On Star TV - Nape afafanua mpango wa "kuhuisha chama"

Status
Not open for further replies.

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
705
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Nape Moses Nnauye atakuwepo katika kituo cha Television cha Star Tv katika kipindi cha tuongee asubuhi akiongelea juu ya dhana ya kujiuhisha iliyopo kwenye mkakati wa Chama ambao sekretarieti ya sasa imekuja nao katika kurejuvenate mkakati wa "kujivua gamba" uliopitishwa na Chama Hiko mwaka jana.

Live LINK: Star Tv - Live
Na Bashir Mkoromo, Mwanza.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye amefafanua juu ya Mkakati uliopo sasa wa Chama Cha Mapinduzi wa kujihuisha. Nape ameyaeleza hayo leo asubuhi alipotembelea katika studio za Kituo Cha Televisheni cha Star Tv kilichopo Jijini hapa katika Kipindi cha Tuongee Asubuhi.

Nape alitoa Ufafanuzi kuwa kwa Taasisi ya Kisiasa kama Chama Cha Mapinduzi ambacho asili ya kuundwa kwake kimetokana na Chama Cha TAA na baadae kuwa na mabadiliko ya muundo na jina mpaka kufikia CCM ya sasa hatua za mabadiliko haya zinabeba tafsir ya kujihuisha na kukifanya Chama Kubaki na Nguvu yake na Uwezo wa kiutendaji na Utekelezaji wa ILANI yake kulingana na mazingira husika.

Pia Nape alieleza kuwa Utaratibu uliopo sasa wa Chama Kuzunguka na Mawaziri katika sehemu mbalimbali ambapo Chama Kinafanya mikutano ya hadhara na kusikiliza pamoja na kutatua kero mbalimbali na changamoto ambazo wananchi wanakutana nazo. Na kueleza kuwa Mkakati huu wa kuzunguka na Mawaziri unatokana na ukweli kuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho chenye dhamana mbele ya wananchi ya kujibu na kujieleza juu ya utendaji wa Serikali.

Pamoja na hayo, Nape akawataka watu kuacha kutoa tafsir potofu na kuwataka watu waelezee uhalisia wa mapungufu yaliyopo kwenye Chama na Serikali bila kuongezea chumvi na kuyakuza kwa lengo la kutaka kuonesha wananchi kuwa Chama kimeshindwa kuisimamia Serikali yake. Akatoa mifano na takwimu mbalimbali na kuelezea ukweli juu ya kelele za uzushi kuwa CCM inaongozwa na watoto wa vigogo na kueleza kuwa kati ya wanachama zaidi ya 5000 waliojitokeza kuwania nafasi za uongozi ndani ya Chama ni wanachama ambao hawazidi 20 ndio wenye majina ya wanasiasa na miongoni mwao hao wapo waliokosa, kwa maana hawakuchaguliwa.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi yupo Mwanza kwa ziara maalum Mkoani humo, ambapo amefuatana na wasaidizi wake na ziara hiyo itaisha hivi karibuni.
 
Steven Robert Masatu

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
2,464
1,819
Nape. nyoka anajivua gamba ili apate nguvu zaidi ya kukabiliana na mzingira na kupata nguvu zaidi ya kusonga mbele. ccm tunapaswa kujivua sasa jabla ya kuvuliwa kwenye sanduku la kura.
 
tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,856
1,101
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Nape Moses Nnauye atakuwepo katika kituo cha Television cha Star Tv katika kipindi cha tuongee asubuhi akiongelea juu ya dhana ya kujiuhisha iliyopo kwenye mkakati wa Chama ambao sekretarieti ya sasa imekuja nao katika kurejuvenate mkakati wa "kujivua gamba" uliopitishwa na Chama Hiko mwaka jana.

hawa jamaa ni kichefuchefu tu
 
TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
705
--> Anaelezea juu ya mpango wa sasa wa kukiongezea Chama nguvu ya kuisimamia serikali, na amefafanua juu ya suala la Mtwara na habari ya kuzomewe iliyovumishwa na magazeti.

--> anaeleza pia kuwa Taasisi ambayo imeanzishwa katika asili yake kama Chama Cha Wafanyakazi na kuendelea kuchukua sura tofauti tofauti mpaka kufikia CCM ya sasa, ni jambo jema kufanya na kuweka mikakati ya kujiuhisha na kujiweka katika hali ya kudumu zaidi na kuendelea.
 
mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,166
776
mnawasafisha sana kuwaleta star, alikuja startv mara ngap, hivi? hakuna watu wengine wa kuja hapo? ninyi ndio maadui zetu. nape anajipya lipi????????? kupotezeana muda.. i wont tune startv now!!:A S angry:
 
zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
250
hakuna matumaini mapya yoyote ndani na nje ya serikali ya CCM! Ufiasadi, utoroshwaji wa fedha na rasilimali nje ya nchi, hali ngumu ya maisha kila kukicha, ukosefu wa ajira kwa vijana, CCM ina jipya gani?
 
TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
705
Mwanasheria wa SAUT Bwana Patrobass Paschal ambae pia ni mwalikwa aelezea juu ya kuachana na Dhana ya kiita Serikali kuwa Ni serikali ya CCM kwa hoja kuwa wanaCCM wanapersonalize serikali na alidai kuwa Chama ni tofauti na serikali.

Aelezea kuwa alitegemea Chama kingelibadili na jina na kujiita jina lingine ili mabadiliko yanayofanywa sasa yapate mambo.
 
Afsa Mkuu

Member
Nov 15, 2012
52
8
Jamani embu nisaidieni, Siyo Nape alisema watu wajivue gamba ndani ya siku 90?? Ss leo anakuja na sera nyingine tena yani apa maji ni yale yale ila chupa tofauti. Wasubiri 2015 tutawavua gamba lote.
 
zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
250
wanajamvi kama mna access ya tv karibu naombeni mwangalie star tv nape anatolewa povu na wanaharakati!!
 
W. J. Malecela

JF-Expert Member
Mar 15, 2009
14,045
8,890
Mwanasheria wa SAUT Bwana Patrobass Paschal ambae pia ni mwalikwa aelezea juu ya kuachana na Dhana ya kiita Serikali kuwa Ni serikali ya CCM kwa hoja kuwa wanaCCM wanapersonalize serikali na alidai kuwa Chama ni tofauti na serikali.

Aelezea kuwa alitegemea Chama kingelibadili na jina na kujiita jina lingine ili mabadiliko yanayofanywa sasa yapate mambo.

- Huyu huenda hajui siasa, Serikali inakuwa ya Chama kinachotawala tu hakuna njia nyingine, kama anataka iitwe Serikali ya Chadema, asubiri uchaguzi ujao labda yanaweza kutokea maajabu ya Mussa, ingawa dalili za mvua huwa ni mawingu, yaaani Majuzi Chadema wameshindwa Uchaguzi wa MAdiwani tu, je wataweza Taifa?

Le Mutuz!!
 
Afsa Mkuu

Member
Nov 15, 2012
52
8
Tulitakiwa tuwe na uchumi mzuri kuliko Kenya na tuwe ktk nchi yenye uchumi mzuri hapa Africa, Ss leo nape anatuambia eti tumepiga atua lkn mzee mwenye suti nyeupe kampatia kweli kamwambia kutokana na rasilimali zetu tulipaswa kuwa mbali sana!
 
TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
705
- Huyu huenda hajui siasa, Serikali inakuwa ya Chama kinachotawala tu hakuna njia nyingine, kama anataka iitwe Serikali ya Chadema, asubiri uchaguzi ujao labda yanaweza kutokea maajabu ya Mussa, ingawa dalili za mvua huwa ni mawingu, yaaani Majuzi Chadema wameshindwa Uchaguzi wa MAdiwani tu, je wataweza Taifa?

Le Mutuz!!

Kimsingi ni kuwa watu wenye mitazamo hasi juu ya chama cha mapinduzi wamekuwa wakihaha kutafuta namna ya kuifanya CCM isisikike katika yale inayoyatekeleza na kuyatimiza katika yale waliyoyaahidi kwenye ILANI ya Chama hicho, hivyo wamekuwa wakiacha kujadili kuchindwa ama kufanikiwa kwa CCM na badala yake wanajadili juu ya majina ya CCM, nguvu za CCM kwa serikali na wanajadili haya kwa kutaka kupunguza kazi na ari iliyopo sasa ya chama katika kuisimamia serikali.
Hivi karibuni alionekana LIssu akitamani kabisa KATIBA ibadilike na yeye apewe fursa ya kuchagua majaji na kuajiri mahakimu.,haya yanafanana na huyu anayetamani serikali isiitwe serikali ya CCM.
 
Mbona uongei kuhusu Arumeru mashariki?
 
Nyangumi

JF-Expert Member
Jan 4, 2007
507
16
Haiwezi kuwa serikali ya ccm. Ni serikali iliyoundwa na ccm. Ukishauza chungu kikanunuliwa kinakuwa si mali ya mfinyanzi tena, bali cha aliyekinunua. Serikali niya wananchi.
 
Ichobela

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
326
156
Hivi Le Mutuz unatumia nn kufikiri? Ubongo au mmbadala?CDM ilikuwa na viti vingapi b4 na maiti sisiem ilikuwa na viti vingapi? Jitu kubwa akili ya kitoto! Ovyooo...bora urudi USA ukaendelee na kuhesabu abiria wa meli men!
 
W. J. Malecela

JF-Expert Member
Mar 15, 2009
14,045
8,890
Kimsingi ni kuwa watu wenye mitazamo hasi juu ya chama cha mapinduzi wamekuwa wakihaha kutafuta namna ya kuifanya CCM isisikike katika yale inayoyatekeleza na kuyatimiza katika yale waliyoyaahidi kwenye ILANI ya Chama hicho, hivyo wamekuwa wakiacha kujadili kuchindwa ama kufanikiwa kwa CCM na badala yake wanajadili juu ya majina ya CCM, nguvu za CCM kwa serikali na wanajadili haya kwa kutaka kupunguza kazi na ari iliyopo sasa ya chama katika kuisimamia serikali.
Hivi karibuni alionekana LIssu akitamani kabisa KATIBA ibadilike na yeye apewe fursa ya kuchagua majaji na kuajiri mahakimu.,haya yanafanana na huyu anayetamani serikali isiitwe serikali ya CCM.

- Katiba ibadilike Lissu achague majaji? Really? akazane kukisaidia chama chake kishinde uchaguzi kama hakishindi maana yake ni kwamba wananchi hawaitaki message yake, hatuwezi kuhamisha magoli ya mchezo ili Lissu achague majaji ni ndioto ya alinacha!!

Le Mutuz!1
 
Snipper

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
1,244
1,946
Star Tv huwa hawajifunzi, huyu mzee Farijala si ndio aliitukana ITV kuwa ni ya kihuni alipobanwa na wapiga simu kutokana na uchangiaje wake wa ajabu ajabu kuhusu kipindi ile polisi walipokuwa wanaua raia kwa kushindana ikiwemo mauaji ya mwangozi na yule jamaa wa morogoro? James Range angalia wageni unaowaleta hapo studio maana at the end nahisi patabadilika hapo studio!
 
W. J. Malecela

JF-Expert Member
Mar 15, 2009
14,045
8,890
Hivi Le Mutuz unatumia nn kufikiri? Ubongo au mmbadala?CDM ilikuwa na viti vingapi b4 na maiti sisiem ilikuwa na viti vingapi? Jitu kubwa akili ya kitoto! Ovyooo...bora urudi USA ukaendelee na kuhesabu abiria wa meli men!

- CCM ndio chama tawala, kama mnataka iwe Serikali ya Chadema jitahidini kushinda auchaguzi sio kupiga piga ramli hapa na maneno mengi ya kusadikika!!

Le Mutuz!
 
fige

JF-Expert Member
Jul 4, 2010
376
61
- Huyu huenda hajui siasa, Serikali inakuwa ya Chama kinachotawala tu hakuna njia nyingine, kama anataka iitwe Serikali ya Chadema, asubiri uchaguzi ujao labda yanaweza kutokea maajabu ya Mussa, ingawa dalili za mvua huwa ni mawingu, yaaani Majuzi Chadema wameshindwa Uchaguzi wa MAdiwani tu, je wataweza Taifa?

Le Mutuz!!

Mwenzio ka quote katiba wewe ume quote wapi,unaagua ?
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom