga,
alivyotoka Cassim Mganga akasema
Cassim anamroga, alipotoka Ali
Kiba akasema anamroga sasa kila
msanii anayetoka anasema kamroga
yeye tu kwa nyota ipi? Ya kuvuta
unga ya kufanya vitu gani! Mimi
sipendezewi anavyowaambia watu
kuwa mimi namroga, kwanini
nisitembelee nyota ya watu kama
akina Omary, akina Ben Pol.
Alumbane na wakubwa wenzie akina
Dully Sykes, mimi sitaki,
namheshimu abishane na wakubwa
wenzie, mimi mdogo aniache na
wadogo wenzangu.
Kuhusu tetesi kuwa show zake
zimepunguza mahudhurio ya
watu kuliko mwaka jana
—Picha ya show yake ya Mwanza
hivi karibuni
Hizo ni drama tu watu
wanatengeneza watu kuna zile
kuvizia mwanzo wa show, maake
kuna show nimeziona watu
wamevizia watu wanavyoingia
mwanzo eti wanapiga picha,
wanatengeneza tengeneza vipicha
halafu wanasema hivyo. Show
yangu ya mwisho nimefanya Arusha
tarehe 16 kiingilio 150,000 watu
walivyoingia pale ukiingia katika
thisisdiamond unaona. H kufanya
msanii yeyote kiingilio laki na
hamsini nimefanya Arusha.
—Diamond akiperform kwenye
show ya Arusha kwenye ukumbi wa
CLUB SAFARI CARNIVAL
Mtu anasema yeye ananiroga mimi
nashuka mwezi mzima ntakuwa na
show Europe, Jumamosi nina show
Hyatt pale, Jumapili nina show
Mombasa wiki inayofuata ninasafiri
naenda nje nina show kama kumi
yaani ukinibook mimi mpaka mwezi
wa saba nimejaa wewe unaniambia
mimi nimeshuka vipi!
Kuhusu uhusiano na Penny
No Penny tunafanya movie
anacheka, kuna movie tunarekodi
sio wapenzi
Fetty: Diamond unadanganya bro
B12: Kwasababu kuna picha nyingi
zinasambaa kwenye Instagram yale
ni mapozi ya kutengeneza hiyo
movie au?
Diamond: anacheka yeah pale
tulikuwa tunarekodi sababu ni
movie ambayo tuna mahusiano
kwahiyo wakati tuna rekodi kuna
picha zinakuwa zinapigwa, ni
dramatic za kuuza movie unajua!
B12: Movie inaitwaje na inatoka
lini? Adam: na kampuni gani?
Diamond: aaaaaaaaaah vitu vingine
vya siri (wote wanacheka)
Fetty: kuna story za chini chini
sana, the reason why unamuita
baby mama (Penny) kwamba she is
expecting….
Diamond: Analikwepa swali huku
akicheka na kudai muda wa kipindi
cha XXL umeisha wawapishe
wengine.
Kuhusu wimbo aliomshirikisha
Tanzanite uitwao Mapenzi
Diamond anasema hajamshirikisha
Tanzanite na kwamba amekuwa
akimchokonoa tangu aseme wimbo
Mbagala ulikuwa wake na baadaye
kudai Diamond anamroga. Anasema
alichokifanya sasa ni baada ya
kupata wimbo wa Diamond uliovuja
ambao ulikuwa na verse moja tu,
Tanzanite aliuchukua na kurekodi
verse yake kisha kujifanya kuwa
ameshirikishwa na Diamond.
Diamond anasema amefanya hivyo
bila ridhaa yake. Amedai kuwa
atamfanya kitu kibaya kama
akiendelea kumtafuta.
Kuhusu kushindwa kwenda show
ya Rwanda
Amedai kuwa Micho ni msanii
anayefanya vizuri nchini Rwanda
ambaye alimpigia simu kumuomba
wafanye collabo. Anasema Mico
alikuja Tanzania na Diamond
akakubali kufanya collabo naye
bure kwenye studio za MJ Records.
Anasema msanii huyo alimtaka
aende kufanya naye show Rwanda
na kumpa advance Diamond dola
1,000 kati ya 6,000 alizotakiwa
kutoa kwaajili ya show hiyo. Micho
aliahidi angempa tena dola 2,000
tarehe 20 January lakini aliendelea
kumpiga chenga Diamond.
Tarehe 11 Feb alimtumia dola
2,000 kwa njia ya western union
lakini kuhusu tiketi za ndege
Diamond anasema Mico alidai kuwa
ndege zimejaa hivyo aende peke
yake na yeye akamwambia kuwa
lazima aende na dancers wake na
mpiga picha wake.Diamond
anasema Micho aliendelea kumpiga
sound mpaka siku ya show na siku
hiyo ndio akamtumia tiketi saa
kumi kasora muda ambao Diamond
asingeweza kusafiri. Diamond
anasema hilo ni kosa la Mico.
 
Wachawi tu kila mtu anamsema yeye?kwa lipi la maana analoimba?wamekuepo kina marijan,kina nguruma itakua diamond?
 
Unaelewa wanaume wengi unaweza kuwaita haters wa Diamond kwani yeye hujiita "sukari ya warembo"na wale warembo wote ndio wanamuona kama "sukari!"Sasa huwezi kuwalazimisha hao unaowaita "haters"kumpenda Diamond iwapo wao sio warembo!Na vile vile huwezi kuwazuia warembo kumpenda "sukari wao"si sukari unajua ni tamu?acha wairambe!na waswahili husema mapenzi hayana macho!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Diamond anajíita sukari ya warembo, pia kipenzi cha mabinti. Je wewe ni binti au ni mrembo?

attachment.php
 
ahahahahahahahhaaaaaaaaaaaaaaaaa....mmmmmmmh_na nani sasa..atakuwa anapumuliwa na Diamond nini?
We pozi gani hizi kwa picha, piko hadi kidevuni bwana, mwanaume unajireeeemba kufa, basi vaa na gauni tujue moja
 
Mtoa mada ck nyingine mfunze diamond kujib maswal kwenye media me jana niliona anajidhallsha huku diva akimchora.....
Shame on him.... Wema sepetu academy bado haijamsaidia japo alimponda sn....
 
Kumbe ndio mana unamuhusudu sana domondi!!!!! Coz yeye anavua nguo na kutuonyesha ------ yake na wew fuul make up usoni!! Coz wote ni marioooooo

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom