On Star TV: Ipi Misingi ya Kuendeleza Amani Tanzania?

Nape sijui ka memory card kake ni Kb!???manake hana hata kumbukumbu ya matamshi yake ya nyuma!....
 
SWALI KWA NAPE:

Anataka ushaidi gani juu ya Polisi kuhusika mauaji Nyololo wakati watanzania tumeshuhudia wazi Polisi akilenga tumbo na kumsabaratisha utumbo David Mwangosi pale Nyololo?

Na kama si hiyo mbona vyombo vya habari leo vimetangaza kuwafikisha kesho Askari Polisi watano Mahakamani waliohusika na mauaji hayo?
 
Mbona Nape anapata hasira za kijinga kihivyoooooo kwa uongo wa mchana wakati picha zipo
 
Nape yupo kwenye shuguli ya kuua chama chake.

Atafanikiwa, kwani hayuko peke yake. kila anayejifanya kuipenda CCM ataiua mda si mrefu. wako wengine kama Magufuli, Nchemba, Lusinde, Kigwangala, Wassira, Kikwete, na wapuuzi wengine
 
kwa namna hii naona kuna agenda imepangwa na watu fulani au kikundi fulani kuhakikisha mtu anauawa kwenye kila mkutano au maandamano ya CHADEMA ili kuuaminisha umma kwamba chadema wanahatarisha amani
 
Nape anaogopa JF hawazi tia mguu hapa kujibu haya maswali.

Alafu hivi Nape asili yake ni mweupe au mweusi kila mara anabadilika rangi
 
Bwana Yahya Mohmed,

Ushauri wangu ni kuwa jambo hili linahitaji mjadala mrefu na wa kutosha kwahiyo ni bora mkatenga muda maalum hata wa masaa 3 na kualika wadau wote ili watu watoe mawazo yao na kuelezea duku duku zilizoko moyoni mwao.

Mwisho Nape atueleze ni kwanini rais wa nchi mpaka leo yuko kimya kanakwamba hili tukio ni jambo dogo. Pili Nape tueleze ni kwanini mpaka leo hakuna aliekamatwa.

Naamuliza kwasababu yeye ni kiongozi wa chaman na ndo kimeshika dola. Chama kama chama kimeshauri nini serikali juu ya hatua za kuchukua. CCM ikishauri ina nafasi kubwa ya kusikilizwa ila kama mmekaa kimya basi hiyo ni ajenda ya chama na serilkali yenu.

Nape tuambie nani anaua, ni CHADEMA au polisi?

Ni kwanini mauaji yanatokea pale tu polisi wanapovamia.

Mjiulize, mbona maanadamano ya waislamu yalikuwa salama licha ya kuwa hayakuwa na kibali?
 
Naomba kumuuliza bwana Nape Nnauye:

Kwanini CCM inahubiri amani kwa nadharia huku ikilitumia jeshi la polisi kuvunja amani hata kwa kuua kwa vitendo zaidi? CCM haioni kwamba inamkosea hata mungu kwa kuwavalisha watanzania mapazia?
 
Swali kwa Lissu:
Ni utaratibu upi wa kisheria unafaa kufuatwa hasa katika wakati huu wa uchunguzi wa kesi za kuteswa kwa Dr Ulimboka na kuuawa kwa Mwandishi ambapo watuhumiwa ni Polisi, wachunguzi ni Polisi na wapelelezi ni Polisi haohao? How is this possible katika upatikanaji wa HAKI?
 
ni nini tofauti ya Lusinde,Mwigulu Na Nape?
badala ya kuongea hoj,anabwabwaja na kutukana.

Nape,unasema chadema ni masikini,swali.
kama unalijua hilo kwanini msiwaache wafanye mikutano yao ya kimasikini?
hadi muwaue,muwapige mabomu..

kama wangekua na hela kama nyie wangeenda gurdoto..waacheni basi!
manake umasikini wao wameridhika nao,nini kinawakera?kihoro cha nini sasa?
 
Nape wewe ndiyo mwongo si Tundu Lissu. Kwa sisi wanasaikolojia tunaangalia hata facial expression mbona una hamaki? Halafu unasema Zanzibar sensa ilikuwa imekamilika mbona ongezeko la muda haukulenga Tanzania bara.

Nape wewe ni kijana acha ushabiki wa CCM unajimaliza kisiasa na kimadili mbona unatetea mauaji ya polisi unafurahia kuua kwa vile tu mnataka CCM iendelee kutawala?
 
Nape tunaijua hii nchi kuliko wewe. Manyanyaso yako chini na si kwenye ripoti unazoletewa
 
Nape pole sana kwakukutana na mtaalamu Lisu na umshukuru huyo host wa Dar asiyejua kuongoza kipindi

Tena ana bahati ya mtende huyo mtangazi mdada amepwaya sana,angekutana na mtu kama massako wa itv lazima angejam pa,tehe tehe teheee..
 
Nape kwa matendo yenu ya kubaka demokrasia ya watnzania na hata kuwazuia wananchi kujiamulia chama wakipendacho si ni ishara kwamba CCM ni chama cha upinzani dhidi ya chaguo la wananchi CHADEMA??
 
ni nini tofauti ya Lusinde,Mwigulu Na Nape?
badala ya kuongea hoj,anabwabwaja na kutukana.

Nape,unasema chadema ni masikini,swali.
kama unalijua hilo kwanini msiwaache wafanye mikutano yao ya kimasikini?
hadi muwaue,muwapige mabomu..

kama wangekua na hela kama nyie wangeenda gurdoto..waacheni basi!
manake umasikini wao wameridhika nao,nini kinawakera?kihoro cha nini sasa?

Natumia mchina mkuu,kula LIKE ya nguvu,hana hoja huyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom