On Star TV: Ipi Misingi ya Kuendeleza Amani Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

On Star TV: Ipi Misingi ya Kuendeleza Amani Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Star TV, Sep 9, 2012.

 1. Star TV

  Star TV Verified User

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibuni tena siku ya leo WanaJF kwenye kipindi chetu cha Watanzania Tuongee Asubuhi.
  Mada yetu ya leo inahusu ni ipi misingi ya kuendeleza amani Tanzania.

  Host Mwanza: Yahya Mohamed
  Host DSM: Joyce Mwakalinga

  Wageni wetu Dar:
  Bwn. Nape Nnauye
  Bwn. Juju Danda
  Mh. Tundu Lissu

  Wageni wetu Mwanza:
  Donald Kasongi

  VIDEO YA KIPINDI:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tunakaribisha Maswali na hoja za mapema zaidi ili twende sambamba wakuu
   
 3. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Swali,kwa nape ccm wanashutumiwa kulitumia jeshi la polisi kwa remoti kudhibiti mikutano ya vyama vya upinzani ambavyo vinaonekana kuwa na nguvu ,kama tlp,cuf na sasa chadema,haoni kama ccm inaleta vita nchini?
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  swali kwa Nape Nnauye'je ccm ipo tayari kuachia madaraka kwa amani kama itashindwa uchaguzi ujao???swali kwa Tundu lisu'je madai yaliyotolewa na Samweli Sita kwamba Chadema haina watu wa kuongoza serikali'je ni keli???
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hi, Mada nzuri Yahya, kwa kuwa hakuna kinachoweza kufanyika kama hakuna amani

  Nadhani msingi mkuwa wa amani ni usawa na haki. Usawa katika ugawaji wa rasilimali, usawa katika demokrasia, usawa katika elimu na katika kila nyanja ya maisha na maendeleo.

  Kunapokuwa na double standards amani haiwezi kuwepo, kunapokuwa na kuonewa amani ni ndoto. Kunapokuwa na wengine kuneemeka, wengine wakipunjwa amani mtaisikia kwa wenzenu.Wengine wanajichotea mapesa ya nchi na kuyaficha uswisi wengine hata mlo wa siku hakuna, amani haiwezi kuwepo. Wengine wanachukua ardhi ya nchi tena kwa kupora wengine, tusitegemee amani hapo.Chadema wananyimwa kufungua matawi, CCM wanazindua kampeni amani itapatikana wapi.Usawa na Haki ndio vitaleta amani.

  Swali kwa Nape, anazungumziaje kutotii sheria kulikofanywa na CCM kule Bububu kwa kufanya mkutano licha ya katazo la Polisi? Na mbona hawakuchukuliwa hatua yoyote?
   
 6. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Amani ya kweli katika nchi yetu itajengwa na kudumishwa pale tu viongozi wa CCM watakapo acha kabisa hila na utawala uliojaa rushwa, ufisadi na udanganyifu, Nape aache mara moja kuropoka na kutetea uongo na udanganyifu.
   
 7. B

  Baba Kimoko Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nape ana uheshimiwa gani?
   
 8. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CCM imekuwa ikitumia dhana ya amani na utulivu kuwatia hofu na kuwatisha wananchi wasidai haki, na wasishiriki kwenye shughuli za kisiasa kwa uhuru. CCM inataka kuficha hofu yake ya kuondolewa madarakani kwenye kichaka cha AMANI NA UTULIVU na matumizi ya mabaya ya nguvu za dola hasa JESHI LA POLICE.
   
 9. M

  Milton Mponda Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Misingi mikuu ya amani ni utoaji haki ulio sawa hasa haki ya kuishi ambayo tunaona kila uchao inavunjwa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wao.

  Haki ni neno pana linalojumuisha vitu vingi sana kama vile haki ya kujieleza (democratic country), haki ya kupata mahitaji ya msingi ikiwemo chakula, malazi, mavazi, elimu, afya na huduma nyingine za kijamii.

  Kwahiyo hivyo vitu nilivyotaja vikikosekana amani katika nchi itakuwa na mashaka na ipo siku itajidhihirisha hivyo.
   
 10. F

  FENI Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Swali kwa Nape: Je, njia ya kumsughulikia mkosaji ni kumtoa roho?
   
 11. S

  SILENT GUNNER Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini CCM imekuwa ikitumia Jeshi la polisi kama 'bullet proof jacket' Panapotokea mauaji yanayoigusa moja kwa moja CCM (mtawala) na kufanya dhana nzima ya amani kuonekana imehodhiwa na CCM kama chama tawala?

  Na nashangaa kuona CCM imekuwa ikiimba sana kuwa mtunza amani wakati ndio wamekuwa wakikatisha maisha ya watu kwa makusudi!
   
 12. S

  Sayfulhaq Senior Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Pamoja na mambo mengine Amani huletwa kwa yafuatayo:
  1) Kila kundi jamii litendewe kiusawa na isionekane kundi fulani linapendelewa dhidi ya kundi lingine
  2) Uvumilivu wa kisiasa na hata itikadi
  3) Rasilimali za nchi zitumike kwa ajili ya manufaa ya wananchi.
   
 13. B

  Baba Kimoko Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nape anyooshe maelezo, awache spin. Tanzania kuna wajibu wa kulazimishwa na hii imetokana na polisi ya Tanzania kutumika vibaya na serikali iliyopo madarakani.
   
 14. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Nimemsikiliza Nape anazungumzia kwamba ili kudumisha amani, ni lazima kuhakikisha haki inazingatiwa. Yeye amekuja na lake kuwa, haki inaendana na wajibu na kusema kuwa wengi hatupendi kulizungumzia wajibu. Sidhani kama ana mifano kwa kurejea uvunjifu wa amani uliofanywa na vyombo vya dola HIVI karibuni, vinavyosimamiwa na CCM.

  Jana pia nilimsikia WASSIRA akiwalaum wana CHADEMA kwa kutokukubaliana na ILANI LA POLISI WA CCM, alichokuwa akijaribu kusema ni kuwa mauaji yanayotokea ni majibu sahihi kwa watu wanaokaidi amri ya Polisi.

  Lakini tuje kwenye ukweli; NAPE ATOE JIBU: Haki za kiraia ni zipi NA wajibu wao ni upi katika haki hizo?
   
 15. C

  CHIEF MVUNGI Senior Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kumuuliza Nape kuhusu madai yake ya kwamba CHADEMA wanaiuza nchi kwa kwenda kuomba misaada nje ya nchi, je ni ya kweli haya?
   
 16. Stanley.

  Stanley. JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Swali: Je Tanzania tunayoitaka ndio hii?
   
 17. B

  Baba Kimoko Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jibu jepesi sana. Kwani stop order ilitolewa Tanzania Bara pekee au Tanzania nzima?
   
 18. M

  MALAGASHIMBA Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Yahya, mada nzuri, lakin kuweni makin na hizi mada na watangazaji (host) wanaotakiwa kuendesha.

  Mtangazaji (host) wa Dar anapwaya, mada ni nzito kwake!
   
 19. gody

  gody JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,227
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Yahya naomba kumuuliza Nnauye kama ifuatavyo:

  Kufungua tawi Nyololo 'NO' sababu kuna sensa, ila Fiesta Mwanza YES... Na waislam Dar wameendamana bila kibali na wamelindwa na polisi!

  Hii inakuwaje?
   
 20. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nape, kusema Zanzibar sensa ilikamilika ni kutudanganya watanzania, lile katazo lilikuwa la nchi nzima, halikuhusu bara pekee, kwanini usikubali kwamba mlivunja sheria?

  Na hizi ndio double-standards ninazozizungumzia.
   
Loading...